Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Tumeshawasili tunataka challenge na sisi wa Mkunya
20230518_081548.jpg
 
MUENDELEZO SEHEMU YA 2

"Ngo ngo ngo!" Mlango wa nyumba yangu ulikuwa ukigongwa. "Ni nani mwenzangu?" niliuliza. "Ni mimi mzee Kingalu nina shida na wewe mara moja!" Nilitoka na kushangaa kwa nje kulikuwa na mwanga mkali sana wa jua, kumbe ilikuwa ni saa nne asubuhi, nimechelewa kazini isivyo kawaida yangu. Mzee Kingalu alikuwa ameongozana na mwenyekiti wa Kijiji, niliwasalimia huku nikionyesha wasiwasi mkubwa, wala hawakujibu salamu hiyo walinidakisha kwa maneno.

"Kijana wewe ni mwalimu wetu na umeletwa ili uwasaidie watoto wetu kielimu, hatuwezi kuvumilia watu wachache wasio kuwa na nia njema waweze kukukatisha tamaa na kukuharibia maisha yako ya sasa na ya baadaye, tumepata taarifa kuwa ile kinga tuliyokupa imeporwa, je kuna ukweli gani kwenye hili?"

Wamewezaje kufahamu kwamba ile kinga imeporwa ijapokuwa sikuwaambia, niliwaza moyoni. "Ndio!" Nilijibu na nikawaelezea kuhusu ile ndoto niliyoiota usiku wa jana kuamkia siku hii ya leo.

"Ndio swala hilo tunalijua, kuna wazee walikuja kwako usiku huu kwa lengo la kukudhuru sisi tulifanya juhudi kubwa kuwazuia na ndio maana tupo hapa saa hii kwa sababu hatupendi kukukosa," alimalizia mzee Kingalu kisha kuingiza mkono wake kwenye mkoba mweusi aliokuja nao na kutoa kichupa cheusi. Alinipa kichupa cheusi chenye mafuta yaliyochanganywa na mavumba fulani, mafuta hayo yalikuwa ni mafuta ya mbarika na mavumba ni majivu ya mchanganyiko wa vingira fulani vya kichawi. alinishauri niwe napaka utosini kila usiku ninapotaka kulala.

Nilijiandaa haraka na kuelekea shuleni nilipofika wala hakuna mtu yeyote aliyeniuliza kitu chochote ama kushangazwa na kuchelewa kwangu kazini kwa sababu ilikuwa ni jambo la kawaida kwa wafanyakazi kuchelewa, mimi sikutaka kujiingiza kwenye mkumbo huo ni siku hii tu nilichelewa bila hata mwenyewe kutarajia.

Mwalimu mwenzangu wa kike aliyeitwa Siti ndiye pekee aliyenihoji na nilimpa jibu moja tu la mkato kwamba aniache kidogo kwani kichwa changu hakipo sawa kwa wakati ule, nashukuru alinielewa. Alinitia moyo sana binti yule, alikuwa ndiye rafiki yangu kwa wakati ule kwani hata ki umri tulikuwa hatujapishana sana tofauti na walimu wengine waliokuwa ni watu wazima kutuzidi sisi. "Soka wewe ni mtoto wa kiume, hapa kijijini umekuja kikazi japo ninakuonea huruma lakini huna budi kujifunga mkanda."

Nilimsikiliza na kuwaza moyoni, mbona haya maswahibu mwenzangu hayampati? Baadaye nilikuja kugundua kuwa yeye mahali napoishi ni nyumba ya Mganga mkuu wa kienyeji pale kijijini, na alikabidhiwa pale na baba yake mzazi kwahiyo wachawi wengi wa pale kijijini Kwamsisi walikuwa wakiogopa kumfanya chochote.

ITAENDELEA...
Ukiendelea naomba unitag K11
 
Itaendelea lini?
 
Back
Top Bottom