Sitosahau siku niliposhuhudia watu wakipigwa mashoka

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,220
1,878
Ni jioni Moja nipo iliotulia nipo viunga vya home salasala dar, mwaka 2004.

Hio siku ndio nilishuhudia Kuna watu makatiri Duniani, kuna mnaokumbuka ule wimbo wa salasala Godzilla Yale matukio yalioimbwa mengi ni kweli kabisa.

Sasa palikua na kikundi Fulani walijiita chafosa wao ilikua ni kukaba kuiba na ukorofi wa hapa na pale
Wale jamaa pia walitumia wanawake kwenye kutimiza azma yao hio kwa maana ukitongoza unakubaliwa freshi mnaingia kama ni gest au mpo bar.

Ndio mmoja wa wale vijana wa chafosa huja na kujidai ni mkewe wamekufunia huja wengi kukupiga na kukupora Kila kitu.

Sasa hio siku waliingia cha kike, una muuza butcher mmoja alikua anauza nyama hapo salasala ni mgeni kidogo kama kawaida chafosa wakatega mtego wao ukafanikiwa.

Wakaenda na yule binti bar ya hapo center kipindi wanapiga urabu na yule demu ndio hao chafosa wakatokea
Bana we wakampiga pale mgogo yule na kumyang'anya pesa zote za mauzo ya butcher siku hio.

Yule mgogo akawa mpole akajifanya anaondoka , kumbe bana alienda butcher akachukua kishoka Cha kukatia nyama.

Kilichofuata hakisimuliki , ndio niliona Hawa jamaa Kanda ya kati ni majasiri kuliko mura

Ebwanaee vilitembea vishoka kwa wale vijana ni mwendo wa viwiko Cha mgongo walikimbia Ile mbayaaa

Yule mgogo baada ya kufanya yake alitoweka ghafla Hadi Leo hakupatikana

Hapakua na vifo Bali ni majeraha makubwa. Nawaasa ndugu zg kua makini na baadhi ya wanawake wengine ni mtego huo.

Kwa wale wanaoendelea kusoma historia yg ya maisha ya kweli nimeshusha epsod nyingine zaidi ya 5 Haina mkwamo wala twende telegram.

Story yg inaenda kwa jina jinsi maamuzi ya mzazi yanavoweza kuathiri afya akili ya mtoto , nimeongelea mengi jinsi baba alipouza Mali zg zenye thamani ya million 20 na kutokomea mkoani huku akiniacha ninaumwa nimelazwa hospital.
 
Back
Top Bottom