Sitashangaa "VOTE OF NO CONFIDENCE" ikapigwa kabla ya 2015...

Mh! Mbona kwa mlolongo huo wa sheria, kuna hatua nyingi sana kufikia hatua ya vote of no confidence. By the way, this can be just the begining, there might be many more to come, let us see what will happen on this Jairo's saga.

Mkuu ni mlolongo mkubwa mno ambao kwa watu wa magamba sidhani kama wana utashi wa kufanya hayo

Kwa mujibu wa mtazamo wangu wa hali ya siasa na bunge katika bunge hili la kumi, nadiriki kusema kwamba sitashangaa sana kama kabla ya mwaka 2015 bunge likaomba kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali hii.

Serikali watch your back you are running solo and soon you will meet an hungry Lion, believe me it wont leave you
Mkuu nchi gani hiyo unayoongelea? Kama ni Tanzania, basi hizi zitabaki tu kuwa ni day dreams. Hakuna kitu kama hicho kwa nchi na wananchi mazuzu kama watanzania.

TF uko kama mimi hii kitu siamini na haitotokea

Ngoja niweke hapa kifungu cha katiba uone mlolongo ilivyo mrefu na ambao magamba hawatakubali hata tone

46A]46A. Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria Na. 20 ya 1992 ib. 8; 12 ya 1995 ib. 4

(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais–

(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba; au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama–

(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekeza kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;

(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani–

(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;

(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar; na

(c) Wabunge saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.

(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashtaka yaliyotolewa dhidi yake.

(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuundwa, itakaa, ichunguze na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.

(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.

(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

Rocky imenibidi kucheka tu maana kwa katiba hii na kwa staili hii watu wataendelea kupeta kama kawa huku sisi tunapiga kelele za vijiweni

Rocky imenibidi kucheka tu maana kwa katiba hii na kwa staili hii watu wataendelea kupeta kama kawa huku sisi tunapiga kelele za vijiweni

Mkuu huo mlolongo waliouweka ni balaa na wanajua kabisa kule bungeni majority ni nani na je kuna mwanamagamba atakayeunga mkono hoja hata mmoja
Na je akiunga mokono maisha yake na siasa si ndio itakuwa mwisho
Vipi kuhusu biashara zake na mali zake na usalama wake yeye mwenyewe
Kwani hajipendi

Kwa maoni yangu inawezekana. Wabunge wa ccm wasipofanya hivyo, watapoteza majimbo yao kwa 90% come next election.

Mkuu huo mlolongo waliouweka ni balaa na wanajua kabisa kule bungeni majority ni nani na je kuna mwanamagamba atakayeunga mkono hoja hata mmoja

Na je akiunga mokono maisha yake na siasa si ndio itakuwa mwisho

Vipi kuhusu biashara zake na mali zake na usalama wake yeye mwenyewe

Kwani hajipendi

Mkuu hapo ni ukweli maana wao huwa wanawaza maslahi binafsi nafikiri cha msingi uchaguzi ujao ni kupunguza idadi ya wabunge wa CCM bungeni

Mkuu hapo ni ukweli maana wao huwa wanawaza maslahi binafsi nafikiri cha msingi uchaguzi ujao ni kupunguza idadi ya wabunge wa CCM bungeni

tunahitaji kama kweli tungependa tuwe na maamuzi magumu na uwajibikaji kw aviongozi na watendaji mbalimballi ni kuwa na wabunge wengi wa upinzani bungeni
Viongozi wakuu kuanzia waziri mkuu na wakurugenzi wote na majaji wote wathibitishwe na bunge ambalo pia litakuwa na uwezo wa kumtimua atakapoboronga
Tuache huu mtindo wa waziri ni mbunge hapo hapo hauna tija na wathibitishwe na bunge pia hata wakiteuliwa na rais
na madaraka ya rais yapunguzwe sana asiwe kama mfalme kweney nchi ambako tunajiita tuna democrasia

Tatizo jingine Rocky ni asilimia chache ya Watanzania wanaoijua katiba ya nchi hii nalo pia ni tatizo

Kama tungekuwa na wabunge wenye akili za kutosha hasa kutoka chama tawala, vote of no confidence to thr GVT ingeshapigwa maana nchi hii imepoteza mwelekeo siku nyingi. Lakini kwa kuwa wazee na mabibi wa kuunga mkono hoja ndo wengi, hata ikitolewa leo hii, itapingwa vikali na wabunge wa CCM kwa maslahi ya yao binafsi na si wananchi waliowatuma. Hata hivyo naamini mabadiliko yanaendelea kutoa na punde kuna wimbi la mageuzi laja katika nci yetu. hata kama hawataki kukubali nakuuona ukweli zaidi ya viapo vyao vya chama, mwisho wa siku tutawapiga mawe ili akili ziwarudi kwa nguvu
Kwa mujibu wa mtazamo wangu wa hali ya siasa na bunge katika bunge hili la kumi, nadiriki kusema kwamba sitashangaa sana kama kabla ya mwaka 2015 bunge likaomba kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali hii.

Serikali watch your back you are running solo and soon you will meet an hungry Lion, believe me it wont leave you

Jamani mi nakubaliana na nyinyi kabisa kwamba kwa mtazamo wa haraka hili haliwezi kutokea kwa nchi hii, but kwa mtizamo wa kina na uchambuzi yakinifu mlolongo huu waweza kuwa mfupi sana. Nitawapa mfano, hakuna watu waliokuwa watiifu kwa serikali kama waarabu lakini when it came to the point of "nothing else" they reacted and we all know the reaction pamoja na kwamba leo hii ukiwauliza kwa mfano watu wa Libya unaweza ukasema they are stupid kwa yale yote yaliyokuwa yamefanywa na serikali ya Gaddafi. So i was just tryna see kwa mtizamo mpana zaidi ya huu tulionao sasa maana politics changes kwa kasi sana

Tatizo jingine Rocky ni asilimia chache ya Watanzania wanaoijua katiba ya nchi hii nalo pia ni tatizo

Mkuu ningekuwa mimi ni mwenyekiti au kiongozi wa chama ningefanya kazi kubwa sana ya elimu ya uraia watu wajue haki zao wajue wajibu wao waijue katiba ya nchi
Mamlaka ya rais ni yapi
mku wa mkoa ni yapi
Mbunge ni yapi
na wanapaswa kuidai nini serikali yao
Sio kujengewa hospital waone kama serikali imewasaidia au wanaiomba serikali wakati wanalipa kodi zao
Wajue ni haki yao kujengewa hospital na serikali kama wanalipa kodi na kutekeleza kile wanachoambiwa na serikali

Mr.Rocky ebu tucheki tuone hizi sindimba za wana-ccm,yani wanatia kinyaa na wametufika kooni kwakweli
shida ingine ni wanataaluma walioshika izo nyadhifa serikali yani wamelewa pesa na wote washenzy tu

Mkuu ni ngumu sana kwa siasa za wanamagamba kufanya maamuzi mazito na sijui ni nani atakayekuwa tayari kufanya au kujitosa kufanya maamuzio hayo

Back
Top Bottom