what if badala ya kupiga kura ya vote of no confindence, wabunge watawashawishi wananchi kuingia street? Hii itamwathiri nani?
Wabunge wapi hao mkuu wenye guts hizo
hawa hawa wa magamba siamini kama wanaweza kufanya hayo
Wabunge wote bila kujali itikadi! Wawapatie wananchi data za kutosha, kisha wao wakae nyuma kwa kuhofia vyama vyao kuwawajibisha...kisha mwendo mdundo! Jamii itaishinikiza serikali kwa mbinu zote ili iheshimu utawara bora
Jamani kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia mienendo ya mabunge ya Tanzania hata ukichukulia mfano wa bunge lililopita tu la tisa utagundua kwamba hata hao wabunge wa CCM nao wanasoma alama za nyakati.
Mtakubaliana na mimi kwamba hivi juzi tu wakati bunge la kumi linaanza hakuna hata mbunge mmoja wa CCM ambaye angemuunga mkono Zitto wakati anatoa hoja ile lakini kwa walioona hii asubuhi watakubaliana na mimi kwamba NOTHING LASTS FOREVER
Wabunge wote bila kujali itikadi! Wawapatie wananchi data za kutosha, kisha wao wakae nyuma kwa kuhofia vyama vyao kuwawajibisha...kisha mwendo mdundo! Jamii itaishinikiza serikali kwa mbinu zote ili iheshimu utawara bora
TF uko kama mimi hii kitu siamini na haitotokea
Ngoja niweke hapa kifungu cha katiba uone mlolongo ilivyo mrefu na ambao magamba hawatakubali hata tone
46A]46A. Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria Na. 20 ya 1992 ib. 8; 12 ya 1995 ib. 4
(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba; au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekeza kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar; na
(c) Wabunge saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.
(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashtaka yaliyotolewa dhidi yake.
(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuundwa, itakaa, ichunguze na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.
(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.
(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.
(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
Inawezekana kuna technical error kwenye report ya CAG ama inawezekana mtoa hoja alitumika ili kupoza joto la hoja za umeme na mafuta zilizokuwa zinaibana serikali kipindi kile...., lakini Watanzania wanajua na wanafuatilia kila kinachojiri.
Haiitaji mnajimu kutabiri hatima ya haya matukio.
Wanajua haya yote..tatizo wamelishwa unga wa ndele..wengi wao wa CCM wameacha akili na utashi wao pale Lumumba na Dodoma makao makuu..wakiingia bungeni wanakua kama mazombi...
Jamani mi nafikiri wabunge wa CCM sio wajinga kiivyo kwamba hawawezi hata kusoma alama za nyakati i am just trying to see the fast change of this bunge, its not the same even when this budget session started na leo linapoelekea kwishaWabunge wapi hao mkuu wenye guts hizo
hawa hawa wa magamba siamini kama wanaweza kufanya hayo
Kwa wabunge hawa wa magamba, walioitwa na Jairo kuwa Ze Comedy, SIDHANI..................Kwa mujibu wa mtazamo wangu wa hali ya siasa na bunge katika bunge hili la kumi, nadiriki kusema kwamba sitashangaa sana kama kabla ya mwaka 2015 bunge likaomba kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali hii.
Serikali watch your back you are running solo and soon you will meet an hungry Lion, believe me it wont leave you
Jamani kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia mienendo ya mabunge ya Tanzania hata ukichukulia mfano wa bunge lililopita tu la tisa utagundua kwamba hata hao wabunge wa CCM nao wanasoma alama za nyakati.
Mtakubaliana na mimi kwamba hivi juzi tu wakati bunge la kumi linaanza hakuna hata mbunge mmoja wa CCM ambaye angemuunga mkono Zitto wakati anatoa hoja ile lakini kwa walioona hii asubuhi watakubaliana na mimi kwamba NOTHING LASTS FOREVER
Hiyo ilikuwa inaonyesha msisitizo tu kidogo wala haina maana yoyoteMkuu hiyo rangi inamaabisha sasa wameanza kukomaa na fikra zao zinageuka kuwa pevu!!!!! la vote of no confidence lawezekana!!!!!
VUGUVUGU LA MABADILIKO YA KISIASA NI KAMA MAJI USIPOYANYWA UTAYAOGA, USIPOFULIA UATAPIKIA NK. It is unkwepable!!!!!!