Sitasahau nilivyonusurika kuuliwa kinyama na baba yangu mzazi

KISIWAGA kuna baba mmoja tajiri alifiwa na mke wake na kumuachia mtoto mmoja wa kiume. Alimlea yule mtoto kama single father lakini alimpenda sana. Alikwenda nae business trips Nairobi hata Afrika Kusini.

Mtoto alikua mjanja na mwenye akili sana. Alipofika secondary alimpeleka boarding school. Mzee alianza kuwa mpweke. Pale ndiyo wazo la kuoa lilimjia.

Mke mpya alijaliwa mtoto wa kiume. Roho ilimuuma alipoona mume wake anaongea na yule mtoto mkubwa mambo mengi ya biashara na mali.

Alipanga kumuua yule mtoto. Alikodi watu na kuwapa pesa wamteke mtoto na kumuua. Wale wauwaji walitokea kumpenda yule mtoto kwakua alikua very gentle man.

Mmoja alimtorosha kwa ahadi kuwa asirudi nyumbani kwao, alimpa mchongo mzima.

Mtoto alikumbia mpaka pumzika ikaanza kukata. Alipata wazo la kwenda polisi. Aliwaeleza polisi kila kitu. Polisi walimfuata baba yake na kumueleza.

Kama siku za za kufa bado utapona tu.
 
Nakumbuka mwaka 2001 enzi hizo bado niko shule ya msingi katika mji mmoja hapa Tanzania baba yangu ambae alikuwa ni mfanyabiashara wa toka enzi za Nyerere na aliyekuwa kwa kipindi hicho akiitwa tajiri alitembelewa na mganga mmoja wa kienyeji kutoka mahali pasipojulikana

Alimpokea na kumchukulia chumba kwenye gest moja ya bei mbaya wakati huo.Mganga huyo alikaa kama siku 3 hivi hapo gesti na kila siku alikuwa akija nyumbani ambako baba alimkaribisha kwa heshima kwelikweli na walifanya mazungumzo ambayo mimi sikuyatilia maanani

Basi wiki moja baada ya yule mganga kuondoka baba alifanya vitu ambavyo ni kama tulikuwa hatuvihelewi helewi,alifanya vitendo ambavyo ni kama vile alikuwa akitaka nife tena haraka sana

Nakumbuka kuna siku nikiwa chumbani kwangu mida ya saa mbili usiku baba alikuja ghafla akiwa kabeba bunduki yake na kuniambia kuwa amesikia kama kuna wezi wameruka geti huko nje anakoegesha magari yake hivyo mimi niende nikaangalie yeye atakuwa nyuma kama nikikuta kweli kuna wezi niingie chini ya uvungu wa gari haraka yeye awatwange wale majambazi risasi

Basi kwakuwa nilikuwa mdogo na nilikuwa siwezi kubishana na baba yangu nilifuata maagizo yake, nilifungu mlango mdogo nikatokea huko nje ya maegesho ya magari nikapiga hatua za tahadhali kusogea mbele lakini ghafla sijui nini kilinishtua kugeuka nyuma du nikakuta mzee kaielekeza bunduki yake usawa wangu,nikalala chini fasta huku wakati huo huo baba akifyatua a risasi ambazo hazikunipata.Niwe muwazi pamoja na umri wangu mdogo ila nilishangazwa sana na kitendo hicho cha baba ila nilihisi huenda labda alipiga zile risasi kwa sababu ya uoga hiyo siku ikaisha



Baada kama ya siku tano nikiwa bado sijasahau kilichotokea kule kwenye marisasi ya baba,baba alianzisha special operation nyingine ya kuhakikisha natoweka kwenye uso wa Dunia haraka iwezekanavyo hata kama NATO hawatamruhusu.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumamosi mida ya saa 3 na ½ baada ya kunywa chai kwa machapati baba aliniita tena akaniagiza nibebe box la spana nipeleke kule kwenye maegesho yetu ya gari.Basi nilikwenda stoo nikabeba hilo sanduku na kulipeleka kule kwenye maegesho ya gari zetu ambako nilimkuta baba akiwa tayari keshafungua mlango wa gari,yale malorry ya kizamani ambayo siwezi kuitaja model yake ili kuwaepusha watu kuunga Dot na kunigundua ubin wangu kwani baba alikuwa ni mtu mashuhuri kwenye huo mji wetu, akaniagiza niweke lile sanduku pembeni nami bila hiyana nikafanya kama alivyoniambia kazi ikaanza

Kiukweli siku hiyo sikumuelewa baba alikuwa anataka kufanya marekebisho gani kwenye hilo lilorry letu la kizamani ambalo kama lingekuwepo mpaka leo tungeliita moskova(meli ya urusi iliyozamishwa kwa makombora ya Ukraine kule bandari nyeusi) maana lilifanya kazi kwelikweli toka mwaka 1971 liliponunuliwa

Basi ilikuwa mara afungue bonnet na kupima oil,mara apige jeki,mara awashe weiper,niwe muwazi nilianza kuingiwa na wasiwasi juu ya ufundi wa leo wa baba ambaye alikuwa ni fundi makenika hatari baada ya kufanya kazi kwenye viwanda vya mkoloni kama kibarua upande wa magari

Ghafla ikawa kama vile amepata wazo jipya akachukua kigunia vile vya zamani vya mkonge akalaza kwenye uvungu wa gari usawa wa gear box akajilaza pale akijitia kugusa hiki na kile mwisho akasimama na kuniagiza nilale pale chini kwenye kigunia nimshikie hiyo gear box yeye anaingia ndani ya gari kuirekebisha nami nikafanya kama nilivyoelekezwa

Baba huyoo akaingia ndani akaanza kuniuliza je inatikisika nikamjibu ndio akashuka kutoka ndani ya gari na kujifanya kama anaitazama ile gearbox kumbe alikuwa akiangalia kama kweli nimekaa usawa ule ule alioniacha akarudi kwenye gari tena

Aliporudi kwenye gari akajifanya kuitikisa tikisa akashuka tena akakuta bado niko pozi lilelile akaniambi niendelee kuishikiria na yeye akarudi ndani ya gari

Sijui ni nini kilinikumbusha kuwa kuna siku niliona gearbox huwa inashushwa huko huko chini nilikolala na kwa jinsi nilivyo bado mdogo sikuwa na uwezo wa kuizuia isishuke,fasta nikasogea pembeni na wakati huo huo gearbox hiyoo puu mahali pale pale nilipokuwa nimelala usawa wa kifua changu

Mara baba huyo akashuka kutoka ndani ya gari jicho kama la kujilaumu likiwa limemtoka akachungulia kwenye uvungu wa gari akanikuta niko pembeni na lirocket/ ligearbox lake likiwa chini bila kunizuru nikamsikia akisema kwa sauti ya chini aisee mungu kweli yupo


Basi akaniambia nitoke chini ya uvungu wa gari na akasema alijisahau kunitaka nitoke chini ya uvungu wa gari ila anamshukuru mungu kaniokoa

Huo ndio ukawa mwisho wa baba kuyawinda maisha yangu na mwanzo wa kufulia kwake sijui kama anajua kuwa nilimgungua kuwa alitaka kunitoa kafara tena bila ganzi ila baba bwana kwa kupenda hela wachaga wanasubiri
Sema mwanangu ww mbinafsi kichizi. Yani umeshindwa kujitoa ili familia iishi kitajiri?
 
KISIWAGA kuna baba mmoja tajiri alifiwa na mke wake na kumuachia mtoto mmoja wa kiume. Alimlea yule mtoto kama single father lakini alimpenda sana. Alikwenda nae business trips Nairobi hata Afrika Kusini.

Mtoto alikua mjanja na mwenye akili sana. Alipofika secondary alimpeleka boarding school. Mzee alianza kuwa mpweke. Pale ndiyo wazo la kuoa lilimjia.

Mke mpya alijaliwa mtoto wa kiume. Roho ilimuuma alipoona mume wake anaongea na yule mtoto mkubwa mambo mengi ya biashara na mali.

Alipanga kumuua yule mtoto. Alikodi watu na kuwapa pesa wamteke mtoto na kumuua. Wale wauwaji walitokea kumpenda yule mtoto kwakua alikua very gentle man.

Mmoja alimtorosha kwa ahadi kuwa asirudi nyumbani kwao, alimpa mchongo mzima.

Mtoto alikumbia mpaka pumzika ikaanza kukata. Alipata wazo la kwenda polisi.
So what?
 
Tobaa huyo labda ni step dad, mzazi kabisa? Aisee wababa wanavopenda watoto wao🤔
I'm not attacking you.
Lakini wewe umelelewa na wababa wangapi na kufanya tafiti pia kuchukua sample za kutosha mpaka uje na conclusion kama hiyo?

Kama umelelewa na baba mmoja basi trust me nikisema una'generalize na kujiongopea, ulimwengu ni mpana sana bi'dada.
 
Nina msemo wangu nasema kwamba "ni bora usizaliwe kabisa kuliko kuzaliwa na mzazi asiyejitambua."
Kama wewe unajitambua una mauchafu yako, akili zako hazipo sawa au labda ni kichaa unayetembea na psychopath, basi bora usizae kabisa ukaja kumpa shida na kumtesa huyo mtoto asiye na hatia.

Wewe subiri tu ufe peke yako.
 
Back
Top Bottom