Sitanyamaza, Rais Kikwete na Hili la Masauni Unatania?

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Salehe Mohamed

SITAKI kuamini kuwa Rais Kikwete, aliamua kutoa kauli kuwa atampangia kazi nyingine aliyekuwa Mwenyekiti wa
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hamad Yusuf Masauni.

Masauni inasemekana kuwa alizaliwa mwaka 1973 lakini aliamua kughushi vyeti vya kuzaliwa ambavyo vilionyesha kuwa alizaliwa mwaka 1979 ili aweze kuchaguliwa kwenye kiti hicho mwaka 2008.

Kiongozi huyo alilazimika kuachia ‘maulaji’ ya UVCCM baada ya wenzake kumkalia kidedea kuwa ajiuzulu kwa uhalifu alioufanya kwenye chama hicho kikongwe chenye historia ya kulindana na kubebana.

Masauni angewezaje kukataa kuachia madaraka hayo licha ya kuyataka wakati wenzake waliomsaidia kukalia kiti hicho kwa masilahi yao walimgeuka baada ya ‘bosi’ huyo kushindwa kutimiza kile walichokitarajia?

Sina haja ya kumzungumzia kwa undani Masauni kwa sababu ameshajiuzulu na kwa utaratibu wa chama jambo amesamehewa kwa kuwa hakujua atendalo!

Kilichonikera zaidi ni kauli ya Rais Kikwete kuwa atampangia kazi nyingine Masauni ama iwe ubalozini au serikalini.

Hivi kweli mtu anayedaiwa kughushi na vielelezo vipo wazi ana stahili kupewa kazi na serikali? Huyu ana sifa gani ya uadilifu mpaka amvutie rais.

Binafsi nashawishika kuamini kuwa Masauni, alifanya uhalifu huo, kwa sababu kama hausiki ilikuwaje akakubali kujiuzulu kirahisi namna ile, kwa nini akubali kuchafuliwa jina lake?

Nilitarajia rais Kikwete angekisafisha chama chake kwa kuagiza hatua zaidi za kisheria zichukue mkondo wake dhidi ya Masauni lakini si kumuandalia mazingira mazuri ya kutumia kodi za walalahoi.

Kama Rais Kikwete ameshatamka hadharani kuwa atampangia kazi nyingine Masauni, basi vyombo vya dola kamwe haviwezi kumuwajibisha mtuhumiwa huyo ambaye kwa mujibu wa sheria za nchi ametenda kosa la jinai.

Inawezekana Rais Kikwete alifanya UTANI, kwa sababu ni kawaida yake kufanya utani kwenye masuala nyeti yagusayo mustakabali wa taifa.

Lakini mbona mpaka sasa hajatokea kiongozi wa serikali au wa chama kusema huo ulikuwa utani? Mbona alipowaambia viongozi wa dini kuwa takrima haikwepeki katika mazingira ya sasa tuliambiwa kuwa alifanya utani?

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ndiye aliyepewa jukumu la kuuambia umma kuwa Rais Kikwete alikuwa akitania na hana ubavu wa kuirejesha sheria hiyo iliyochinjwa na mahakama.

Sote tunajua kuwa hakuna aliye juu ya sheria sasa kwa nini Masauni apewe kinga na chama chake pamoja na Rais Kikwete ambaye anamtafutia ulaji?

Kila kukicha wanafunzi wanaoghushi vyeti vya elimu au kuzaliwa ndio wanaopelekwa mahakamani lakini wabunge, vigogo wa CCM wanaendelea kula kuku kwa mrija.

Watakamatwaje wakati kiongozi mkuu wa nchi bado anawahitaji? Tunawezaje kujenga kizazi cha kuwajibika kama sisi wenyewe si wawajibikaji?

Kulindana kunakofanywa na CCM ndiko kunakotufanya tupate viongozi wasio na upeo mzuri pamoja na wenye kujali masilahi binafsi badala ya wananchi.

Leo hii kuna wabunge wameshabainika kughushi vyeti vya elimu, lakini hawajawajibishwa na wanaendelea kuhudumiwa kwa kutumia kodi za wananchi ambao kadiri siku zinavyokwenda wanazidi kuwa maskini.

Inasikitisha kuona kiongozi mkuu wa nchi akifikiria kumpangia kazi mtu aliyeghushi vyeti badala ya kuuliza ni mahabusu gani atapelekwa ili kama anataka kumpelekea chai na chakula afanye hivyo?

Sitanyamaza kukemea kauli au vitendo vya kuwalinda wanaotenda makosa, kwani ninaamini njia pekee ya kujenga taifa imara lenye viongozi wanaofuata maadili bora ni kutofumbia macho maovu.

Napenda kumshauri Rais Kikwete kuwa kama anamuona Masauni ni mchapakazi ni vema akamuajiri kwenye miradi yake binafsi au ya familia yake.

Anaweza kumuajiri kuwa mkuu wa shamba lake la mananasi pale Kiwangwa, lakini si kumtafutia ulaji serikalini kama anavyofikiria.

Kama hataweza kumuajiri kwenye mradi huo ni vema akazungumza na rafiki zake ambao wana viwanda, mashamba na vitega uchumi mbalimbali ambavyo vinatoa ajira kwa Watanzania na wageni.

Najua Rais Kikwete ana historia nzuri ya kuwakumbuka ‘rafiki’ zake au wale waliomtendea mema lakini si busara kutumia cheo chake kuwaridhisha au kuwapoza kwa masahibu yaliyowapata.

Lakini kubwa zaidi ambalo napenda Rais Kikwete alisikie na kulifuata ni kuwa kasi ya kuwaumbua walioghushi vyeti vya kuzaliwa na elimu isiishie kwa Masauni pekee.

Kama itaishia kwa Masauni, minong’ono ya watu itaibuka kuwa uovu wa kiongozi huyo umeibuliwa kwa kuwa alikuwa kikwazo kwa watu waliokuwa wakitaka maulaji ndani ya UVCCM.

Zipo taarifa ambazo hata mimi zinaanza kuingia akilini kuwa Masauni alikuwa akigoma kuidhinisha baadhi ya masuala ambayo yanaonekana kuwa yana masilahi binafsi, hasa kwenye jengo jipya la umoja huo linalotarajiwa kumalizika hivi karibuni.

Minong’ono hiyo inapata mashiko katika kichwa changu kwa kuwa ninawafahamu baadhi ya vigogo ambao vyeti vya elimu zao vina utata lakini mpaka sasa wapo madarakani, kwa kuwa wanatii amri mbaya na safi za wakubwa wao.

Source: Tanzania Daima.
 
Ndugu yangu kwani wewe ni mwanachama wa ccm???? kama ni mwanachama basi tumieni vikao vyenu kukosoa hayo. Binafsi sioni ubaya mkubwa aliyofanya masauni umfanye asipawe shuguli nyingine katika jamii. Kipi kibaya kudanganya umri au kudangaya kiwango cha elimu/kuwa na vyeti to vyuo feki/kudanganya mali ambazo upatikanaji wake ni rushwa/ujambazi????
mbona hao wapo kwenye jamii yetu na wanaendelea kudunda tu.
 
vyote vibaya na hukumu yake ni jela... hatuwezi kutetea upuuzi wa dhambi ndogo au kubwa kwani zote zina madhara sawa wa maskini wa tanzaniza... _)(*&^%$#%^&*()_
 
Ndugu yangu kwani wewe ni mwanachama wa ccm???? kama ni mwanachama basi tumieni vikao vyenu kukosoa hayo. Binafsi sioni ubaya mkubwa aliyofanya masauni umfanye asipawe shuguli nyingine katika jamii. Kipi kibaya kudanganya umri au kudangaya kiwango cha elimu/kuwa na vyeti to vyuo feki/kudanganya mali ambazo upatikanaji wake ni rushwa/ujambazi????
mbona hao wapo kwenye jamii yetu na wanaendelea kudunda tu.
Nani amekuambia kwamba mdanganyifu ana mipaka? Akidanganya kuhusu umri eti kwenye vitu vingine atakuwa mtakatifu! Kwani alipodanganya kuhusu umri si alikuwa anataka vijisenti vya UVCCM? Kitakachamzuia kufanya udanganyifu mwingine ili ajipatie vijisenti vingine ni nini?
 
Kipi kibaya kudanganya umri au kudangaya kiwango cha elimu/kuwa na vyeti to vyuo feki/kudanganya mali ambazo upatikanaji wake ni rushwa/ujambazi????
mbona hao wapo kwenye jamii yetu na wanaendelea kudunda tu.

Huyu Abunawasi vipi! Eti kwa kuwa wengine walidanganya halafu iweje sasa? Kwa kuwa Anunwasi amempiga mke wake kwa hivyo ni halali nimpige wa kwangu, namna gani sasa! Cheap Argument. Buree kabisa
 
Nani amekuambia kwamba mdanganyifu ana mipaka? Akidanganya kuhusu umri eti kwenye vitu vingine atakuwa mtakatifu! Kwani alipodanganya kuhusu umri si alikuwa anataka vijisenti vya UVCCM? Kitakachamzuia kufanya udanganyifu mwingine ili ajipatie vijisenti vingine ni nini?

Mkuu mimi nadhani kinachogomba hapa ni "unfair treatment"
Kwani kuna tofauti gani kati ya kughushi umri na kughushi elimu/cheti kwa minajiri ya kupata wadhifa fulani? Mbona chitalilo bado ni mbunge ili hali polisi walihakikisha kabisa alighushi?

Kwa mtaji huu, Masauni hajatendewa haki, mbeleko iliyowabeba kina chitarilo na wa degree feki, imechanika lini isimbebe Masauni?
 
Ndugu yangu kwani wewe ni mwanachama wa ccm???? kama ni mwanachama basi tumieni vikao vyenu kukosoa hayo. Binafsi sioni ubaya mkubwa aliyofanya masauni umfanye asipawe shuguli nyingine katika jamii. Kipi kibaya kudanganya umri au kudangaya kiwango cha elimu/kuwa na vyeti to vyuo feki/kudanganya mali ambazo upatikanaji wake ni rushwa/ujambazi????
mbona hao wapo kwenye jamii yetu na wanaendelea kudunda tu.

Mkuu vipi wewe. kwani kosa la kughushi umri siyo kuvunja sheria ya nchi?. Na kwa nini apewe nafasi nyingine wakati ameonyesha ni muongo? Vijana tuko wengi hivi kikwete ana maana gani kusema atampa kazi nyingine, je na sisi ? Ni kazi gani hiyo ambayo watanzania hawapewi kulingana na uwezo? amenikera huyu rais wangu. kumbe ndo maana tuko maskini uwezo na uaminifu si vigezo vya kupata watumishi ni kujiana tu!
 
Kaka kwani serikalini kuna waadilifu? Mkae mkijua kuwa masauni alishindwa kula nao tu, alikuwa na misimamo tofauti na walaji wengine na ndo maana wamemtoa otherwise la umri walilijua toka mwanzo. Huko serikalini wakikuingiza wanakuwa wanajua mitego yote ya kukutolea uki-mess nao kidogo tu wamekukutoa.
 
Rais ameweka bad precedent katika hili... period. Mwema hawezi kuinuka tena saa hizi na kusema kuwa wanamchunguza Masauni, ameshazuiliwa na bosi wake ambaye anaona kuwa bado mzee huyo aliyeidanganya nchi anafaa kupewa kazi nyingine
 
Sina uhakika na suala la Chitalilo lakini najua kuna watoto wa Vigogo waliopata kazi BOT bila kuwa na sifa walishafikishwa Mahakamani. Sikuona wamekingiwa kifua kama Masauni! Sijaona mantiki ya mhalifu kutetewa mchana kweupe kama ilivyo kwa Masauni! Huyu bwana ikitokea akapewa kazi nyingine kama alivyoahidi JK itampa doa baya sana kwenye uongozi wake!
 
Salehe Mohamed

SITAKI kuamini kuwa Rais Kikwete, aliamua kutoa kauli kuwa atampangia kazi nyingine aliyekuwa Mwenyekiti wa
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hamad Yusuf Masauni.

Masauni inasemekana kuwa alizaliwa mwaka 1973 lakini aliamua kughushi vyeti vya kuzaliwa ambavyo vilionyesha kuwa alizaliwa mwaka 1979 ili aweze kuchaguliwa kwenye kiti hicho mwaka 2008.

Kiongozi huyo alilazimika kuachia maulaji ya UVCCM baada ya wenzake kumkalia kidedea kuwa ajiuzulu kwa uhalifu alioufanya kwenye chama hicho kikongwe chenye historia ya kulindana na kubebana.

Masauni angewezaje kukataa kuachia madaraka hayo licha ya kuyataka wakati wenzake waliomsaidia kukalia kiti hicho kwa masilahi yao walimgeuka baada ya bosi huyo kushindwa kutimiza kile walichokitarajia?

Sina haja ya kumzungumzia kwa undani Masauni kwa sababu ameshajiuzulu na kwa utaratibu wa chama jambo amesamehewa kwa kuwa hakujua atendalo!

Kilichonikera zaidi ni kauli ya Rais Kikwete kuwa atampangia kazi nyingine Masauni ama iwe ubalozini au serikalini.

Hivi kweli mtu anayedaiwa kughushi na vielelezo vipo wazi ana stahili kupewa kazi na serikali? Huyu ana sifa gani ya uadilifu mpaka amvutie rais.

Binafsi nashawishika kuamini kuwa Masauni, alifanya uhalifu huo, kwa sababu kama hausiki ilikuwaje akakubali kujiuzulu kirahisi namna ile, kwa nini akubali kuchafuliwa jina lake?

Nilitarajia rais Kikwete angekisafisha chama chake kwa kuagiza hatua zaidi za kisheria zichukue mkondo wake dhidi ya Masauni lakini si kumuandalia mazingira mazuri ya kutumia kodi za walalahoi.

Kama Rais Kikwete ameshatamka hadharani kuwa atampangia kazi nyingine Masauni, basi vyombo vya dola kamwe haviwezi kumuwajibisha mtuhumiwa huyo ambaye kwa mujibu wa sheria za nchi ametenda kosa la jinai.

Inawezekana Rais Kikwete alifanya UTANI, kwa sababu ni kawaida yake kufanya utani kwenye masuala nyeti yagusayo mustakabali wa taifa.

Lakini mbona mpaka sasa hajatokea kiongozi wa serikali au wa chama kusema huo ulikuwa utani? Mbona alipowaambia viongozi wa dini kuwa takrima haikwepeki katika mazingira ya sasa tuliambiwa kuwa alifanya utani?

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ndiye aliyepewa jukumu la kuuambia umma kuwa Rais Kikwete alikuwa akitania na hana ubavu wa kuirejesha sheria hiyo iliyochinjwa na mahakama.

Sote tunajua kuwa hakuna aliye juu ya sheria sasa kwa nini Masauni apewe kinga na chama chake pamoja na Rais Kikwete ambaye anamtafutia ulaji?

Kila kukicha wanafunzi wanaoghushi vyeti vya elimu au kuzaliwa ndio wanaopelekwa mahakamani lakini wabunge, vigogo wa CCM wanaendelea kula kuku kwa mrija.

Watakamatwaje wakati kiongozi mkuu wa nchi bado anawahitaji? Tunawezaje kujenga kizazi cha kuwajibika kama sisi wenyewe si wawajibikaji?

Kulindana kunakofanywa na CCM ndiko kunakotufanya tupate viongozi wasio na upeo mzuri pamoja na wenye kujali masilahi binafsi badala ya wananchi.

Leo hii kuna wabunge wameshabainika kughushi vyeti vya elimu, lakini hawajawajibishwa na wanaendelea kuhudumiwa kwa kutumia kodi za wananchi ambao kadiri siku zinavyokwenda wanazidi kuwa maskini.

Inasikitisha kuona kiongozi mkuu wa nchi akifikiria kumpangia kazi mtu aliyeghushi vyeti badala ya kuuliza ni mahabusu gani atapelekwa ili kama anataka kumpelekea chai na chakula afanye hivyo?

Sitanyamaza kukemea kauli au vitendo vya kuwalinda wanaotenda makosa, kwani ninaamini njia pekee ya kujenga taifa imara lenye viongozi wanaofuata maadili bora ni kutofumbia macho maovu.

Napenda kumshauri Rais Kikwete kuwa kama anamuona Masauni ni mchapakazi ni vema akamuajiri kwenye miradi yake binafsi au ya familia yake.

Anaweza kumuajiri kuwa mkuu wa shamba lake la mananasi pale Kiwangwa, lakini si kumtafutia ulaji serikalini kama anavyofikiria.

Kama hataweza kumuajiri kwenye mradi huo ni vema akazungumza na rafiki zake ambao wana viwanda, mashamba na vitega uchumi mbalimbali ambavyo vinatoa ajira kwa Watanzania na wageni.

Najua Rais Kikwete ana historia nzuri ya kuwakumbuka rafiki zake au wale waliomtendea mema lakini si busara kutumia cheo chake kuwaridhisha au kuwapoza kwa masahibu yaliyowapata.

Lakini kubwa zaidi ambalo napenda Rais Kikwete alisikie na kulifuata ni kuwa kasi ya kuwaumbua walioghushi vyeti vya kuzaliwa na elimu isiishie kwa Masauni pekee.

Kama itaishia kwa Masauni, minongono ya watu itaibuka kuwa uovu wa kiongozi huyo umeibuliwa kwa kuwa alikuwa kikwazo kwa watu waliokuwa wakitaka maulaji ndani ya UVCCM.

Zipo taarifa ambazo hata mimi zinaanza kuingia akilini kuwa Masauni alikuwa akigoma kuidhinisha baadhi ya masuala ambayo yanaonekana kuwa yana masilahi binafsi, hasa kwenye jengo jipya la umoja huo linalotarajiwa kumalizika hivi karibuni.

Minongono hiyo inapata mashiko katika kichwa changu kwa kuwa ninawafahamu baadhi ya vigogo ambao vyeti vya elimu zao vina utata lakini mpaka sasa wapo madarakani, kwa kuwa wanatii amri mbaya na safi za wakubwa wao.

Source: Tanzania Daima.
Sasa ni Waziri wa mambo ya ndani , wizara inayohakikisha kwamba nchi hii hakuna kufoji
 
Masauni ni wa znz pia
naona huu mwaka spika nae atoke tu znz
Waziri mkuu nae znz!

Hivi akina Kabudi, Mkuvi na wengine hata Majaliwa
si wajitoe ccm?
Kweli hii nchi imekuwa genge sasa!

Upinzani hii ndiyo nafasi pekee ya kuingia Ikulu
huenda Mungu amejibu maombi yenu
Cha msingi mleteni mtu sahihi!
NDUGAI atakufaeni au KABUDI
 
Unataka kusema hii ni fursa sio?
IMG-20220107-WA0010.jpg
 
Back
Top Bottom