Kupaka krimu, yaani ni kama karolaitHiyo kwenye bold ndio uwezo wa kufanya nini?
Hata alipoenda UD aliwaburuza mno wenzake!!!kwenye utendaji ni tofauti sana ukizingatia kuna suala la mfumo mzima kuwa corrupt!
Huyu jamaa inasemekana alikuwa kichwa mbaya shuleni enzi zile, form four alipata A masomo aliyotahiniwa. Form six, A tupu. Mara zote hizo akiibuka Tanzania One. Amepewa wizara akafanya kama Mwanaasha wa Feza girls. Mi nashindwa kuelewa hizo A alizipataje? alikuwa anajilipua (kudesa)? au kazeeka? Wataalam naombeni jibu!
Jaribu kufikiria kwa mapana zaidi, ikiwa muheshimiwa Chami alishawahi kumushauri mkuu wa nchi kwamba Ekerege hafai lakini mkuu akuchukua hatua, unafikiri kwamba muheshimiwa chami anaweza kumuumbua mkuu wa nchi sasa hivi kwamba alisha mshauri? kwa hiyo tujue kwamba kuna sababu nyingi ambazo zaweza kumfanya mtu ambaye kimsingi ni mahili katika mambo akaonekana si kitu mbele ya jamii. Mfumo wa uwajibikaji ni mojawapo ya vikwazo kwa watu kutoonyesha umahili wao katika nyanja mbalimbali. Bila kuwa na katiba ambayo inamupunguzia Raisi madaraka ya kuajiri watu bado maprofessor,na madaktari wetu wa falsafa wataonekana vituko kana kwamba hawakwenda hata chekechea.
Anaonekana mtu makini lakini kanyonyoka nywele labda ndo sababu maana anakila dalili ya kisukari!
Kaka songoro! Nakuunga mkono kabisa siasa ni field chafu sana! Kumchukulia hatua ekelege kwa maneno ya wanasiasa ni kinyume na taratibu. Na pia ni lazima hatua zichukuliwe kukiwa na written evidence na sio tuhuma za maneno. Ila sehemu chami ambapo anabanwa ni katika kusimamia utendaji. Madudu yaliyotokea TBS hawezi kujitoa maana wizara yake ilipaswa kuujua huo udhaifu hata kabla kamati haijaufunua. Kwa hiyo kuna swala la kumuwajibisha mkurugenzi (ambalo mi naona Hawezi kuhukumiwa kwa kushindwa hilo sababu taratibu hazikukamilka kumruhusu kufanya hilo) na la pili ni kushindwa kufuatilia utendaji wa maeneo yanayomhusu hivyo kusababisha hasara. Hili hawezi kilikwepa.
Unashangaa nini sana
Hujawahi kuona Daktari akivuta sigara ?
hujawahi kuona Civil Engineer akichakuchua vipimo na magorofa kuanguka ?
huawahi kuona computer scientist , hana antivirus kwenye computer yake ?
Hujawahi kuona Askofu akiiba pesa za kanisa ?
hujawahi kuona takukuru wakipokea rushwa ?
Uadilifu sio Elimu !!!!
Kuzingatia unachujua na kuamini kwamba ni sahihi ni Uadilifu hata kama wewe au mtu mwingine mtapoteza chochote kile