Erasto Mpemba: Mwanasayansi aliyefariki bila kuthaminika nyumbani Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Erasto Bartholomeo Mpemba (1944 - 2023) alikuwa mwanasayansi kutoka nchi ya Tanzania aliyegundua tabia ya pekee ya maji inayojulikana leo kwa jina la athari ya Mpemba (kwa Kiingereza Mpemba effect). Jina hili linaeleza tabia ya maji kuganda kwa haraka zaidi yakiwa ya moto kuliko maji ya baridi.

MAISHA

Mpemba alizaliwa tarehe 1 Februari 1944 katika kijiji cha Bumbuli, wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Alikua mtoto wa mwisho kwenye familia yenye watoto nane ya Foibe na mchngaji Bathoromeo Mpemba.

Alifunga ndoa na Bi. Naomi Vuhahula mwaka 1986 na alikua na watoto 6.

1685885276732.png

ELIMU

Mpemba alipata elimu ya Msingi katika shule ya Msingi Bumbuli na baadae kuendelea na shule ya kati Lwandai. Baada ya hapo, aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Magamba iliyopo mkoani Tanga. Elimu ya kidato cha tano na sita ("A level") alipata shule ya sekondari Mkwawa.

Mwaka 1969, Mpemba alipata stashahada ya elimu ya wanyamapori kutoka chuo cha Mweka kilichopo Kilimanjaro, Tanzania. Baadae mwaka 1977 alipata shahada ya sayansi kutoka chuo kikuu cha Canbera kilichopo nchini Australia. Alijiendeleza kwa mafunzo ya uda mfupi katika nyakati mbalimbali, mwaka 1980 kutoka chuo cha Kivukoni na mwaka 1984 kutoka Michigan, Marekani.

Jinsi alivyogundua athari ya Mpemba

Mnamo mwaka 1963 Mpemba alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenye shule ya sekondari ya Magamba (Tanga). Vijana walikuwa na kawaida ya kutengeneza aiskrimu yao wenyewe jikoni mwa shule. Kwa kawaida walichemsha maziwa wakakoroga sukari ndani yake, wakaiacha kupoa halafu kuiweka kwenye friza.

Siku moja Mpemba alichelewa kazi hii akaogopa ya kwamba mwanafunzi mwingine angechukua chombo cha mwisho kilichopatikana kwa aiskrimu kwa hiyo alimwaga maziwa ya moto katika chombo kile cha mwisho na kuiweka vile kwenye friza pamoja na chombo cha mwenzake aliyewahi kuchemsha na kupoza maziwa tayari. Alipofungua friji baada ya saa moja na nusu alikuta aiskrimu yake ilikuwa tayari ilhali ile ya mwenzake (aliyeweka maziwa iliyopoa haikuganda bado ilikuwa katika hali ya ujiuji.

Siku iliyofuata akamwuliza mwalimu wa fizikia kwa nini maziwa ya moto iliganda haraka kuliko ile ya kupoa. Mwalimu akajibu hii haiwezekani lazima alikosa.

Katika likizo zilizofuata Mpemba alikutana na rafiki aliyefanya kazi ya upishi mjini Tanga akitengeneza aiskrimu. Huyu rafiki alimweleza ya kwamba hata yeye na wapishi wengine wa aiskrimu huko Tanga waliweka mchanganyiko wa aiskrimu kwenye friza ilhali ni moto kwa sababu inaganda haraka zaidi. Habari hii ilimkumbusha kuhusa maarifa yake shuleni.

Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Mpemba aliendelea kusoma A-level kwenye Mkwawa High School huko Iringa. Hapa alifundishwa kuhusu sheria ya kupoza ya Newton.

Akamwuliza tena mwalimu wa fizikia kuhusu siri ya maziwa ya moto kuganda haraka kuliko maziwa ya kupoa. Hata mwalimu huyo alikataa akasema haiwezekani na hii ni fizikia ya Mpemba si fizikia ya kawaida. Tangu siku hiyo utani wa "fizikia ya Mpemba uliendelea shuleni.

Mpemba aliamua siku moja kurudia jaribio la kuweka vyombo viwili vya maji ya moto na maji baridi ndani ya friza akaona matokeo ni yaleyale.

Siku moja shule ilitembelewa na profesa Denis Osborne wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mpemba alishika moyo akasimama na kumwuliza Dr Osborne kwa nini maji ya moto yanaganda haraka kuliko maji baridi. Osborne alishtuka kidogo lakini aliona ni muhimu kuwahamasisha wanafunzi, kwa hiyo hakutaka kumkatisha tamaa, hivyo akajibu kwa upole kuwa hajasikia habari kama hii, pia hailingani na fizikia jinsi anavyoijua, lakini labda inaweza kutokana na athari isiyojulikana alimwahidi kurudia jaribio akifika tena Dar es Salaam. Wiki iliyofuata Osborn alifanya jaribio na matokeo yalikuwa yaleyale.

Baadaye, wakati Mpemba aliposoma kwenye Chuo cha utawala wanyama pori huko Moshi alitunga muswada pamoja na Dr Osborne walipoeleza pamoja majaribio yao wakijaribu kutoa maelezo ya athari.

Katika maisha ya baadaye Mpemba alikuwa mtumishi kwenye wizara ya maliasili hadi kustaafu.

Mpemba hakuwa mtu wa kwanza wa kugundua athari hii, lakini alikuwa mtu aliyefaulu kuitambulisha mara ya kwanza katika jamii ya wanasayansi.

Anastahili sifa kwa ujasiri wake wa kutetea hoja yake mbele ya walimu na wanafunzi waliomcheka. Vilevile utambuzi wake uliweza kuzaa matunda baada ya kukutana na mwanasayansi Dr Osborne aliyekuwa tayari kusikia hoja ya ajabu na baadaye kumpa sifa mwanafunzi badala ya kutangaza athari kama kazi yake mwenyewe tu.
1685885377818.png

KAZI

Mpemba alianza kazi kama afisa wa wanyamapori wa mkoa wa Mara mwaka 1969. Mwaka 1970 mpaka 1972 alifanya kazi kama afisa habari wa makao makuu ya wizara na baadae kurudi kua afisa wanyamapori wa mkoa wa Shinyanga kati ya mwaka 1972 na 1974. Pia aliwahi kufanya kazi kama afisa maliasili wa mkoa wa Iringa kati ya mwaka 1981 - 1989. Mpemba alifanya kazi wizara ya maliasili kati ya mwaka 1989 hadi mwaka 2005 akisimamia kitengo cha maendeleo na usimamizi ambapo alistaafu mwaka 2005 kama afisa maliasili mwandamizi.

Ulimwengu wa Sayansi unalitukuza sana jina la Isaac Newton. Sijui dunia ingekuwa wapi bila ugunduzi wa 'kichwa' huyu. Aligundua kanuni mbalimbali zinazofanya leo hii maisha yawe yalivyo. Kwa mfano, aligundua kanuni za mwendo(Newton's Law of Motion) ambazo dunia inazitumia kuendeshea vyombo mbalimbali kama magari.

Lakini kati ya kanuni zote hizo, kanuni moja ya upoaji wa vitu vilivyopata joto (Newton's Law of Cooling) ilikutana na changamoto kutoka kichwa kimoja cha kitanzania kinachoitwa Erasto Bartholomeo Mpemba. Kanuni ya Newton inasema 'Kitu chenye jotoridi sawa au linalokaribiana na jotiridi la mazingira yake, hupoka haraka zaidi kile chenye jotoridi kubwa kuliko jotoridi la mazingira yake'

1963 akiwa kidato cha tatu shule ya sekondari Magamba Lushoto Tanga(siku hizi ni chuo kikuu cha Sebastian Kolowa SEKOMU), aligundua kwamba maziwa yaliyochemshwa hupoa na kuganda haraka kwenye friji kuliko maziwa ya baridi. Ugunduzi huu unapingana na kanuni ya Newton kitu kilichomfanya hata mwalimu wake ampuuzie.

Alipomaliza kidato cha nne, akachaguliwa kujiunga na shule sekondari Mkwawa Iringa(siku hizi ni chuo kikuu elimu MUCE). Akamuuliza mwalimu wake wa fizikia, naye pamoja na wanzafunzi wengine wakamuona mpemba kama mjinga.

Akiwa bado shuleni hapo, walitembelewa na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar Es Salam, Dk. Denis Osoborne(siku hizi ni Prof.). Mpemba akamuuliza swali lile lile, Dk. Osborne akasema hajawahi kutana na hicho kitu ila ataenda kufanya utafiti akirudi Dar...na kweli akafanya utafiti huo, akajiridhisha.

Ugunduzi huo ukasambaa dunia nzima na kupewa jina la MPEMBA EFFECT.

2012, Jarida la ‘The Royal Society of Chemistry’ la Chuo Kikuu cha Cambridge cha Uingereza lilitangaza zawadi nono ya pesa kwa mtu au kikundi cha wanasayansi watakaoweza kutoa maelezo mazuri, bora na ya kuhusu “Mpemba effect'.

Watu zaidi ya 22,000 walijitokeza,11 wakaingia fainali, na Nikola Bregovic kutoka Croatia (mfanyakazi wa maabara ya Kemia Chuo Kikuu cha Zagreb) akatangazwa mshindi. Januari 10, 2013 Erasto Bartholomeo akaombwa kukabidhi zawadi kwa mshindi.

KIFO

Kufuatia kifo cha Mwanafizikia Erasto Mpemba, Mtanzania aliyegundua nadharia ya Mpemba Effect, The Chanzo imezungumza na Dk Aneth David, mwanasayansi, mtafiti, na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujadili mchango wake kwenye tasnia ya sayansi Tanzania na duniani kwa ujumla.

‘Mpemba Effect’ ni nadharia ya kisayansi inayosema kwamba maji yakiwa ya moto, au kimiminika kikiwa cha moto, kinaganda haraka zaidi kuliko kikiwa cha baridi. Ni nadharia ambayo tafiti bado zinaendelea kufanyika juu ya namna inavyoweza kutumiwa kwenye maeneo kama vile ya viwandani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia yake, Mpemba alifariki hapo Mei 14, 2023, jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa takriban miaka miwili. Mwanasayansi huyo alizikwa nyumbani kwao, Bumbuli, mkoani Tanga.

Mpemba alikuwa na Bachelor of Science kutoka Chuo Kikuu cha Canbera, Australia, aliyoipata mwaka 1977. Pia, alipata mafunzo ya muda mfupi kutoka Chuo cha Kivukoni (1980) na Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani (1984).

Mpemba alistaafu kazi Serikalini mwaka 2005 akiwa na cheo cha Afisa Maliasili Mwandamizi, Wizara ya Maliasili na Utalii, wizara aliyojiunga nayo mwaka 1969 kama Afisa Wanyama Pori, mkoa wa Mara.

Mwanafizikia huyo ameacha watoto sita, wajukuu saba na kitukuu kimoja aliowapata na mke wake, Naomi Vuhahula.
 
Januari 10, 2013 Erasto Bartholomeo akaombwa kukabidhi zawadi kwa mshindi.

Waafrika mbowe na lisu wanatucheleweshea sana maendeleo.

Agundue yy zawadi apewe mungine
 
Januari 10, 2013 Erasto Bartholomeo akaombwa kukabidhi zawadi kwa mshindi.

Waafrika mbowe na lisu wanatucheleweshea sana maendeleo.

Agundue yy zawadi apewe mungine

Yeye kavumbua matokeo (effect) lakini hukuwa anajua chanzo (cause) ya hiyo effect, huyo aliyepewa zawadi kapewa zawadi kwa kufafanua kisayansi chanzo cha hiyo effect ndio maana Ndugu Mpemba akapewa heshima ya yeye kwenda kutoa zawadi kwa huyo aliyetoa sababu ya kwanini kimiminika chenye joto hupoa haraka zaidi ya kimiminika chenye baridi isitoshe naye alipohudhuria pia alipata somo kujua ni kwanini hali hiyo hutokea hivyo.
 
Hii concept mbona inaonekana ni uongo.

Yani uchukue maji "A" yenye 25°C na Maji "B" yenye 50°C uweke kwenye friji, alfu kuganda(kufika 0°C) yawahi maji A!!!?

Ndio, sasa unatakiwa ufafanue kisayansi inakuaje.
 
Hii concept mbona inaonekana ni uongo.

Yani uchukue maji "A" yenye 25°C na Maji "B" yenye 50°C uweke kwenye friji, alfu kuganda(kufika 0°C) yawahi maji A!!!?
mkuu we mwenyewe umejichanganya hapa, ni kama hujaelewa mada.
25°C na 50°C ipi ni joto zaidi?
 
Katika watu wana akili san ani Huyu jamaa aligundua MPEMba Effects
hamna akili sana hapo. Yeye mwenyewe amekiri jamaa zake huko Tanga wamemshuhudia kuwa katika utengenezaji wao wa Iscrem wamekuwa wakitumia maji ya moto ili icecrem zao zigande haraka. Hivyo, suala la maji ya moto kuganda haraka wajasiriamali walishakuwa wanakijua siku nyingi. Yeye alitakiwa aende mbali zaidi kwani maji ya moto yanaganda haraka kuliko ya baridi jambo ambalo hakulifanya zaidi yeye mwenyewe kuendelea kuwauliza wanasayansi wenzanke bila jibu.
 
Mzee wajasiriamali mwaka 1963 wanatoka wapi?
Hebu acha porojo mzee..
Ice cream mwaka 1963?
Umesoma Thesis yake?
Tatizo wabongo kila kitu huwa tunabisha bila kujua!

Unasema walikuwa wanajua kitambo wajasiriamali kabla yake siku nyingi..?

Hivi unajua Hali ya Umeme mwaka 1963 ya Tanganyika?
Wangapi waliokuwa wanafnya Biashara hiyo unayotaja?

Kuzaliwa Tanzania ni Mzigo wa Miiba aisee
 
Mkuu mbona umemshambulia hivyo huyo wakati alichosema ndicho kilichoandikwa kwenye bandiko au hujalisoma

"Katika likizo zilizofuata Mpemba alikutana na rafiki aliyefanya kazi ya upishi mjini Tanga akitengeneza aiskrimu. Huyu rafiki alimweleza ya kwamba hata yeye na wapishi wengine wa aiskrimu huko Tanga waliweka mchanganyiko wa aiskrimu kwenye friza ilhali ni moto kwa sababu inaganda haraka zaidi. Habari hii ilimkumbusha kuhusa maarifa yake shuleni"

Alichosema kimetoka hapo
 
Nanukuu "Katika likizo zilizofuata Mpemba alikutana na rafiki aliyefanya kazi ya upishi mjini Tanga akitengeneza aiskrimu. Huyu rafiki alimweleza ya kwamba hata yeye na wapishi wengine wa aiskrimu huko Tanga waliweka mchanganyiko wa aiskrimu kwenye friza ilhali ni moto kwa sababu inaganda haraka zaidi. Habari hii ilimkumbusha kuhusa maarifa yake shuleni". haya siyo maneno yangu. Acha kudhalilisha Udaktari wako.
 
Mkuu mbona umemshambulia hivyo huyo wakati alichosema ndicho kilichoandikwa kwenye bandiko au hujalisoma

"Katika likizo zilizofuata Mpemba alikutana na rafiki aliyefanya kazi ya upishi mjini Tanga akitengeneza aiskrimu. Huyu rafiki alimweleza ya kwamba hata yeye na wapishi wengine wa aiskrimu huko Tanga waliweka mchanganyiko wa aiskrimu kwenye friza ilhali ni moto kwa sababu inaganda haraka zaidi. Habari hii ilimkumbusha kuhusa maarifa yake shuleni"

Alichosema kimetoka hapo
Daktari uchwara huyo. Mpemba alitakiwa kutuambia kwani maji ya moto yanaganda haraka kwenye friza kuliko ya baridi. Kujua tu maji ya moto yanaganda haraka Mpemba mwenyewe kashudia kwamba hata rafiki yake mpishi huko Tanga anafanya hivo. Mpemba mwenye hakuendelea na sayansi ya ugunduzi zaidi ya kuishgia kuwa afisa wanyama pori. Tatizo Waafrika tunapenda sana kutukuzwa kwa vitu vidogo sana wakati wenzetu wanelekea safari za Mars.
 
Mkuu mbona umemshambulia hivyo huyo wakati alichosema ndicho kilichoandikwa kwenye bandiko au hujalisoma

"Katika likizo zilizofuata Mpemba alikutana na rafiki aliyefanya kazi ya upishi mjini Tanga akitengeneza aiskrimu. Huyu rafiki alimweleza ya kwamba hata yeye na wapishi wengine wa aiskrimu huko Tanga waliweka mchanganyiko wa aiskrimu kwenye friza ilhali ni moto kwa sababu inaganda haraka zaidi. Habari hii ilimkumbusha kuhusa maarifa yake shuleni"

Alichosema kimetoka hapo
Basi aliyeandika hivyo na yeye alikuwa na MisInformation kuhusu Mpemba Effects aende akasome vizuri Thesis zipo Ukienda UDSM utazikuta au Duniani Kote Kwenye Maktaba za Science kuhusu MPEMBA Effects
Na sio kama ilivyo..
 
Back
Top Bottom