Sirro: Sakata la kina Roma kutekwa ni jambo la kawaida, awashangaa wasanii na Makonda kuingilia

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake ni jambo la kawaida huku akisitiza kuwa hayajaanza kutokea leo kwani ni tukio kama matukio mengine.




sirro%20lai..jpg

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro

Kamanda Sirro amesema hayo baada ya kelele za watu kwenye mitandao ya kijamii ndani ya siku tatu, huku wasanii, wanasiasa pamoja na wadau mbalimbali wa muziki kuja juu juu ya suala la kupotea vijana hao katika mazingira ya kutatanisha huku wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini.

“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, hili la kina Roma na wenzake ni tukio kama matukio mengine yaliyokuwa ya ujambazi kwa hiyo tupeni muda tupeleleze, tukifika mahali pazuri tutawaita tuwape taarifa lakini nimeona mitandao mingi inazungumza, jana nikaona wasanii wamekutana lakini nikajiuliza hivi yangekuwa haya matukio yanatokea ya uhalifu yanapotokea watu wanakutana ingekuwaje ?,

Jamani kazi hii tumepewa kwa mujibu wa Katiba na ni lazima tutimize wajibu wetu kwa hiyo tupeni muda tutakuwa na majibu mazuri katika hili”. Alisema Kamishna Sirro pindi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisni kwake Jijini Dar es Salaam

Aidha Kamanda huyo amesema mpaka sasa wameshaunda timu ya uchunguzi na inaendelea vizuri katika upelelezi huku akiwataka wananchi kuwa na subra kwa kuwa upelelezi ndiyo utasema kila kitu.

Kwa upande mwingine amewataka watu waache tabia ya kujifanya wao ndiyo ‘Kamishna Sirro’ na kutaka kuzungumzia habari za upelelezi hivyo amewataka watu kuliamini jeshi la Polisi kwa kuwa hawapendi vitendo hivyo viwepo na viendelee kutokea.


....sawa mzee....just as simple like that?
 
Nlipata wasaa wa kukutana na kamanda ziro. Nilichojifunza ni kuwa jamaa hawezi kumwangalia mtu straight machoni, nadhan ni moja ya principle zao au anaona haibu ujinga wanaofanyaga wakiwa kwenye nguo za kaki.
 
Kauli iliyojaa kiburi, jeuri, na ulevi wa madaraka,kauli ambayo imetoa ujumbe mubashara kwa raia kwamba kupotea kwake ni kawaida kama mbuzi, kwamba kukutana kujadili kupotea kwa raia rafiki yetu ni kuingilia uchunguzi polisi, wapi tunalipeleka taifa letu ???
 
Sirro hili swala wanachukulia la namna namna? mtu inakuwa kawaida vipi kutekwa? tuweke wazi
 
Kamanda sirro watanzania wanauwezo mkubwa ki upembuzi kuliko unavyoongea.. naomba kuuliza jeshi la polisi lipo kisiasa au kwa kufata mwenye madaraka au lipo kwa ajili ya ulizi wa raiya na Mali zake.? Naomba huo mkono mrefu ufatilie kujuwa haya matukio yanafanywa na nani acheni Propaganda.
 
Danadana zimeshaanza.
Huu mchezo anaocheza bashite na sirro na anayewatuma utawacost. ICC inawahusu actually naombea watu fulani hiviiii kupeleka Tz mahakama ya ICC. Kwa hili bashite hatakuwa na pakutokea. Waache waendelee kukusanya ushahidi wenyewe. Kauli hizi Ben Saanane atapata justice ikiwa yu hai au mauti. Let's wait n see! Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Hili tukio ni wazi lilipangea ku outsmart mkutano wa Nape Mtama! Kama wapanga mikakati ndo wako hivi! Heri mm sijasema!!
 
Kweli aliyeturoga amekufa, yani kwa akili yako unasubili ifike kesho!!!! kwa hiyo swala la Roma limebaki ni la mkuu wa mkoa pekee hadi kesho??? Hili swala ni letu sote mana leo kwake kesho kwangu na wewe.
Inamaana wewe husubiri? Watu mko makini kwelikweli. Mwenyezi Mungu akutangulie. Tupe mrejesho wa upelelezi wako, mkuu.
 
Back
Top Bottom