SIRI ya CCM Kuudhoofisha upinzani kabla ya 2014

Yaliyo mkuta Mwanza hatokaa hayasahau ktk maisha yake ya siasa. Bt still wanawakati mgumu kurudisha imani juu yao ya wabongo waliofunguka Mawazo.
 
CCM haiwezi kuudhoofisha upinzani kwa sababu kwa sababu zifuatazo ambazi pia nimezipost kwenye thread yangu ya NYOKA AKIJUA VUA GAMBA ANAKUWA CHURA?.

Kwa mtu yo yote mwenye ufahamu wa kawaida anajua kuwa, Nyoka akijivua gamba hawi Chura au Mjusi, kama anasuma wala sumu yake haipungui makali. Sana sana anajipanga kutenda yale yale ya siku zote kwa kasi zaidi.Habadili chakula, wala habidili tabia, umri wa kuishi au kitu chochote. Ni yule yule Nyoka hata jina lake halibadiliki. Kilichobadilika ni ngozi tu imekuwa nzuri zaidi, mpya zaidi inayovutia.

CCM wamebadilisha sura za secretariet, wamebadili pia baadhi ya wajumbe wa kamati kuu. Hivi kumweka mkama nafasi ya makamba kunaleta nafuu gani kwa watazania? Hawa wote walikuwa ni viongozi wa CCM na Serikali yake kabla ya uteuzi wa jana. Mkama alikuwa katibu wa wizara ya afya miaka kadhaa akikumbwa na tuhuma kibao zilizohusu dawa ya ukimwi. Magazeti yaliandika sana tu. Chiligati alikuwa waziri wa ardhi. Hakufanya lolote zaidi ya kuharibu na kurudisha nyuma kazi nzuri aliyoanzisha magufuli katika wizara ile. Je, kubadili secretariet inawafaidije watanzania? Au itawasaidiaje CCM? Ina punguzaje mikataba ya feki kama IPTL. Je, itaibuka na kauli ya kutokulipa Downs? Itatoa tamko la kuridhia mabadiliko makubwa ktk mswada wa mabadiliko ya katiba yanayopigiwa kelele kila kona wakati mkiti wake ni Rais JK aliyeuleta mswada huo? Au kumtosa Fisadi mkubwa kuliko wote RA kwenye CC wakati mfanyakazi wake wa zamani/Swahiba wake ni waziri wa Nishati na Madini (Ngeleja) kwa kupigiwa debe na RA mwenyewe kunaleta jipya gani?
HII ni danganya toto, tatizo la CCM ni la kimfumo, halibadiliswi kwa kubadili sura za watedaji.
My take,
Maisha bora hayawezi kuletwa na Chama kile kile, chenye sera zile zile kikiongozwa na Kikwete yule yule aliyeleta ombwe la uongozi ktk nchi yetu, eti kwa kubadili nafasi za baadhi ya viongozi na kuwa hadaa wananchi kuwa kimejivua gamba CCM kingali na sumu ile ile ya Ufisadi

Shetani hawezi kuokoka.
 
Habari za kuaminika kutoka kikao cha CCM Dodoma ni pamoja na ajenda ya siri ya kudhoofisha nguvu za upinzani hasa Chadema. Kuhakikisha haipenyi vijiji na hivyo CCM kuendelea kuimarisha mashina vijijini ambako kuna wapiga kura wengi wasiojua maana ya mageuzi.

Chama chochote kilicho madarakani, hakiwezi kujiimarisha kwa wananchi kwa kutumia hila bali ni kuwaletea maendeleo wananchi. Kama maazimio hayo ya 2014 yanajumuisha yafutayo
  1. By 2014 vijiji vyote Tanzania viwe na nyumba za tofari na kuezekwa kwa bati siyo nyasi
  2. By 2014 vijiji vyote viwe na maji safi ya bomba ya uhakika
  3. By 2014 vijiji vyote viwe na umeme wa uhakika
  4. By 2014 vijiji vyote viwe vimeunganishwa na barabara zinzopitika wakati wote (I mean tarmac roads) kuwawezesha wanakijiji kuuza mazao yao mijini kwa wakati
  5. By 2014 CCM iwe imehakikisha kuwa kwenye vijiji kuna huduma bora za afya na ulinzi
  6. By 2014 CCM iwe imeimarisha ajira kwa vijana na hivyo kujenda mazingira ya kila mwenye kutaka kufanya kazi ananufaika na kazi zilizopo ambazo zinalipa vizuri.
  7. By 2014 CCM ikihakikisha kuwa mijini watu wana maji safi 24 hours a day per week per month per year na umeme haukatiki, kwa kuwa ITV wanaonesha mdahalo wa Upinzani inaikandia CCM
  8. By 2014 haki inakuwa ni primary objective kwa watawala, polisi hawanyanyasi wananchi, Huduma za afya zinaboreshwa vifo vya uzembe vinapungua mahospitalini.
Kama hayo juu yakitekelezwa mimi binafsi nitahakikisha nashawishi watu wangu wa karibu kama 200 nilio nao kwa pamoja tuipigie kura CCM mwaka 2015. Anything short of that is a total waste of time and opportunity for a party in power. I mean if they embark on seducing and bribing opposition leaders like Shitambala to defect, they have to be prepared for more bribes to attract those who will fill the vacuums left by defectors as they will be more strong than ever. The strength of opposition does not come from the types of opposition leaders but from the hardship of regular citizens after they feel marginalised by the rulers who are seen to live porsche lives while themselves are struggling with one meal a day without success.
 
Acha watu wawe na uwanja mpana zaidi kuota ndoto zenye kuwaletea wao faraja mioyoni mwao; Tanzania hakuna tena chama cha kudhoofisha vingine isipokua tu CCM chenyewe kujichimbia kaburi kwa kujipaka mafuta mgongo wa nyoka na kujishangilia ovyo kama zuzu kujivua kule gamba lenye gundi zito kiasi hiki.

Unafiki wa Zitto wala isihesabiwe chochote kama mbinu kwani Nguvu ya Umma tayari inayo data zote na kazi ni rahisi sana hapo wala kusiwe na taabu kulitatua hivi karibuni.

CCM wala haipo jirani na kujivua gamba mbaka kwanza kiwe kimeunga mkono kwa dhati kabisa kuundwa kwa katiba mpya ya wananchi ndipo wala mtu atakielewe, kubadilisha tu sura za watu badala ya misingi ya utawala ni kule CCM kujiangamiza jumla nchini!!!!!!
Sasa hapo zitto kaingiaje?? elewa topic ndo uchangie, nyie ndo kina SHITAMBALA Zitto yupo Chadema na ataendelea kuwa Chadema labda ukaanzishe Chama chako, wala hahitaji comment zako kujua kama ni mwana kindakindaki wa Chadema, kwa Taarifa yako ZITTO kaanza kuwa Chadema kabla yenu nyie wafata mkumbo!!!!kama kina mzee Mtei,Makani na wazee wengine wameona ni Bora Chama kiwe na watu wenye tafakuri tofauti wewe unataka watu wenye mawazo yenye kufanana kama COCACOLA nenda kwa Tendwa kaanzishe Genge lako,Chadema ni Tofauti na CCM kwa kuwa hawana yes sir,.. but why sir?..
 
Wakuu.

Dont underestimate CCM. Hawa watu ni wazuri katika kupanga mbinu chafu.
Nani alitegemea surprise ya CCM ya kutangwazwa washindi 2010?

Historia inaonesha kuwa mipango yao ya kusambaratisha upinzani imefanikiwa mara zote miaka iliyopita.
Sasa wakati tunasema CCM imekwisha ni vizuri tujitathmini na sisi wenyewe isiwe sisi ndio tumemalizika.!!!

Mpaka sasa hakuna chama ch siasa chenye mbinu chafu kama CCM, lakini pia hakuna chama chenye nyenzo na mtaji kama CCM.

Na wananchi wengi si wananchama wa vyama vya siasa.

Sasa Ninyi wenye vyama isitokee kuwa caught off- guard na CCM!

Ndugu yangu, ccm ilishakufa siku nyingi ila inabebwa na dola tu hawana mbinu yoyote kisiasa. Ndio maana wajuzi wa mambo waliliona hili na kuanza kulilia katiba ambayo itatupatia tume huru. NEC ndio mtajiwa ccm kwa sasa, wakidhibitiwa huko utaona walivyo watupu maana hawajui siasa ila wanapenda kutawala kwa maslahi ya wachache.
 
Chama chochote kilicho madarakani, hakiwezi kujiimarisha kwa wananchi kwa kutumia hila bali ni kuwaletea maendeleo wananchi. Kama maazimio hayo ya 2014 yanajumuisha yafutayo
  1. By 2014 vijiji vyote Tanzania viwe na nyumba za tofari na kuezekwa kwa bati siyo nyasi
  2. By 2014 vijiji vyote viwe na maji safi ya bomba ya uhakika
  3. By 2014 vijiji vyote viwe na umeme wa uhakika
  4. By 2014 vijiji vyote viwe vimeunganishwa na barabara zinzopitika wakati wote (I mean tarmac roads) kuwawezesha wanakijiji kuuza mazao yao mijini kwa wakati
  5. By 2014 CCM iwe imehakikisha kuwa kwenye vijiji kuna huduma bora za afya na ulinzi
  6. By 2014 CCM iwe imeimarisha ajira kwa vijana na hivyo kujenda mazingira ya kila mwenye kutaka kufanya kazi ananufaika na kazi zilizopo ambazo zinalipa vizuri.
  7. By 2014 CCM ikihakikisha kuwa mijini watu wana maji safi 24 hours a day per week per month per year na umeme haukatiki, kwa kuwa ITV wanaonesha mdahalo wa Upinzani inaikandia CCM
  8. By 2014 haki inakuwa ni primary objective kwa watawala, polisi hawanyanyasi wananchi, Huduma za afya zinaboreshwa vifo vya uzembe vinapungua mahospitalini.
Kama hayo juu yakitekelezwa mimi binafsi nitahakikisha nashawishi watu wangu wa karibu kama 200 nilio nao kwa pamoja tuipigie kura CCM mwaka 2015. Anything short of that is a total waste of time and opportunity for a party in power. I mean if they embark on seducing and bribing opposition leaders like Shitambala to defect, they have to be prepared for more bribes to attract those who will fill the vacuums left by defectors as they will be more strong than ever. The strength of opposition does not come from the types of opposition leaders but from the hardship of regular citizens after they feel marginalised by the rulers who are seen to live porsche lives while themselves are struggling with one meal a day without success.

Hata kikifanya yote hayo hakitaweza kujiimarisha bila kwanza kutoka madarakani!
Kikitoka tu madarakani uchafu wake wote utajitenga! Hapo kitajivua gamba kiukweli na tutaweza kuona kama ni joka kweli ama Jini
 
Ndugu yangu, ccm ilishakufa siku nyingi ila inabebwa na dola tu hawana mbinu yoyote kisiasa. Ndio maana wajuzi wa mambo waliliona hili na kuanza kulilia katiba ambayo itatupatia tume huru. NEC ndio mtajiwa ccm kwa sasa, wakidhibitiwa huko utaona walivyo watupu maana hawajui siasa ila wanapenda kutawala kwa maslahi ya wachache.

Kinga ni bora kuliko kuponya
 
Back
Top Bottom