Sio tu tusichanganye Dini na Siasa, bali pia tusitumie maneno ya Mungu kwa hoja za kisiasa, shuhudia maajabu ya neno "MENE MENE TEKELI NA PERESI'!

Kama maneno MENE MENE TEKELI NA PERESI yalikuwa kwa ajili ya mfalme basi yalikuwa kwa ajili ya mwanasiasa huyo na wajao katika siku zote ulimwenguni.

Maneno katika biblia na Qur'an hayajaandikwa hivi hivi tu bali yana misingi yake na makusudi yake. Pascal angalia hilo.

Maneno matakatifu hutoa funzo, huonya, hukumbusha na kutoa matumaini.

Ama hakika huu ndio wakati wa kuyatumia maneno hayo kuliko wakati mwingine wowote tuliowahi kuupitia Tanzania

nakazia MENE MENE TEKELI NA PERESI!
 
Mkuu naona na wewe umekuwa brainwashed!!
Hivi unafanya kusudi au ndo umeamua kuamini kuwa dini haipaswi kuwa sehemu ya siasa?
Mimi naamini kabisa kuwa tukikataa dini isiwe sehemu ya siasa basi tujiandae kupata wanasiasa wa ovyo ovyo kuliko hawa tulio nao...
Siasa imejaa utapeli mwingi sana.... Dini zinahitajika sana kurekebisha mambo na kuweka checks and balances!!
Tukiwa na viongozi wa dini wanaowaogopa wanasiasa tutaishia pabaya Sana!
I

Hapo ndipo Pascal anashindwa kutofautisha. Dini huzungukia mfumo mzima wa maisha ya mwanadam tangu kale mpaka sasa na wakati ujao duniani na akhera.

Dini inapaswa kuwa sehem ya siasa ili siasa zetu zijali utu , ziepushe kujimwambafai lakini siasa haipaswi kuwa sehemu ya dini.
dini ichanganywe na siasa lakini siasa isichanganywe na dini.
 
Mkuu hiyo Biblia unayosoma wewe ni ya kwako peke yako. Kweli unamtukuza Hitler na Iddi Amin kwa mauaji ya halaiki aliyofanya?
Nitakuombea kwa Mungu wetu aliye hai akuteremshie Roho Mtakatifu upate ulewa mzuri na sahihi wa uelewa wa Biblia Takatifu.

Kama mimi ndiyo naelewa vibaya basi Ukristu wangu hauna maana.

Kwa nini Mungu aliwaepusha wana wa Israel na mateso ya Farao nchini Misri kama Falme zote zinatoka kwa Mungu? (Mwanzo 12:10-20, Mwanzo: 37-50. na Kutoka: 1-40)

Je nao utawala wa Nebucadnezar wa Babeli ulitoka kwa Mungu? Mbona aliwatumia manabii kuwatoa mikononi mwao na kuwarudisha Jerusalem ? (Ezra: 1-10)
Kwenye agano jipya Yesu mwenyewe amejaribiwa mara tatu na Shetani lakini amekaidi akiwa kwenye mfungo wa siku 40. (Luka 4:1-13). Yesu amekataa kumtii Herode alipomtaka ageuze maji ili iwe mvinyo ili amuachie baada ya Wayahudi kumkamata kabla ya kuhukumiwa na Ponsio Pilato.(Luka 23:7-15)

Hii ina maana kuna tawala dhalimu ambazo zinatoka kwa shetani lazima tuzikatae kwa nguvu zote kama Wakristu. Kinyume cha hapo ni kudhalilisha Ukristu wetu.

Utawala wa Magufuri unatoka kwa shetani, siyo kwa Mungu wetu aliye hai, lazima tuukatae kwa nguvu zote. Magufuri hana Mungu kabisa katika matendo na fikra zake. Mtawala anayetoka kwa Mungu hawezi kuwa na roho kama ya Magufuri inayotuma kuua Tundu Lissu, kuua Ben Saanane, Azory Gwanda.

Utawala unaotoka kwa Mungu hauwezi kubomoa nyumba za watu wa Kimara- Mbezi bila kuwafidia halafu ukaacha nyumba za Wasukuma wa Mwanza bila kuzibomoa.

Utawala unatoka kwa Mungu hauwezi kukawafukuza wafanyakazi waliofoji vyeti vya Form IV ili wawe madreva na kumuacha Makonda aliyefoji cheti cha dorm IV na kuwa Mkuu wa Mkoa.

Muache afe au ateseke kitandani yote sawa tu
 
Kuna wakati unapaswa kutii Mungu na sio mamlaka za kidunia. Ushahidi upo Kitabu chs Daniel ambao vijana watatu walikataa "amri halali" ya mfalme wa kusujudia sanamu. Walikubali kufa kuliko kutii amri ya mfalme ingawaje Mungu aliwaokoa na ghadhabu ya mfalme.
Hivyo, kwa sisi Wakristo tunaaswa kutii amri ile tu ambayo haiendi kinyume na maagizo ya Mungu.
 
TUSICHANGANYE DINI NA SIASA. Hivi ni wakati gani hii sentensi hupaswa kutumika.

Sisi tunaoamini Quran ni kitabu kitakatifu tunaamini Mitume wote Rehma na Amani ziwaendee akiwemo Suleiman, Daudi, Mussa, Yesu, Muhammad walikuwa ni kiongozi wa ufamle wa diniani na waliongoza kwa uadilifu kwa matarajio ya kupata ufalme wa mbinguni.

Quran inatuambia katika sura ya 38:26

[ S'AAD - 26 ]
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa (kiongozi) katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.

Hata hivyo mambo mengi yalikuja kubadilika walipoondoka hawa mitume, wakaja watawala waliotawala kwa jina la dini ingawa walitawala kinyume na Maamrisho ya Mungu, na ktk kujiimarisha ktk tawala zao walifikia hadi kuingiza maneno yao ndani ya vitabu vya Mungu na kuwalisha maneno hayo mitume ya Mungu. Likiwemo 'la kaizari mwachie kaizari', tujiulize ikiwa Julius Kaizari alikuja kuwa mtawala mkuu wa rumi miaka 1400 baada ya yesu kuondoka ni vipi Yesu amtaje Kaisari ktk biblia.au ktk uislam kuna msemo 'msiwaseme vibaya wenye mamlaka.' Hata ni maneno ndani ya katiba ya Saudi analishwa mitume wetu, na wala si ktk mafundisho yake.

Na kwa bahati mbaya, neno hili USICHANGANYE DINI NA SIASA kwa Tanzania linatumika pale tu tunapoona kikundi Fulani cha jamii kinapotaka kupokonya haki za walio wengi.

Haki kwa maana zote.

Binafsi naamini Siasa bila dini ni Uwendawazimu na kuchanganya dini na siasa si kosa, Bali kosa ni ubaguzi wa dini kwa kutumia siasa.


https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjABegQIBBAB&usg=AOvVaw2nIzwIK6qbqDYoQaMT7928
 
Mene mene tekeli na peresi ni ujumbe kwa ajili ya viongozi wa chadema wa serikali za mitaa, udiwani na ubunge kwenye chaguzi zinazokuja kuwa wajiandae kuondoka
 
Back
Top Bottom