Sio tu tusichanganye Dini na Siasa, bali pia tusitumie maneno ya Mungu kwa hoja za kisiasa, shuhudia maajabu ya neno "MENE MENE TEKELI NA PERESI'!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,521
113,654
Wanabodi,
Katika uendeshaji wa siasa zetu, tumewahi kuaswa mara nyingi tuu kuwa tusichanganye dini na siasa.

Sisi Wakristo tumefundishwa na Bwana Wetu Yesu Kristo kuwa " Mpeni Mungu Yaliyo ya Kimungu na Mpeni Kaisari Yaliyo ya Kaisari"

Lengo ni kueleza kuwa sisi binadamu tuko kwenye tawala mbili tofauti, au falme mbili tofauti. Falme hizo ni falme za mbingu na falme za duniani. Falme za mbingu ndio ufalme wa Mungu na falme za duniani ni utawala wa Kaisari.

Tumche Mungu na kutii amri zake ikiwemo kufanya yale ya Kimungu ili tuweze kuurithi ufalme wa Mungu, ikiwemo kutimiza wajibu wetu kwa Mungu wetu kwa mujibu wa mafundisho ya dini zetu.

Lakini wakati huo huo tuna wajibu wa kutii mamlaka zote halali za Kaisari kwasababu mamlaka zote huwekwa na Mungu, hata Hitler aliwekwa na Mungu, hata Iddi Amini aliwekwa na Mungu, ni Mungu ndiye ameweka serikali za mataifa hivyo wananchi wote tuna wajibu wa kutii mamlaka za kiserekali kwa kufuata sheria bila shuruti, hata tuwe hatuzipendi vipi mamlaka hizo au hatuwapendi vipi viongozi wake, maadam tumefundishwa kumpa Mungu yaliyo ya Kimungu na kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari, ukienda kinyume, ni kutenda dhambi kwa Mungu.

Mfano hoja ya sadaka, usipomtolea Mungu fungu la kumi ni dhambi, utaadhibiwa kwa kutokufanikiwa. Vivyo hivyo serikali za mataifa zinatoza kodi, usipolipa kodi sio tuu unaikosea mamlaka ya Kaisari, bali pia ni dhambi kwa Mungu kwa kutomiza wajibu wako wa kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari. Hivyo wajemeni tufuate sheria bila shuruti.

Katika kutokuchanganya dini na siasa, mimi nimefanya utafiti wangu mdogo tuu humu jf kuhusu matumizi ya maneno ya Mungu kutoka kwenye vitabu vitakatifu vya dini.

Utafiti wangu, umetumia sampling ya matumizi ya maneno ya Biblia Takatifu Kitabu cha Wafalme. Neno " MENE MENE TEKELI NA PERESI".

Nimefuatilia threads kadhaa zilizotumia neno hilo kisiasa humu jf, nikakutana na an amazing coincidence ya ajabu kuhusu threads hizo,

Kabla sijaisema coincidence hiyo ni nini, naomba nikupe na wewe kaji homework kadogo tuu, zichungulie threads hizi, sio lazima usome contents bali kwa kuzifungua tuu na kuziangalia, can you notice what they have in common?. How can it be?. Is just a coincidence or it is amazing coincidence?.


[/URL]

Kufuata coincidence hiyo, nime reach conclusion kuwa sio tuu hatupaswi kuchanganya dini na siasa, bali pia hatupaswi kutumia maneno ya Mungu, kuwianisha na hoja za kisiasa.

Jumapili Njema
Paskali
Bariadi, Simiyu (near Gambosh)
 
Hata majambazi yakikuteka tii sheria, hata yakikushika matako tulia, hata yakiamua kujirusha na mke wako kuwa mpole tu ili kulinda uhai wako, hapo tumeelewa vizuri mkuu 😀😀😂😂😃😃
 
[QUOTE="Pascal Mayalla, post:
Jumapili Njema
Paskali
Bariadi, Simiyu (near Gambosh)
[/QUOTE]
Naona umeamua kututisha huo mstari wa mwisho,hatutishiki...haaa haaaa
 
1571545925190.jpeg
 
Yohana mbatizaji alivyomkemea Herode kwa uovu wake alichanganya dini na siasa? Nabii Yeremia alipomkemea mfalme mpaka akawekwa shimoni alichanganya dini na siasa? Yesu mara nyingi aliwakemea Waandishi na Mafarisayo alichanganya dini na siasa? Nabii Musa alivyopambana na Farao alichanganya dini na siasa? Dini na siasa kamwe haviwezi kutenganishwa.
 
Yohana mbatizaji alivyomkemea Herode kwa uovu wake alichanganya dini na siasa? Nabii Yeremia alipomkemea mfalme mpaka akawekwa shimoni alichanganya dini na siasa? Yesu mara nyingi aliwakemea Waandishi na Mafarisayo alichanganya dini na siasa? Nabii Musa alivyopambana na Farao alichanganya dini na siasa? Dini na siasa kamwe haviwezi kutenganishwa.

Anacho shindwa kuelewa kwenye Imani tunafundishwa namna ya kuishi vema hapa Duniani kwa namna ya kumpendeza alie juu ya yote haya kwa maana ya Mungu,na kwenye Siasa tuna lazimika kufuata Sheria za Nchi na Matakwa ya Mtu binafsi (Watawala).

Vyote hivyo vina shabihiana tofauti ni kuwa kwenye Imani una hiari ya kuchagua Mema au Mabaya ila kwenye Siasa una lazimika ila vyoote hivyo ni ktk kutengeneza Ustaarabu flani wa hapa Duniani ili pawe Mahali pazuri kwa kuishi Binadamu.
 
Mkuu naona na wewe umekuwa brainwashed!!
Hivi unafanya kusudi au ndo umeamua kuamini kuwa dini haipaswi kuwa sehemu ya siasa?
Mimi naamini kabisa kuwa tukikataa dini isiwe sehemu ya siasa basi tujiandae kupata wanasiasa wa ovyo ovyo kuliko hawa tulio nao...
Siasa imejaa utapeli mwingi sana.... Dini zinahitajika sana kurekebisha mambo na kuweka checks and balances!!
Tukiwa na viongozi wa dini wanaowaogopa wanasiasa tutaishia pabaya Sana!
I
 
Back
Top Bottom