Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,515
Habari wakuu,
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwanza niwape pole single mama katika kipindi kigumu mnachokipitia hasa pale mnapokuwa mmetelekezwa na mimba.
Hakika kipindi hiko ni kipindi ambacho mnapitia mengi sana.
Pia niwapongeze kwa kuamua kuwalea hao watoto na hamkuamua kuwatoa.
Lakini kuna hilo suala la kuongea maneno tena ya uongo na mabaya ambalo mmekuwa mkiwaambia watoto.
Hasira zenu mmekuwa mkizimalizia kwa kunena maneno mabaya tu.
Utakuta mtoto ni mdogo ila anaambiwa kwa hasira kuwa baba yako alikuwa ni mala...
Mmesahau ya kuwa kinywa kinaumba na mauti na uzima yapo kinywani.
Hii imepelekea kuwa na chuki kwa watoto juu ya wazazi wao wa kiume.
Imefikia mahali pa kuwaambia watoto kuwa wazazi wenu wamekufa ila wapo hai
Hili ndio janga lingine kwa kizazi cha watoto wanaolelewa na single mama.
Utakuta mwanamke aliachana na mwanaume ila sasa hasira zile anaharibu uhusiano kati ya baba na mtoto wake.
Inasikitisha sana kuona watoto wanakuwa wakiwa na visasi visivyo na ukweli.
Kuzaa na kuolewa ni jambo lingine ieleweke.
Muache hii tabia kwakweli, sio nzuri maana mnaharibu watoto.