SIMULIZI: Eliza na Ndoa Yangu (Kisa cha kweli cha kusisimua)

Man Middo tz

Senior Member
Sep 9, 2020
154
230
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA KWANZA (01)
man Middo +255 655 969 973

Ilikua 2012 nilipata kumaliza kidato cha 4. Nilijijua kuwa nitafeli tu kutokana na sababu ambazo ndugu na mama yangu walijua.

Kwanza kipindi hicho nilikua naumwa sana na nilikua nanguka ghafla sikujua kwa kipindi hicho kama ni presha. Mama yangu alikua akiniasa nisome sana kwa bidii na nihakikishe nafaulu.

Sasa kila nikikumbuka hayo masuala ya kuambiwa nihakikishe nafaulu najikuta nanguka ghafla nakupoteza fahamu, kwa wakati huo nilikua bonge na kilo 80. Mama yangu alikua asikari magereza hivyo niliogopa sana. Nakumbuka kipindi cha mtihani wa moko nilianguka presha nikajikuta nipo hospitali.

Baadae dokta aliniuliza kama kuna vitisho vyovyote napewa na wazazi wangu, ni kweli nilikua natishiwa. Baadae mama aliitwa nakuambiwa Kama ataendelea kunisistizia kuhusu shule anaweza kunipoteza, hivyo baadae waliona bora nifeli tu lakini niwe hai.

Nilipomaliza kidato cha nne nilikuja kutamani kusomea Hotel Management. Nilipenda hiyo kozi kwakua niliona kwanza rahisi kwa upande wangu pia ada ya kawaida sana kwa wakati huo. Harafu sababu nyingine chuo kilikua karibu na nyumbani.

Niliomba nakuchaguliwa katika chuo kille ambacho kilikua Morogoro, nikanza kusoma pale chuo muda huo ile hali ya kuanguka ishanza kupotea.

Sasa katika wanafunzi wote wakike Mimi kwa upande mmoja au mwingine nilikua nateseka sana, haswa upande wa kifedha maana mzazi wangu alikua ananipa elfu 30 nitumie mwezi mzima, halafu tunajitegemea kwa kula wenyewe. Sisemi hiyo ni hela ndogo hapana ila kama msichana bajeti yangu ilistahili kuwa kubwa kidogo kulingana na sababu za hapa na pale nazani hapo mnanielewa.

Hivyo hali ikawa ngumu kwangu, nilikua mnyonge sana mbele za wenzangu pale chuoni, kutokana na hayo niliamua kila ijumaa niwe narudi nyumbani ili jumapili niwe narudi chuo.

Sababu kuu za kurudi ilikua kupunguza gharama nikiwa chuoni. Maisha yaliendelea hivyo, sasa ikawa wenzangu wakagundua kwa kiasi maisha yangu yalivyo yakinyonge, wakanza kunidharau sana na kuniona mjinga sana.

Dhihaka za hapa na pale kwakua tu sikuwa na mavazi mazuri zaidi yao, pia sikuwa na pesa.

Lakin mpenzi niliyekua nae kwenye mahusiano alikua maskini sana kiasi kwamba kunipa pesa kubwa sana ilikua elfu 5, sio kwamba alikua mchoyo hapana ndicho alicho barikiwa kwa kipindi kile.

Pia ukiachilia mbali kutokua na pesa pia alikua na wivu sana, alikua ananipenda Sana na mimi nilimpenda sana ila suala lake la wivu ilikuja kunichosha mnoo.

Hali hiyo yakua na wivu usio wa kawaida ulikuja kusababisha kuanza kupishana kiswahili mwishoni. Kipindi naanza chuo alikua anakuja kunichukua kila ijumaa nakurudi wote nyumbani, ukiachilia mbali wivu ila nilikua naboreka sana kwa kunichukulia dhaifu kwani aliamini nikirudi peke yangu nitatongozwa, ndio sio tatizo kutongozwa ila kunichukulia nitamkubali tu kila atakaenitongoza sikupenda kabisa.

Basi katika hayo yote kuna rafiki yangu mmoja nilikuja kumgundua kuwa ni mnafiki kwasababu alipenda kutusifia na kupenda jinsi tunavyoishi katika mahusiano yetu na mpenzi wangu japo hatuna pesa, kumbe alikua mnafiki kwasababu alijipendekeza kwa boy wangu na baadae akaanza kumpa taarifa za uongo.

Kipindi hicho mimi nipo chuo kama nilivyosema nasomea hotel management ila mpenzi wangu yeye hakua na kazi yoyote ya maana, alipenda sana kucheza mpira pale kijijini na kukaa kijiweni tu kitendo ambacho mimi sikupenda kwasababu niliwaza maisha yetu ya baadae yatakuaje.

Kutokana na hayo nilianza kumshauri mwenzangu kuwa ni heli atafute kazi yeyote au asomee ufundi, nilimshauri hivyo kwa maana mimi nikimaliza kusoma nitapanga chumba na siwezi kuolewa wakati hatuna uwezo.

Mwenzangu pamoja na kumshauri lakini hakuitikia kwa kumaanisha ila alikua anaishi akusema nitangalia huku yupo tu kijiweni, nilikua naumia sana maana hajishughulishi kwachochote.

Nilikua na kwaida ya kwenda kwao na kuna baadhi ya siku maalum hua naenda kwao, na mara zote katika siku hizo ilikua hawezi kwenda popote lazima anisubirie kwakua nakua lazima nitaenda tuu.

Basi siku moja nilimfuata kwao ila nilishangaaa siku hiyo kwa mara yakwanza sikumkuta, nikarudi nyumbani kwetu, kwao yeye ni kijiji cha pili. Baadae nikarudi tena sikumkuta kuuliza wakaniambia yupo mpirani.

Nilienda hadi uwanjani na kweli nikamkuta uwanjani na ilikua desturi yetu kuwa nikienda mpaka uwanjani huwa lazma atoke uwanjani anifuate lakini sikuile hakufanya hivyo.

Sikua na hiyana nilisubiria hadi alivyo toka tukaanza kurudi huku kanuna hakuwa sawa kivile, nilistuka kwakua sio kawaida yake kuwa vile ikanibidi nimulize

“mh! Niambie vip mbona hukunipa jibu umefikia wapi kuhusu kujisomesha?''
alinijibu jibu moja kwa ukali na kwa jazba

''Kama umepata mpenzi mwenye kazi au mwenye uwezo kuwa nae tu mimi sipo tayar kuoa leo wala kesho….''

Aiseeee niliumia niliumia sanaaaa yan nilitamani ardhi ipasuke, kwanza hajawahi nijibu vibaya wala kunidharau hata siku moja nilibaki kumshangaa nikamjibu sasa huku machozi yanatoka moyon niliapa kuwa

“Mimi Eliza kuja kurudi hapa kumfuata huyu mwanaume sitorudia tena labda sio mimi, kama kumpenda huyu mwanaume imekua fimbo basi liwalo na liwe”

Kiukweli nilikua nampenda sana kwasababu nishawahi kunywa hadi sumu kwajili yake, nishawahi kulazwa hospital mara mbili kwajili yake, na leo tena yajirudie yale yale! Hapana aisee siwez nimeshindwa.

Nilirudi chuo lakin usingizi kuupata ilikua shida. Kiukweli nilikua nampenda sana boyfriend wangu na yeye niliamini ananipenda kutokana na wivu wake aliokua ananionyesha.

****

Baada ya kuzozana na boyfriend wangu nikapata nguvu baada ya siku kadhaa. Siku hiyo nikarudi zangu nyumbani, sasa kawaida kila kiwa narudi chuoni kutoka nyumbani lazima nipitie kwa boy wangu lakini sku hiyo sikupitia kutokana na kunidharau na maneno yake.

Basi njiani wakati narudi chuoni nikiwa natoka kushuka daladala kuelekea chuo nikaona ghafla kuna gari inapunguza mwendo taratibu huku kama naitwa lakin nikapuzia wala sikuitikia.

Kwanza mimi niliamin wanaume wenye magari wengi wameazima, pili wengi niliamini ni malaya halafu kwakua sikuiwekea maanani niliona kama mkubwa sana kwangu na ukizingati pia sikuzoea kusimamishwa njiani.

Niliendelea tu kutembea lakini nikaona mtu hachoki tu, mmh! nikaamua kuzuga kuingia dukani. Nilikaa humo dukani kwa dakika kadhaa badae nikatoka nikajua atakua kakata tamaa kaondoka.

Hee! Ghafla kumbe alipaki pembeni akanza kunita tena mmh! nikaona huyu asije akajua ninapo soma ikawa mtihani maana sikupenda usumbufu kabisa. Nilichofanaya nikamuliza

“Unasemaje?” akanambia

“Tusiongee sana inaonekana unaharaka ila naomba namba yako nitakutafuta”

“Sina simu”

Nilijibu kwa haraka ili niondoke zangu lakini nikaona anatafuta pen ila hakupata nilifurahi sana, aah! Katika kupekua akapata makapen akanipa namba yake kisha akanisihi sana nimtafute............... ITAENDELEA.

SWALI WAKINA KAKA ULITUMIA NJIA GANI HADI KUMPATA ULIYENAE AU NDIO HII NJIA MAARUFU YA KUOMBA NAMBA TU?

NUKUU “Muda mwingine mdada anafuatwa na mtu anampuuza puuza kumbe ndio mume wake bila kujua, Siku zote ikipangwa imepangwa tu huwezi kuipangua.

Utakwepa kwepa lakini mwishoe pete inanasa kidoleni kama ishara ya pingu za maisha. Muangalie na mchunguze kwa makini huyo anaekufuatilia ujiridhishe ndio ukubali maana hujui ya kesho unaweza kukubali kwa kumzuga kumbe ndio nitolee, watu wengine huwezi kuwazuga ukikubali umekubali” soma kifuatacho hapa hapa kwa

man Middo on FB
@middotz_ on Instagram
@manmiddo on Twitter
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA PILI
Man Middo tz +255 655 969 973

ILIPOISHIA…………. akanambia “Tusiongee sana inaonekana unaharaka ila naomba namba yako nikakutafuta” “Sina simu” Nilijibu kwa haraka ili niondoke zangu lakini nikaona anatafuta pen ila hakupata nilifurahi sana, aah! Katika kupekua akapata makapen akanipa namba yake kisha akanisihi sana nimtafute...............SONGANAYO

Baada ya kuchukua ile namba nikaondoka zangu huku nikimuona amesimama na gari yake, nilihisi atakua akinisindikiza kwa macho ila maajabu mimi hata sikumtazama usoni.

Basi nilifika hostel nikawahadithia wenzangu jinsi yule mzee alivyonifuatilia, kwanza niliwambia

“kuna libabu limenichelewesha njian na kigari chake”

Basi tukacheka pale baadae nikachukua ile namba nikaweka kwenye mkoba wangu. Mkoba ambao nilikua nimetundika ukutani ndani yake nilijaza namba na business card nilizopewaga na wanaume walionisimamisha njiani lakin sikuwahi kuwatafuta.

Kwa kweli nilikua nimemzoea boyfriend wangu na sio kumzoea tu ila nilikua nampenda mnoo japo alianza kunizingua.

Basi siku ikaisha ikafika usiku nikalala zangu, sasa usiku kila nikigeuka usingiz hauji nikawa nakumbuka tu yule mtu jinsi alivyonipa namba, mmh! Nilistuka Sana niliamka nikawaza Sana

''MMH! Mbona wanaume wengi walinipa namba lakin sikuwahi kuwawaza hivi?''

Baada ya kuona sipati jibu niliamua kuwaamsha wenzangu. Waliamka nikawambia wakaanza kutoa ushauri kila mmoja

''Eliza huenda uyo ndo Mume wako Mungu kakupangia'' Nikacheka nikisema

“Mwanaume mwenyewe mweusi”Kipindi kile nilikua siwapendi wanaume weusi.

Basi nikawambia kesho nitajaribu kumtafuta lakin sio kwa simu yangu kwasababu nilimuambia sina simu.

Tukakubaliana pale na Halima (huyu ni yule rafiki yangu anayejifanya napenda mahusiano yetu na boyfriend wangu)
akaniambia usijali utatumia simu yangu.

Basi tukalala pale ilivyofika asubuhi tuliamka nakufanya usafi nakumbuka ilikua siku ya jumapili. Tulivyomaliza usafi tukiwa tumeoga tayar Halima akaniuliza

''Vipi humtafuti yule mtu?''

''Mh! Basi ngoja nimtafute'' nilimjibu, tukapiga simu (Yaani najuta kwanini nilimtafuta bora ningechana namba tu)

***

Nikampigia akapokea akauliza

“Hlw naongea na nani?” Nikajibu

“Ni mimi Agness” nilidanganya jina, akauliza

“Yupi nikumbushe?”

“Ulinipa namba jana usiku!” (Yani ilikua kwenye simu tu lakin alifurahi sana)

Basi akanza kuuliza maswali mfululizo

''Ahaa! ok! Niambie za asubuhi? Umeamkaje? Upo wapi kwasasa? Naweza kukuona? Umekunywa chai?”

Wakati wote huo nilikua nikijibu maswali yake, lakin alikua mtu asiyeamini kuwa ningemtafuta kwasababu wakati akinipa namba nilikua natabasamu mithili ya mtu anayepuuzia na kweli sikupanga kumpigia. Basi nikamjibu

“Nipo hostel na unaweza kuniona harafu bado sijanywa chai” (nikajifunza kauongo) akanimbia

“Nipe dakika 10 uanze kunielekeza”

“sawa” Nikajibu.

Nikamwambia rafiki yangu anakuja sijui itakuaje! Tumbo likanza kunguruma kama naendesha kwa uoga sikuwahi simamma na mwanaume njiani au kuniita sehemu zaid ya boyfriend wangu.

Dakika 10 zilifika akapiga nikatoka na rafiki yangu Halima maana simu ilikua yake na pia nilitaka aone jinsi ninavyotekwa nilikua muoga sana.

Basi nikamuelekeza hapo ila hakuelewa hadi nikaanza kuchukia ila baadae nikamuelekeza kwa njia nyingine ya kutokea stand, kweli akaelewa akafika tukaonana.

Alikuja na gari ya kifahari ilikua tofauti na ile ya jana yake usiku, sikujua ni gari ya aina gani lakini pia mimi sikujali gari wala nini.

Basi wakati namfuata alikua ananichora tu ninavyotembea na tege langu. Nikafika nikaingia kwenye gari, nilishangaa tofauti namafikirio yangu ya jana kumbe ni kijana bwana ila alikua na aibu sana kwani hakuweza hata kuningalia usoni.

‘‘Hapa unafanya nin?''

''Nasoma'' nilijibu ''Nimerisit' niliongezea jibu (nilidanganya)

“Ahaa! kumbe mwanafunzi?”nikajibu

“ndio” akauliza

“kidato cha nagapi?” Nikajibu

“Cha pili”, akaniambia

“Ok! Jitahidi sana kusoma naamin mimi sitokua sababu ya wewe kufeli”.

Akaendelea kaniambia

“Nilikuja tu kukusalimia kesho nitaenda sehemu ila nikirudi nitakuja tena kukusalimia na nimekuletea vitafunwa hapa”

(Alileta mkate mkubwa, mawaziwa ya nido, Blueband, sukari kg zaid ya 5 na box la majani ya chai) Nilibaki nashangaa tu.

Nikamshukuru sana akanipa elf 5 akaniambia ya vocha nikashukuru sana.

Kabla ya kushuka kwenye gari nikajikuta namkiss kwa nia ya kumuaga maana nilishazoea kwa boyfriend wangu.

Alizubaa akaniangalia nilijikuta navutiwa na macho yake flan ivi Amazing kwa kweli niliyapenda sana, na hapo ndo nilifaidi sura yake. Nikashuka nakuelekea zangu hostel, Lakini kabla sijafika nikakutana na mwalimu wangu wa mapishi.............. ITENDELEA.

JE MWALIMU WAKE ATAMFANYAJE NA KIFURUSHI CHAKE? USIKOSE KIFUATACHO HAPA KWA man Middo.

NUKUU “Siku zote mahusiano huanza kwa namna ya ajabu sana ambayo kila mmoja anajikuta tu yupo kwenye mahusiano na wakati huo yashapamba moto hata kujinausua huwezi tena.

Mara nyingi wakati huu unanza kusema mbona sijamchunguza na kwakua moyo ushazama huwezi kuwaza baya juu yake, huwazi akikusaliti, hufikirii kama alikua na mahusiano mengine ila hapo unawaza tu kwakua yeye anakupenda na wewe unampenda.

Ukiwaza matokeo chanya ni lazima pia Uwazie matokeo hasi hivyo ndivyo ilivyo.

Kwenye POSTIVE lazima patakua na NEGATIVE pia. Ukiwaza unapendwa sana waza pia kama anakudanganya itakuaje” Ni Man Middo #2022.

Follow me on Twitter @manMiddo
 
ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA TATU
Man Middo tz +255 655 969 973

ILIPOISHIA…………..Kabla ya kushuka kwenye gari nikajikuta namkiss kwa nia ya kumuaga maana nilishazoea kwa boyfriend wangu. Alizubaa akaniangalia nilijikuta navutiwa na macho yake flan ivi Amazing kwa kweli niliyapenda sana, na hapo ndo nilifaid sura yake. Nikashuka nakuelekea zangu hostel, Lakini kabla sijafika nikakutana na mwalimu wangu wa mapishi…………..SONGANAYO.

Kabla sijafika chuo nikakutana na mwalimu wangu wa mapishi akaniuliza

“Umetoka dukani”nikajibu

“Hapana nilikua kupokea vitu kutoka kwa ndugu yangu” akasema

“Mmh ivi vitu mtahalisha hamjazoea jamani”

Basi akachukua maziwa ya nido na mkate nusu ulikua wa silesi na sukari nusu, tukacheka pale nikarudi zangu hostel. Kufika nilikuta Halima kachoka kusubiria yaani kachoka balaa.

Basi nilivyofika na mizigo room nzima walishangaaa sana kwanza walizoea kuona meza yangu ikiwa tupu zaid ya mswaki na dawa ya meno na madaftari pia. Meza za wenzangu zilikua na vitu vingi vya garama ikiwemo rosheni majuisi ya kopo, sukari, mikate na vitu vingine.

Pale room mimi nilionekana mtu wa hali ya chini sana kiasi kwamba waliniona fukala flani ivi, kwanza walinitenga hadi kula maana kuna kipindi tulikua tunapika kwa kuchanga pamoja, lakini eti ikaonekana mimi maskini siwez kuchangia kwahiyo ikawa kama sina hela nalala njaa tu mpaka nisubirie mama atume au nirudi nyumbani.

Basi nikawa natoa vile vitu walibaki wanashangaaa tu, kuna mdada mmoja anaitwa Vick alibaki kununa tu kwani alikua hanipendi. Vicky hanipendi kwasababu mimi nilionekana ni mzuri chuo kizima japo sina hela (sikua na matunzo) lakin Vick pesa ya urembo ilimbeba kwahiyo akawa hapendi kuambiwa kuwa mimi ni mzuri zaid yake.

Hivyo alipenda sana aitwe mrembo wa chuo ila mim sikuonaga uzuri wake. Basi nikapika chai pale tukanywa nilivyomaliza nikalala, ilivyofika mchana simu ikaita Halima akaniletea alikua yule boy mpya aliitwa Mudy nikapokea akaniuliza

“vipi unaweza kupata chakula cha mchana pamoja” nikajibu

“Ndio” akanambia

“OK nitakuja kukuchukua mchana hapo”

Sasa wakati naongea jasho linanitoka mwili mzima, nikajibu

“Ila utanisamehe sitokuja peke yangu” akajibu

“Mimi sio wahivyo wewe njoo nao hata 10”

Kidogo nikapata ahueni nikamwambia tatizo hostel huwa hawaruhusu mwanafunzi kutoka pekeako aliwahi kupotea mwanafunzi, na hapa wengi wageni alinielewa pale.

Baadae akaja kutuchukua, kweli tukaenda hadi hapo hotelini tukashuka Mimi na rafiki yangu Halima (Kipindi hicho Halima aliinjoi japo alikua mnafiki) Mudy akaniita akanambia

“Sorry mpenzi (kwa mara ya kwanza alinita hivyo) naomba nikukute mnaendelea Mimi naenda kupeleka gari waioshe”

Akanipa elfu 10 harafu akanambia agizeni chochote ata kikizidi hiyo pesa nakuja kulipa.

Basi nikaingia na rafiki yangu Halima, (hapo nguo niliyovaaa nimepekua begi zima yani) tukafika tukakaaa ikaletwa menyu tukawa tunasoma menyu tukagiza chipsi nyama yai. Baadae akaja akacheka sana akasema

“Nilijua tu lazma muagize chipsi si ndo kawaida yenu wanafunzi”

Akamuita mhudumu akamwambia wape kuku mbili. Basi baada ya mhudumu kuleta tukanza kula kuku tukaachana na mishkaki, akaanza kuniuliza maswali lakin kwakua nilikua na rafiki yangu sikuhofia chochote, katika maswali yake ...aligundua kuwa Mimi mnyakyusa halafu kwetu mbeya.

Akanambia ile safari niliyokwambia ndio naenda Mbeya! Mimi nikafrahi kusikia hivyo nikamtajia mitaa ya kwetu akasema amefika huko na ndo boss wake aliko huko, mimi nilibaki nashangaaa tu!

Akaniomba afike kwa hata ndugu akamsalimie nikakataa nikamwambia mbona mapema. Kweli aliachana nayo na kuendelea kula tulivyomaliza kula vingine tukabeba! (Nikaona naachaje kuku aisee wakatupwe hahaha si unyoko huu) akanambia

“Nimekupenda na nimekukubali huigizi maisha umekula na umebeba wengine hushia kugusa gusa tu eti warembo”

Tukacheka (ningejua neno nyoko kipindi hicho ningemuambia hao ndo Nyokoz), Basi akaniuliza

“Mwisho sangapi kuwa nje ya hostel”

“Kwa kawaida mwisho saa moja join”

Basi akasema twendeni sehemu nyingine tukaenda hiyo sehemu nilishiaga kuiona kwenye TV tu ila siku hiyo ndo niliona “LIVE” tukafika akamwomba rafiki yangu akae sehemu tofaut na sisi kidogo ili awe huru……..

*******

Basi tukakaaa sehemu wenyewe akanza kunielezea historia yake, alianza kuniambia kuwa anaishi Pwani, hana mke wala mpenzi lakini ana uwezo kiasi flani wa kipesa sio tajir ila kiasi flani anajimudu. Akasema kuwa huwa wanawake kwake wanafuata pesa tu na si kitu kingine chochote kile kwahiyo anatafuta mpenzi atakae kuwa mke wake kwani amechoka utapeli wamapenzi kwa watu wengine (sasa kweli muda huo mimi pia nilikuaga natafuta mpenzi mwingine moyoni ambaye hatokuwa akinionea wivu muda wote) akanambia

“Nimejenga nina nyumba” (moyoni niliona afadhali maana kipindi kile nilichoka kufanya mapenzi na boyfriend wangu kwenye mageto ya kuazima nilichoka na siku nyingine tulisubiria wenzetu watoke sisi tuingie maana hatukuwa na pesa ya guest sasa).

Basi nikamwambia

“Usijali mimi pia nimetoka kuachana na mtu” ila sikumpa sababu nikamuliza

“Kwanini mpaka saivi hujaoa?”

(Maana nilivyomuona nilikuaga nahisi ni mume wa mtu yani sikuamini ghafla kuwa yupo single) akaniambia

“Siku ukija kwangu utajua ukwel”

Basi nikamwambia ukweli kuwa naitwa Eliza nasomea Hotel management si kweli kuwa narisit akakubali tukapeana romance (nilihisi msisimko wa ajabu tofauti na kwa yule boyfriend wangu wa mwanzo) akaniuliza

“Nikienda mbeya kesho nikirudi nikuletee nini?” nikamwambia

“Mimi ndizi na maziwa” alicheka sana

“OK nitakuletea mnyakyusa” Baada ya hapo akaniambia

“Nahitaji uwe na simu yako binafsi sitaki ya huyo rafiki yako” nikamwambia sawa akanipa elfu 15 kama ya vocha.

Baada ya hapo akaturudisha hostel, Maisha yalianza kuwa mengine sasa na baada ya kama siku 3 akarudi kutoka mbeya................ITAENDELEA.

JE ALILETEWA ZAWADI ZAKE ZA NDIZI AU ALIMDANGANYA?

KIPI KINGINE KILIENDELEA?

BASI ILIKUJUA USIKOSE SEHEMU YA NNE HAPA KWA Man Middo tz

NUKUU “Mahaba bhna wee! Manjonjo ndio kila kitu tazama kuna mtu anaachwa solemba uko, huku upande wa pili mtu ashapata hifadhi kimasihara tu.

Mtu anasubiri arudi Mbeya wanze kufanya yao, ile bajeti ya elfu 30 kwa mwezi ishanza kusahaulika unambiwa matunzo ndio yananza kutolewa uko” Hiyo ndio ELIZA NA NDOA YANGU tusonge nayo hadi kwenyye hiyo ndoa.

Man Middo tz
Twitter @middotz_
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA NNE
Man Middo +255 655 969 973

……………….“Nikienda mbeya kesho nikirudi nikuletee nini?” nikamwambia “Mimi ndizi na maziwa” alicheka sana “OK nitakuletea mnyakyusa” Baada ya hapo akaniambia “Nahitaji uwe na simu yako binafsi sitaki ya huyo rafki yako” nikamwambia sawa akanipa elfu 15 kama ya vocha. Baada ya hapo akaturudisha hostel, Maisha yalianza kuwa mengine sasa na baada ya kama siku 3 akarudi kutoka mbeya..............SONGANAYO.

Baada ya kama siku 3 akarudi kutoka mbeya, kweli alituletea ndizi kibao na maziwa alikua bize mno alinishushia tu kwenye gari akanambia nina haraka kuna taarifa napeleka kwa boss then nirudi kwangu pwani hapo ilikua ni Morogoro.

Aliondoka aliahidi wikiendi ijayo atakuja kuniletea simu ili tupange mambo yanayohusu penzi letu. Akaondoka akaniacha na maswali kibao halafu nilishamzoea yaani nilijikuta ghafla kaingia moyoni japo haikua kivile.

Baada ya wiki moja akanipigia simu akaniambia kuwa alikua anaumwa ndo maana hakuja kuniletea simu akasema amemtuma mtu akanunue akishaleta anapanga kuja.

Basi nikampa pole nyingi sana sikumbuki ilikua siku gani ila ilikua katikati ya wiki, ilivyofika jumamosi moja akaniita nje ya chuo lakin kama kwaida yangu nikamuuliza kama naweza kwenda na rafiki yangu.

Aliniruhusu nikaenda nje ya chuo nikamkuta yupo na taxi tukapanda akatupeleka hadi kwenye garden flan ivi nzur kwa kweli.

Yeye kwakua hatumii kilevi chochote alikua hapendi kujichanganya sehemu zenye starehe sana hasa unywaji wa pombe.

Tulikaa sehemu akaanza kutoa vitu alivyo ninunulia ilikua laptop, simu kubwa ya smart samsung Galax, kipindi hicho sijawahi kutumia smart na pia sijawahi kuwa na simu nzuri kama ile.

Nilifurahi halafu nilikua simuamini kabisa nilijua muigizaji tu, Akanza kunipiga picha nikampiga picha na yeye tukawa tunainjoy sana. Akaningizia nyimbo kwenye simu yangu ile mpya ila kuna wimbo mmoja ivi aliupenda sana sikumbuki jina wala msanii aliyeimba nakumbuka tu ile video yake tu.

Baadae akaniwekea na mimi nikajikuta naupenda ghafla, akaniuliza

“Vip rafiki yako ni mtu mzur kwako”
Nikamwambia

“sijui yeye awe na roho mbaya yake kikubwa mimi nakupenda na sina mwingine”.

Alinisihi sana kwani alishakua na mwanamke ambaye alimpenda sana na alimpa kila kitu lakin akaja kumsaliti tena hadi na rafiki yake.

Mimi nikamwambia kuwa sioni sababu yakumuacha hata ingekua nini ila kuna tatizo kwani mimi na yeye ni dini tofauti,( yeye ni Muislam na mim ni Mkristo) nikamwambia

“Siwezi kabsa kuishi na wewe kwakua Dini tofauti na mamangu hapendi kabsa dini hiyo maana Baba yangu alikua dini hiyo halafu alimtesa sana mama hadi ndugu walimchukia kwakua dini tofaut hadi waliachana kwahiyo huwa hapendi mtu yeyote aingie uko itakuwa ngumu sana” akanambia

“Kuhusu dini usijali mimi nitajua namna yakufanya, wewe relax tu nitaanza kuongea na dada yako”

Nikaitikia tu (lakini kutoka moyoni niliamini akinipenda tu kwa dhati atakuwa mume wangu asipo nipenda tu siwez kuolewa nae kwanza dini tofauti)

Baadae akanisihi nikifikia kipindi cha field nijitahidi kuanza kuwataarifu wazazi tufunge ndoa maisha yaendelee nikakubali.

Basi tukaruudi sehemu tuliyomwacha rafiki yangu, wakati tunatembea kurudi alipo rafiki yangu akanza kuniuliza

"Kwa mwezi unatumia kiasi gani?”
“Elfu 30” nilijibu alishangaa sana akacheka akaniambia

“Sikudhaarau ila nimekupenda nikiishi na wewe bajeti haitasumbua kingine maendeleo yatapatikana”

Mimi nilibaki kutabasam tu na kuitikia. Baada ya hapo akanipangia bajeti mpya akasema

“Kwa mwezi nitakuhakikishia unatumia laki na zaid , kwa wiki nitakua nakutumia elfu 70 kila siku uwe unatumia elfu 7 halafu elfu 3 uwe unanunua vocha ila nakuomba sana usijiunge facebook sipendi mtu ninaempenda awe facebook”

Akanionya sana kuwa fb wengi Malaya tu na mimi nikaamini kwa kuwa kipindi hicho sikujua kabisa kuhusu mitandao ya kijamii.

Basi akanipa laki na nusu akaniambia chukua hii yote nunua nguo, kwa kweli nilifrahi sana tena sana, tulipomaliza wakati huo tushafika kwa rafiki yangu Halima akaita tax ileile iliyotuleta tukaingia tukaondoka tukafika mitaa ya bank akashuka akaenda kutoa hela akaja akanipa tena elfu 50 rafki yangu akampa elfu 20 akanikiss mdomoni.

Kwa mara ya kwanza yeye ndo alinikiss nilihisi kama nimepigwa shoti hivi sikuamini kabisa nilijihisi napendwa sana akaniaga

(wakati huo dereva alitoa macho tu na rafiki yangu aliishia kutamani tu kwa kweli rafiki yangu nilimjua sana kuwa mnafki ila sikutaka tu kuwa natoka peke yangu kwa mtu nisiye mzoea sana) akanambia

“Kwaheri nakupenda”

Kisha akamwagiza dereva atufikishe hadi chuo ndani. Kweli tukafika hadi chuo na simu yangu mpya na laki mbili keshi kwa mara ya kwanza sikuwahi shika pesa nyingi kama ile (kwa kipindi hicho) nilifika room kwetu nilifrahi sana kupata mkombozi wa njaa na pia mkombozi wa dharau za pale chuoni nilidharaulika sana kuwa eti mimi mzuri nisie na matunzo.

Basi baadae nikiwa nimepumzika nikawaza sana

“Hivi nilichelewa wapi kula pesa hizi maana sio kwazarau za boyfriend wangu wa mwanzo nilimpenda sana halafu cha ajabu alikua haniamini hata kidogo na aliona rahisi sana kupata mtu kama Mimi”

Basi eti baada ya hapo hostel nzima wakaanza kuniheshimu. Sasa wivu tu ndo ukawajaaa rafiki yangu yule akawa anang’ata na kupuliza sikujali maana ndo alikua mtu anaenifariji kiasi.

Nikaendelea kuwasiliana na Mudy lakin mara nyingi mimi ndio nilimtafuta yeye alikua akinitafuta usiku tu ila Mimi asuhuhi kabla sijaingia tu darasani salamu, mchana nikirudi salamu kama hatojibu kwa sms basi atapiga simu.

Nilikaa kama miezi 3 kasoro nikanza kutamani kufanya tendo la ndoa nae lakin alinisihi tuwe wavumilivu mpaka tutakapo karibia kumaliza muhula pale chuon ndo niende kwake.

Lakini umumilivu ulinishinda niliishia tu kumiss sana kuliko hata nilivyo kuwa nammiss kwa boyfrend wangu wa kwanza ambaye kwa kipindi hicho alishakuaga ex wangu.

Kuna siku alipanga kuja ila mambo yakaingiliana hakuja basi akaja ghafla tu siku nyingine akauliza unaweza kulala nje ya chuo nikajibu ndio kwajili yako tu (nilifurahi kwa kweli kwani nilitaman sana)

Siku hiyo ilikua ndo siku ya kujua mwamaume rijali yukoje yaan…................. …ITAENDELEA.

JE UNAJUA KILICHOTOKEA HUKO NJE YA CHUO?

USIKOSE KIFUATACHO.

NUKUU “Mtege uwezavyo, mkatae uwezavyo, msumbue uwezavyo lakini jitahidi pia usijekuingia kwenye mtego wake.

Wadada wakishaingiaga kwenye mitego ya maboy wao haswa wale ambao waliwachukulia kama sehemu ya kupita tu, huwa wanaingia kweli kweli na bahati mbaya watu kama hawa akifanya tu mimba hiyo sijui kitakachotokea kwa Eliza ila kama ametamani na kukurupuka kulala nje ya chuo shughuli imeisha”

Nifollow Twitter @middotz_
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 5
Man Middo tz +255 655 969 973

ILIPOISHIA……………Lakini umumilivu ulinishinda niliishia tu kumiss sana kuliko hata nilivyo kuwa nammiss kwa boyfrend wangu wa kwanza ambaye kwa kipindi hicho alishakuaga ex wangu.

Kuna siku alipanga kuja ila mambo yakaingiliana hakuja basi akaja ghafla tu siku nyingine akauliza unaweza kulala nje ya chuo nikajibu ndio kwajili yako tu (nilifurahi kwa kweli kwani nilitaman sana) siku hiyo ilikua ndo siku ya kujua mwamaume rijali yukoje yaan…………..SONGANAYO.

Basi aliniambia njoo sehemu flani (mtaa umenitoka) panda boda boda kwel nikapanda boda boda nikashuka kituoni aliponiagiza.

(wakati huo ilikua miezi miwili hatujaonana ila ananitumia pesa tu vizuri kwa wiki 70 na 30 emergence)

Pale kituo cha boda watu walikua wananishangaa sikujua ni kitu gani mpaka wananishangaa, nikampigia kumuambia

“Nimefika uko wapi?” akaniambia

“Duuh!!!! Nimekuona watu wanavyo kutolea macho tu umependeza hatari, yani umebadilika sana”

Nikacheka tu kuna mtu akawa ananiita nikamuona nikamfuata ila kuna mwanaume alikua ananifuata kwa nyuma kwa kweli alishiwa pozi nilivyo mfikia Mudy akarudi kwa aibu.

*****

Basi tukanza safar yakwemda alipofikia tukafika nilikuta kaja na laptop yake akanza kufanya mambo yake mimi nikiwa nimelala kitandani sasa nikawa nashangaa

“Huyu mwanaume vipi si tulipanga tuje kufurahi kulikoni sasa anaanza kazi tena”

Mimi nikaanza kuchat na rafki yangu chuo nikamjuza akanambia

“Eliza rafiki yangu asije kuwa mgonjwa kwanini yupo bize na kazi wakati ndo katoka kazini” akanipa mbinu sasa, akasema

“Hebu nenda kaoge vaa taulo kisha rudi tupa taulo mwite halafu tuone, mbona hapindui”

Kwel nikafanya hivyo kwel alivyo geuka kukuta tu nipo vile alibadilika akaja akanambia:

“Kumbe sikukosea kukupata wewe mzuri, wewe mrembo kuliko nilivyo dhani, ushawahi lala na mtu kweli?” nikajibu

“Ndio” tukanza kuandaana, nikamwambia

“Umeandaa condom?”

“Hapana” nikamwambia

“Sasa itakuaje mimi naogopa siwezi bila condom (Yani na stimu zote zilikata) akanambia

“Usijali mimi ni mzima na wewe pia nakuamini tufanye sitokupa mimba nitamwaga nje japo ngumu sana lakini nitajitaid please”

Sikutaka mabishano sana nilimkubalia hata hivyo nilikua na matatizo ya tumbo huenda sitopata mimba (nilijiwazia) mmh!

Kwa kweli nillinjoi sana hadi leo nakumbuka, alipomaliza alinibusu alinibusu mno akaniambia

“Wewe mbona mpyaa! Kweli umewahi kutana na mwanaume? basi kama umewahi ni mtoto mwenzio maana si kwa utamu huu”

Ilivyofika asubuhi akanimwagia pesa mwili mzima akanambia

“Hizi nakupa za kujitunza kwako sijawahi waza kupata msichana wa aina yako”

Yaani nilifaidi utamu wake kwa kweli, Basi mimi nikawa najiuliza inamana yule wa kwanza alikua hajui au kwakua mtoto mwenzangu.

Mmh! basi ilifika asubuhi kwa kweli ilikua zaid ya utamu maana hadi chozi lilinitoka kwa raha, niliamka macho malegevu nimelegea tukaoga uko bafuni dah!!!! tukaoga tukavaaa tukatoka nje tuliwaaga wahudumu tukaita pikipiki yeye akapanda kuelekea stend arudi zake Pwani Mimi nikapanda kuelekea chuon.

Nilifika chuo ninafuraha yani kama zote nililala nilikuja kuamka saa 1 jioni nikamwandikia meseji

“NAKUPENDA”

Akapiga simu tukaongea sana akaniambia nikifika nyumbani nitakupigia tena ukawa mwanzo wa mahusiano yetu.

Nilikaa mwezi mzima chuo nikafanya mtihani tukawa tunafunga chuo kwajili ya kwenda field, niliambiwa na mama nichague hapo hapo morogoro.

Kweli nikachagua morogoro sasa tulipanga na Mudy niende kwake sasa namna ya kwenda ndo ilikua mtihani nyumbani nitaagaje kwa mama nikamshikirikisha rafki yangu Halima akaniambia

“Mwambie mama likizo hii unaenda Dar na umwambie twende kwetu kisha tuachane njiani ili uende kwa Mudy”

Nikaongea na Mudy akakubali Plan yangu akatuma nauli, bahati nzuri mama alikuja Moro mjini kikazi akapitia chuo nikamwambia mama kuhusu kwenda Dar kwa rafiki yangu akaguna akaniambia

“Mwanangu Dar nakufahamu sana kuliko unavyozani” Nilishia kujuta moyoni tu….

(huwa nawazaga sana laiti ningemsikiliza mama yasingenikuta haya mimi)

Kweli nikamuahidi mama kuwa nitarudi……..ITAENDELEA.

Like nyingi Napata motisha ni wangapi wanaipenda na kuifuatilia hii simulizi.

Comment uwezavyo Kama unaihitaji yote au episode ijayo nicheki sms 0655 969 973.

Vipande vitatu sh 500 tu.

NUKUU “Majuto ni mkukuu, neno ningeujua huja mwisho wa safari, huja wakati mambo yashakua magumu. Mabinti wa leo wasikilizeni wazazi wenu pindi wanapowakataza jambo, acheni kujifanya mnajua zaid kuliko wao. Punguzeni hivi vichaa vya mahuasiano na ndoa. Mbarikiwe wote mnaofuatilia simulizi hii”

Mje Twitter @middotz_
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU SEHEMU YA SITA
Man Middo 0655 969 973

ILIPOISHIA……………“Mwambie mama likizo hii unaenda Dar na umwambie twende kwetu kisha tuachane njiani ili uende kwa Mudy”

Nikaongea na Mudy akakubali Plan yangu akatuma nauli, bahati nzur mama alikuja Moro mjini kikazi akapitia chuo nikamwambia mama kuhusu kwenda dar kwa rafiki yangu akaguna akaniambia

“Mwanangu Dar nakufahamu sana kuliko unavyozani”

Nilishia kujuta moyoni tu…. (huwa nawazaga sana laiti ningemsikiliza mama yasingenikuta haya mimi) kweli nikamuahidi mama kuwa nitarudi…………SONGANAYO

Nikamuahidi mama nitarudi salama asiwaze, mama hakua na namna alikubali then akatuaga akaondoka, kilichobaki kujianda na safari kesho yake.

Siku ya safari ilifika, nakumbuka tulipanda basi kipindi hicho BM MPYAAAA! Tukaanza safari ya kuelekea Dar, tulifika sehemu inaitwa bwawani kulikua na ajali, gari ikasimama tulikaaa pale mpaka saa 11 jioni ndo tukatoka tukaendelea na safar. Muda huo n njia nzima nilikua nawaza nikijiambia

“Mtu nimemjua Moro leo naenda hadi kwake harafu namdanganya hadi mama je nikipatwa na tatizo itakuaje?” Niliwaza bila kupata jibu.

Muda wote najiwazia lakin pia nilikua nawasiliana na Mudy, njia nzima ananielekeza alifurahi sana mimi kwenda kwake maana nilikuaga nampa kalenda sana.

Basi nilifika salama stendi nikamkuta yupo pembeni na gari alikua yupo na rafiki yake nikamkimbilia nikamhug na kumkiss mdomoni.

Kwa kweli aliona aibu mbele ya rafiki yake, kwa aibu aibu zake tukaingia kwenye gari kuelekea kwake, Rafki yake alishuka njiani.

Tulipofika akaniuliza kihisia kuwa nyumba yake ni ipi, kwa kweli sikuweza kupatia, akaniambia si nilikuonyesha kwenye simu, (sasa nikawa nawaza kwa muonekano wake hakufanania kabisa kumiliki hata baiskeli sio kuwa namponda au kumsemea vibaya lakin kiukweli alikua rafu sana yani).

Baada ya hapo akanionyesha nyumba yake tukaingia ndani Dah!! Asee nje nje kulikua na nyasi nyingi mno halafu ilikua kipindi cha mvua, kulikuwa na wapangaji pia.

Kwa kuangalia jinsi palivyo ilionyesha hakua msimamizi katika nyumba yake na sio mtu wakufuatilia maana nyasi ndefu mpaka mlangoni! Tukaingia zetu ndani na bahati nzuri tulishakula njiani kwahiyo ilikua kuoga na kulala.

Baada ya hapo tukaenda bafuni tukaoga pamoja tukaenda kulala!! Kwa kweli maandalizi ya chakula cha usiku wa manani yalikua mazuri ajabu yaan balaa maana sikutaka kujinyima na kuzingatia alikua fundi mzuri wa mapishi na utamu wa chakula chake sio wa nchi hii.

Kwakua nilificha kitumbua sehemu salama nikamwambia tunywe juice kwanza kwa mrija, asee juice haikua ya baridi sana na ukizingatia pale kwake kuna kiyoyozi kwa kweli kiliongeza hamu ya kula.

Ghafla bin vuu akatoa muhogo wa kuchoma sijui aliutoa wapi haraka vile! Mara akaacha juice akavamia kitumbua changu nilikua naona raha ya ajabu huku mziki taratibu nakumbuka alikua “Celine Dion na wimbo wake Because you loved me” kuna wakati nilihisi kukojoa ile ya kutoenda chooni mpaka ile ya mfululizo kuna kipindi nilihisi kama kaniko*.. nikamuliza

“Vipi mbona kama sielewi?” akasema

“Hapana utamu tu wa muhogo” ...... ITAENDELEA.

NUKUU "Kila utamu na Raha unayohisi huwa Ina madhara yake, mara nyingi tunapokuwa wakati wa chanya+ huwa tunasahahu kuhusu Hasi- kumbe hivi vitu vinaenda pamoja sana. Eliza yupo kwenye kipindi Cha furaha lakini ashatuambia angejua angemsikiliza mama yake kuhusu kwenda Dar, tusikilize wazazi wetu pale wanapotuasa kwenye jambo lolote"

NAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KUPOST SIKUA VIZURI KIAFYA, SASA TUPO PAMOJA. USIKOSE LEO SAA MBILI USIKU.
Instagram @middotz_
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU SEHEMU YA SABA (07)
Man Middo 0655 969 973

Kesho yake tukapanga anitoe kwenda mjini kuosha macho kidogo sehemu nzuri nzuri, nikafrahi sana na kweli alinitoa tukapitia kazin kwake kuna mtu alimwita akaongea nae akarudi kwenye gari akanambia

“Sorry nimeshindwa kukutoa tena ngoja nikurudishe nyumbani nikiwahi kurudi tutatoka maana kuna kazi flani hapa inabidi niende Kibamba kwanza”

Sikua na hiana nilikubali akanirudisha nyumbani akaondoka nikabaki sebleni nangalia TV, ukweli nyumba yake ilikua nzuri tena ya kifahar flan ivi japo haikua kubwa sana alijitahidi kiasi chake. Nilibaki hadi usiku wa saa 2 nikampigia kumuuliza kama bado yupo Kibamba akaniambia

“Kazi ngumu na mvua hii kurudi imekuwa ishu ila nitangaika mpaka nirudi mpenzi sikupenda iwe hivi nilipanga siku 3 hizi ziwe zako tu”

Kweli ilikua kipindi cha mvua, nilibaki pale hadi nikaletewa chakula alimtuma mtu akaleta nikala zangu nikaenda kulala. Sasa usiku ule nikawa naogopa peke yangu, sijui kitu gani kilinituma, kwanza jana yake kuna harufu flani ivi niliisikia harafu leo kuna harufu nyingine mpaka pia mafua yalinishika gafla.

Basi huko chumbani nikaanza kukagua kila kona nikavuta droo mmh! Nilikuta ile droo imejaa pesa nilishangaa imekuaje mtu aniache kwake hata hanijui vizur na pesa kiasi hiki au kaniwekea mtego aah! Nikaachana nazo mmh! Nikaona maji flani hivi meusi yatoka chini ya kitanda kwa kweli niliogopa sana.

Niliwaza ni kitu gani huku chini ya kitanda asee kuja kuinama nilishangaa sikuamini macho yangu huku namulika na tochi nilikuta nguo chafu zimeozaa inaonyesha zilikua zimelowekwa kwa muda mrefu sana maana zilikua zinatoa hadi funza, nilishangaa sana kuwa mwanaume na hela zake anakua mchafu hivi, kuna muda niliwaza labda ndo njia zake za kupatia pesa.

Nilimpigia simu muda huo huo nikamuuliza

“Nini hiki chini ya kitanda?”

alikaa kimya kama dakika mbili hivi kisha akaongea kwa aibu flani hivi

“Nisamehe mpenzi wangu hizo nguo ni za kufua”

“Kwanini usingeacha nifue?”

Kwa kweli mwanaume yule hakua na jibu kabisa zaid ya kujiumauma tu, niliachana nae na hapo nikaanza kukagua kila sehemu usiku ule ule kwa kweli nilikutana na mambo ya ajabu sana ambayo sikuamin kwa uwezo wake wa kipesa angekua vile nyumbani kwake.

Jikoni nilikuta nguo nyingine zimelowekwa na zimeoza alificha nisizione pia na kila sehemu haikueleweka kabisa, niliwaza kuwa kumbe wanawake wanaokuja hapa wanakuja tu kuchukua pesa na kuondoka na yeye mwenyewe alikua rafu sana yani kwa muonekano wake na vitu anavyomiliki ni tofauti kabisa.

Kwa kiasi flani iliniuma japo sikuwaza kuolewanae lakini niliwaza aina ya wanawake anaowapata ni wanamna gani ambao wanawaza pesa tu kutoka kwake hata usafi wanashindwa kufanya.

Siku iliyofuatia niliamka nikaanza kufanya usafi nyumba nzima na kwakua hakurudi usiku nilipanga iwe kazi yangu asubuhi kabla hafika.

Na kweli nilifanya hivyo, nilichukua nguo zote ammbazo zilikua kwenye kabati, kwa kweli zilikua nyingi mno maana nilianika kwenye kamba hadi zikajaa, mpaka chini kwenye majani, nilifua viatu vyote na baada ya hapo nikasafisha ndani Dah!! Lile vumbi utafikiri kulikua hakuishi watu.

Ilivyofika saa mbili asubuhi akarudi yeye na rafiki yake nikamuona anakaibu flani hivi, na yule rafiki yake alibaki akishangaa tu kwa jinsi nilivyofua nguo nyingi kwa muda ambao nimekuja.

Basi baadae aliniambia niingie ndani nikaingia zangu chumbani na yeye akaja rafiki yake akiwa sebeleni

“Mh!! Asante sana kwa usafi uliofanya na pia pole nilishindwa kabisa kufua mara nyingi nipo bize ndo kama uonavyo kulala ndani kwa kuhesabika na kazi zangu ngumu sana” Nikamuambia

“Usijali nalo pia ni jukumu langu”

Basi akaniambia nijiandae tutoke ngoja amsindikize rafiki yake then akirudi twende zetu kusafisha macho nikamjibu sawa nikaenda zangu kuoga nikamaliza nikawa na msubiri, hakucheewa sana akatokea nae akaenda kuoga akavaa tukaondoka.

Tulivyofika mtaa flani hivi alipand arafiki yake ambaye sio yule aliyemsindikiza muda flani akaniambia

“Huyu ni rafiki yangu saana naweza sema ni zaidi ya ndugu na ukimuona huyu ni kama umeniona mimi yaani umuheshimu kama unavyoniheshimu mimi”

Muda wote nilikua natikisa kichwa kumanisha kukubali alichikua anasema, Basi tukasalimiana pale alijitambulisha kwa jina la Godii.

Huku tunaendelea na safari tukanza kuingia sehemu za starehe na viburudisho hiyo ndo ilikua mara yangu ya kwanza kutembea Dar kwa kweli nilikua nashangaa tu wadada wanavyovaa nusu uchi..... ITAENDELEA.

Eliza anashangaa watu wa Dar, Je akimaliza kishangaa itakuaje? Usikose episode ijayo
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 8
Man Middo: 0655 969 973

wakawa ananiambia wewe si unajiona unavaa wazi kuna wanaovaa wazi zaid yako.

Tulifika sehemu sikumbuki jina tukaingia tukaagiza chakula mimi niliagiza chipsi samaki, sasa chakushangaza wenzangu waliletewa waichokiagiza ila mimi sijaetewa akaniuliza

“Mbona hujaletewa au hujaagiza?”

“Nimeagiza ila sielewe kwanini hawaleti”
akaniambia

“Agiza tena huenda hukusikika vizuri”

Basi nikawaza ngoja niagize chipsi nyama tu maana mwanzo niliagiza chipsi samaki ndo hawakuleta nikaagiza pale wakaleta chipsi nyama.

Sasa ile naanza kula tu kumbe ile oda ya kwanza pia walikua wanandaa ikaja wee!! nilishia kutoa macho tu, Mudy ndo nilimjua siku ile yupoje upande wa hasira alifoka mpaka nilijihisi kutetema

“Tamaa tu unagizaje vitu viwili mtu mmoja mara samaki mara nyama utamaliza vyote na tamaa zako aah!”

Bahati nzuri rafiki yake akamwambia wenye kosa ni wahudumu sio huyu ndo akakaa kimya ila kwangu chakula hakikushuka kwa kweli cha kushukuru tu akalipia vyote tukafungiwa samaki.

Niliwahi kwenda kwenye gari maana niliumia sana hasa alivyoniaibisha mbele za watu nikajua hata atanibembeleza angalau nitoe upweke yeye kimya kwake hakuna kitu kama hicho.

Tukaondoka kuelekea coco beach na ndio ikawa mwanzo wangu wakuiona bahari, tulifika sasa tukawa tunaangalia watu wanavyo jitupa kwenye maji.

Mimi sikuwahi kuona meli live nikaiona meli kubwaa nilifrahi sana nikawa napiga picha tu, siku hiyo ilikua sikukuu ya pasaka nikamuomba Shem Godii atupige picha Mimi na bae.

Mmh! Sasa mwenzangu kila nikionesha ushirikiano wa mapozi yeye aibu tu kazi yake kushangaa wanawake wenye makalio makubwa yaani nilibaki kumshangaa tu.

Basi tukainjoy pale coco baadae tukaondoka tukapitia suparmaket uchumi kipindi hicho inaitwa Game tukapitia na Mlimani city kwa kweli siku ile nilinunua kila nilichokitaka.

Kwakua tulisoma sana chuo kuhusu vinywaji nilinunua vinywaji baadhi vingi kidogo akawa ananikataza kununua vinywaji vyenye vilevi akidai wewe huviwezi nilikazania akawa hana namna, tukanunua piza bagar siku hiyo ndio nilivila kwa raha kwasababu nilivyokua chuoni tunajifunza sikufaidi vizuri.

Tukarudi hadi nyumbani na mizigo kibao Shem Godii alishuka njiani kwake, sisi tukafika nyumbani tukaoga tukaenda kulala na kesho yake mimi safari ya kurudi Moro.
********

Basi ikafika muda wa chakula cha usiku kwa watu wazima, chakula kisichohitaji karaha na bughdha wakati wa kukila.

Basi ikawa mwendo wa pilau na viungo kama vyote siku hiyo na ukizingatia kesho yake naondoka! Hehee! Pilau ilikua tamu balaa usiku huo.

Asubuhi ikafika! Kama kwaida ya asubuhi lazima mpate chai hasa kabla hujashuka kitandani basi kwa upande wetu chakuagiana tulichagua kahawa ya moto kidogo na ukizingatia kale kabaridi kaasubuhi kahawa ilikua tamu mnoo!

Baada ya kahawa nzuri akaniambia nichukue kiasi cha pesa ninachotaka kwenye droo nikachukua pesa ila nikachukua tu kama anavyonipa elfu 70 kwa wiki na elfu 30 dharula akanambia

“Ongeza za wiki ya mbili chukua na za mandalizi ya kuanzia field kutuma na choka harafu nabanwa, muda mwingine nachoka kweli kutuma tuma”

Nikafanya hivyo nikaondoka kama na laki 4 hivi na makolokolo yakuondokanayo niliyonunua suparmakert.

Baada ya hapo nikampigia simu rafiki yangu kujua kafikia wapi ili turudi kama tulivyopanga ili ionekane tulikua kwao Dar nilimpigia akasema yupo anajiandaa.

Basi sisi tukapanda gari hadi ubungo, kufika ubungo tulisubiri wee!! Halima hatokei hadi Mudy akachukia akanza kufoka

“Huyo mwenzio anafikiri mimi sina kazi au?”

Akawa mkali yani tayari nilishia kumsoma Mudy kwa muda mchache kuwa ni mkali sana moyoni nikajiambia bora nimekujua mapema usinioe tu. Badae akaamua tu anikatie tu tiketi niondoke akasema

“Huyo rafiki yako atakua ananauli maana asinge sumbua hivi mimi nawahi kazini”

Nikamuaga pale nikapanda bus nikanza kurudi Moro

(kama kunaendeka nijue kama hakuendeki njue wapii? Dar mpaka Moro)……. ITAENDELEA

Inaitwa ELIZA NA NDOA YANGU je huu ndio mwanzo wa hiyo Ndoa?

Usikose kitakachojiri hapo baadae.

NUKUU “Muda upo Huru lakini Hauna gharama (Huwezi ukaununua muda) Huwezi ukamiliki muda lakini unaweza ukautumia muda. Huwezi ukautunza muda, lakini unaweza ukautumia muda. PINDI UKIUPOTEZA MUDA, KAMWE HUWEZI UKAUREJESHA MUDA”

Rudia kusoma ukishasoma shusha like Yako,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom