gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 759
- 1,250
Bado sijapata Title maalum ya hii Simulizi twende nayo hivyo hivyo.
UTANGULIZI
Kuna jamii ya watu iliyozuka na kuleta sintofahamu miongoni mwa jamii nyinginezo, watu wanaozisaka pesa kwa namna yeyote ile hata ikibidi kumkufuru mwenyezi Mungu, amini nakwambia si kila ukionacho kwa macho kuwa kipo sahihi basi ukakitafsiri hivyo bila kukifanyia uchunguzi. Ungana nami katika mkasa huu wa kusisimua uweze kujifunza mengi, usisite kunitumia ujumbe mfupi kwa maoni na ushauri.
SEHEMU YA 01
Alfajiri na mapema vishindo vilisikika, ni kama vile kuna mtu aliyekuwa akikimbizwa kisha sauti ya kuomba msaada ilisikika. "Nisaidiee nisaidiee nakufaa!" Sauti ilikuwa kubwa na ilisambaa kwenye maeneo mengi ya kitongoji cha Iptus katika jiji la Greenville hakukuwa na mtu yeyote aliyethubutu kuufungua mlango wake kutoa msaada. Si kwamba walikuwa hawasikii la hasha, walijua fika jambo ambalo linampata mtu huyo anayepiga kelele kwa hivyo waliogopa kujitokeza kupambana na watu hao hatari.
Sauti ya kuomba msaada iliendelea kusikika na mwisho ikapotea na ukimya ukatawala. Damu nyingi zilitapakaa, tukio la kinyama la mauwaji ya kikatili lilikuwa limekwisha kutendeka. Kijana aliyeuwawa na kuchomolewa moyo wake alibaki akiwa amelala huku damu zikiwa zimesambaa, alikuwa amelala juu ya dimbwi la damu!
"Kijana huyu ameonyesha msimamo mkali kwa Mungu wake na kugoma kujiunga na kikundi chetu cha dini mpya na hivyo imempasa kuuwawa, na hili ni onyo kwa yeyote ambaye atakiuka agizo la kujiunga na dini mpya ya Wateule itampasa kuteketea kabisa." sauti ya mtu ilisikika kupitia kwenye kipaza sauti. Wafuasi wa dhebu hili la wateule (The chosen one) waliokuwa mstari wa mbele katika kusambaza dini hiyo mpya wakiongozwa na kiongozi wao Mchungaji Masambula walijizatiti kuisambaza dini hii mpya.
Askari walizungushia utepe kwenye eneo ambalo tukio hili lilitokea, picha zilipigwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hii iliongeza woga kwani watu wengi walikuwa wakiogopa kujitenga na dini hiyo mpya, vituo vya kujiunga na dini hiyo vilikuwa busy kupokewa waumini waliokuwa wamefurika kujiandikisha.
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, ni kwanini watu hawapendi kusoma maandiko, upotoshaji huu mpaka lini, siwezi kukubaliana na jambo hili lazima nitafanya kitu." Kijana Marcus alikuwa amekaa mgahawani akipata kahawa huku akisoma matangazo ya dini hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
Marcus alikuwa kijana mahiri na msomi alisomea theolojia na mambo ya sheria huko Roma Italia, hakupenda kuona yale mauwaji yaliyoshamiri katika kitongoji kile, watu waliokuwa na malengo binafsi wakifanya mambo ambayo kwake aliona kwamba hayampendezi Mwenyezi Mungu. Alitoka kuelekea kwenye maegesho ya magari akaingia kwenye gari yake ya kifahari aina ya Marcedez Benz na kutembea taratibu kuelekea kwenye makazi yake. Huko njiani hali ilikuwa inatisha alipishana na mizoga ya watu iliyokuwa wametapakaa kila kona ya mji ule. "Kwanini serikali imekaa kimya kanakwamba hawafahamu lolote linaloendelea juu ya mauwaji haya?" aliwaza moyoni mwake.
****
Mlipuko wa makanisa ya 'wateule' ulishangaza wengi siku hii ya Jumapili matawi mbalimbali ya makanisa yakiwa yamefurika waumini, watu wakisifu na kuabudu. Kwenye kanisa kuu lililokuwepo kwenye kitongoji cha Iptus mchungaji alikuwa amesimama mbele akihubiri.
"Sikilizeni enyi waumini, hakuna jiwe litakalo salimika juu ya jiwe hii ni amri kutoka kwangu ya kwamba kila mtu lazima ajiunge nasi atakayegoma kujiunga nasi huyo sio mwenzetu, naamuru kuanzia sasa watu hao waangamizwe popote mtakapo waona." Waumini walishangilia kwa nguvu, "ndioo hao wasiokuwa nasi ni lazima waangamizwe." Baada ya ibada mchungaji aliondoka huku akisindikizwa na walinzi wake.
Marcus aliingia kwenye viunga vya kanisa la Wateule akiwa na lengo la kuonana na mchungaji Masambula. Aliegesha gari yake na moja kwa moja akaelekea eneo la mapokezi, waumini wengi walikuwa wakitoka kuelekea majumbani mwao. Marcus, akiwa amevaa suti yake nyeusi na miwani nyeusi, alificha bastola yake ndogo iliyofanana na kalamu kwenye mfuko wa koti lake hakuna aliyeweza kumshtukia akafika mpaka pale mapokezi. "Naitwa Marcus Desmond ni mwana utume wa Jesuits kutoka kanisa la magharibi nimekuja kuonana na mchungaji Masambula." alijitambulisha.
"Mchungaji, kuna mgeni yupo hapa anahitaji kuonana na wewe," alisema dada wa mapokezi kupitia kwenye simu ya mezani. "Mwambie apite," ilisikika sauti kutoka upande wa pili. Marcus aliingia pale ndani, michoro ya kushangaza ilikuwa kwenye chumba kile msalaba uliogeuka juu chini ukiwa ndio alama kuu ya dini ile, kwa mbele kabisa kulikuwa na picha kubwa ya moyo uliotobolewa kwa kisu ukivuja damu. "Hizi ndizo alama kuu za dini hii, kwanini wanatumia alama hizi? Msalaba uliogeuka juu chini na moyo uliotobolewa na kuvuja damu?" alijaribu kuhusianisha michoro ile na matukio ya kinyama yaliyokuwa yakiendelea mitaani.
"Kila mtu aliyeuwawa akihusishwa na mauwaji yale basi alitobolewa kifuani na kuchomolewa moyo wake, na vipi kuhusu msalaba uliogeuka juu chini, hii haiwezi kuwa alama ya ukristo labda wapinga kristo...?" Aliwaza huku akiingia kwenye chumba kikubwa kilichokuwa ndani ya jengo hilo la kifahari lililokuwa ndio makao makuu ya kanisa la Wateule. Kila kona kulikuwa na nakshi za dhahabu, sanamu ya fuvu la kichwa ilikuwa mezani na mchungaji alikuwa ameketi kwenye kiti chake wakati Marcus akiingia.
Alifika wakapeana kupeana mikono na kisha kuketi kwenye kiti mbele ya mchungaji aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha kifahari chenye kuzunguka. Mara tu baada ya kusalimiana kwa ujasiri mkubwa Marcus anamweleza sababu zilizomfanya afike hapo. "Naitwa Marcus ni mwana theolojia na mwandishi wa habari nimesoma na kuhitimu huko Roma Italia nimekuja kukusanya habari juu ya uendeshaji wa kanisa hili na dini hii mpya, nashangazwa na namna yako ya kuhubiri injili, ni dini gani unayo isambaza kwa namna hii?" alihoji Marcus na kuendelea.
"Angalia ni watu wangapi ulio wauwa kwa kuwa tu wamegoma kufuata matakwa yako ya kidini, unadhani jambo unalolifanya lina baraka za kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu?" Mchungaji Masambula alionyesha uso wa kukasirika, hakupenda kabisa kukosolewa naye akajibu. "Sikiliza kijana nchi hii nimeiweka mikononi nakuhakikishia kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayenizuia kwasababu ninagawana nao maslahi kila inapoitwa leo, na kuhusu dini kusambazwa kwa upanga mbona hilo sio jambo jipya?"
"Waulize wakatoliki na vita ya msalaba, watu wangapi walikufa wakiutetea ukristo, waislamu nao vivyo hivyo walipigana jihad kuutangaza uislamu, dini yoyote lazima isambazwe kwa vita kwasababu haya ni maelekezo ya mwenyezi Mungu na kwa ninavyojua sio kila mtu atakayekubaliana na maelekezo haya wapo watakao kubaliana na pia wapo watakao pinga, watakao pinga ni lazima tuwateketeze hatuwezi kumuacha mchawi aishi imeandikwa kwenye biblia," alisisitiza mchungaji Masambula.
"Kwahiyo unataka kuniambia kwamba dini yenu ni ya kweli na ya haki kuliko vikundi vingine vyovyote vya kidini na kiimani?" alihoji Marcus.
"Kila mtu huona dini yake kuwa ndio yenye haki kwahiyo kwangu mimi ninaamini kwamba dini yetu ndio yenye haki na hivyo nitatumia mbinu zozote zile kuhakikisha kwamba dini hii inasambaa kwa kila raia wa nchi hii," alizidi kusisitiza mchungaji Masambula.
"Vipi kuhusu hizi alama zenu mnazo zitumia msalaba uliogeuka juu chini pamoja na moyo uliotobolewa na unaovuja damu?"
"Sitoweza kukujibu kwa sasa juu ya haya maswali yako yote labda unipe muda ndio nitaweza kukujibu maswali haya.
Kufumba na kufumbua, Marcus alichomoa bastola yake iliyokuwa kama kalamu ya kuandika ni bastola ndogo sana ambayo ilikuwa na kiwambo cha sailensa na kisha kumuelekezea mchungaji na hapo akamsihi asali sala zake za mwisho. "Haiwezekani haya mateso yote yawe yanatokea kwa ajili yako kwahiyo nitakupoteza kwa manufaa ya wengine!" Mchungaji alishangaa, alinyoosha mikono yake juu kuomba msamaha Marcus hakufanya makosa alimlenga moja kwamoja kifuani kwa risasi moja tu ilitosha kabisa kumfanya mchungaji Masambula kuanguka chini.
Haraka haraka alichomoa kisu alichokificha kwenye mfuko wa koti akamtoboa kifuani na kutoa moyo, akaufunga kwenye mfuko wa nailoni na kisha kuuweka kwenye kibegi chake cha mgongoni. Akatoka pale mapokezi bila hata kugundulika na kuingia kwenye gari yake kisha kuondoka kwa kasi na kutokomea. Kilikuwa ni kitendo cha haraka kilichotokea ndani ya nusu saa tu. Mchungaji aliyeonekana kuwa ni kinara wa mauwaji ya kidini leo hii yamemtokea yaleyale aliyokuwa akiyafanya kwa watu waliokataa kujiunga na dini yake.
ITAENDELEA...