Simulizi: Alitaka Kuniua

Apr 19, 2023
77
123
ALITAKA KUNIUA

Nilikuwa nimekaa chumbani hostel kipindi hicho nasoma chuo mwaka wa pili. Nikapigiwa simu na mama akiwa na furaha kubwa sanaaa. Akaniambia kama ninaweza kwenda nyumbani kwa wiki moja itafaa sana.

Aliniuliza “Je, unaweza kuomba likizo chuo ukapewa?” Nilishangaa kwanini mama ananiambia hivo. Shahuku yangu kubwa ikawa ni kutaka kujua kwanza sababu ya furaha yake na wakati huo huo nijue kwanini ananiambia niombe ruhusa.

Akaniambia mdogo wangu Anethi anaenda kuolewa na ameshalipiwa posa. Ilipidi nivute pumzi kwanza
halafu nimwambie “sawa mama nitakupigia” Akanisistiza nifanye kila namna nipate ruhusa kwani jambo hili ni la muhimu kwa kila mwana familia kuwepo.

Nilikata simu na kukaa chini kwa maumivu na uchungu kwani mdogo wangu huyo alikuwa amemaliza form four siku chache zilizopita na alikuwa akisubiria selection za advance kwani alikuwa amefaulu vizuri tu.
Na isitoshe nilikuwa nikimtia sana moyo asome kwa bidii huku nikimuahidi kuwa nitakuwa msaada sana kwake katika kutimiza ndoto za kuwa msomi mkubwa sana hapa nchini.

Hilo jambo kwa familia lilikuwa ni la kawaida Kabisaa kwani kwa wakati huo jamii zetu hasa za vijijini ilikuwa ni kawaida kumuachisha mtoto wa kike masomo na kumuozesha. Kwa hiyo nilielewa vizuri ni kwanini jambo hilo kwao lilikuwa ni la furaha bila kujali kuwa wanakatisha ndogo za mtoto wao.

Niliondoka chuo bila kuomba ruhusa kwani ni kawaida kutoka chuo na kwenda kufanya mambo yako hata
kwa mwezi muhimu ni kuwa assignment, quiz na test zikitolewa uweze kufanya na isitoshe utaratibu wa kuomba ruhusa chuoni nilikuwa siufahamu na hata ningeufahamu sikuwa na sababu ya msingi kabisa kuomba ruhusa.

Nilifika kijijini kwetu nikiwa na huzuni sanaa. Sikutamani hata kwenda lakini baba alikuwa ameshanitumia nauli
tayari hivyo sikuwa na sababu ya kuwakatalia nyumbani kutokwenda.

Nilifika mpaka nyumbani, walinipokea kwa furaha sanaaa na mama alikuwa akiruka kwa furaha, ngoma ya jadi ilichezwa na baadhi ya maneno ya shukrani kwa mizimu ya nyumbani yalitamkwa. Niliingia mpaka ndani na habari nyingine zikaendelea. Walakini sikuwa na furaha muda huo wote Kwa sababu ya mdogo wangu kukatishiwa ndoto zake.

Nilipata nafasi ya kuonana naye mdogo wangu. Yeye alionekana kuwa kawaida yaani ni amesha amua kukubaliana na hali na kuungana na furaha ya wazazi na ndugu zake.

Baba yangu mdogo mzee Stanley aliona ya kuwa sina furaha. Na jambo hilo aliliona pamoja na watu wengine. Na wakaelewa ni kwanini sina furaha. Walichoanza kuhisi ni kuwa naweza nikawa na mpango mbaya wa kuharibu mpango huo wa ndoa.

Hivyo panapo usiku kama majira ya saa nne hivi, kiliitishwa kikao cha familia ambapo walikuwepo na ndugu wengine waliokuja kwa ajili ya sherehe ya ndoa. Na katika kikao hicho mzee Stanely ndo akawa muongozaji wa hicho kikao.

Aliamua kuongea moja kwa moja lengo la kikao hicho ambalo lilikuwa ni kunieleza kuwa mpango wa ndoa ni
wa familia na kwa namna yoyote nisijaribu kuuingilia mpango huo wala kumshawishi mdogo wangu kwa chochote

Wanafamilia wote walisimama na kunitupia lawama huku waki isema elimu niliyokuwa nayo kuwa ndicho
chanzo cha ujuaji ninao uleta huku wakidai elimu yangu niiweke chini na sasa haya ni mambo ya familia.

Nilisimama na kumueleza baba mdogo pamoja na watu wote kuwa huo sio mpango wangu hata kidogo.
Na mimi ninaheshimu kabisa mawazo yao na pia isitoshe mdogo wangu ameshahafiki suala hilo hivyo mimi sina sababu yoyote ya kupinga uamuzi huo. Hivyo wasiwasi na mimi waondoe kabisaa na nitashirikiana nao kwa lolote

Niliamua kumuuliza baba mdogo kuwa muoaji ni nani. Sasa, jibu ambalo baba mdogo alinipa ndilo chanzo na sababu ya mimi kukuandalia story hii maana nilishikwa na hasira kali sana huku machozi yakinitoka. Sikuweza kabisaa kuidhibiti hasira yangu maana nilijikuta nimemuingiza baba mdogo katikati ya mikono yangu, yaani shingo yake katikati ya mikono yangu, huku nikimfokea kwa nguvu “ni kwa nini unataka kumuhozesha mdogo wangu kwa katili mkubwa kama yule?”

Hasira ilikuwa ni kubwa sana mpaka watu wote walinishika hadi kunifunga kamba. Nilifoka sana huku nikipiga makelele kama mwendawazimu wakati huo hali isiyokuwa ya kawaida ilikuwa ikiendelea kichwani mwangu na mwilini mwangu kwa sababu ya hasira ile niliyokuwa nayo.

Watu wote walishangaa na kustaajabu huku wakiulizana ni kitu gani kinaendelea. Wote walishangaa sana kuniona katika hali ile Kwa Sababu haikuwa kawaida yangu kuwa hivyo wala hawakuwahi kuniona nikiwa na hasira namna hiyo hata mara moja.

Na shahuku yao ikawa ni kutaka kujua ni kwanini nimekasirika hivyo. Kwani huyu joramu (muoaji) ana shida gani mpaka nikasirike hivyo baada ya kujua kuwa yeye ndiye muoaji?! Shahuku waliyokuwa nayo ni kama uliyo nayo wewe hapo msomaji.

Binadamu tuna moyo wa nyama lakini kuna wengine mioyo yao inaweza ikawa mioyo ya Visu kwa sababu ya
yale wanayoyatenda kwa wenzao.

Sehemu ya pili imebeba majibu ya fumbo hili, unaweza kupata break fupi halafu tuendelee sehemu ya pili.

ALITAKA KUNIUA 2
(The Last Episode)

Nilisoma shule ya msingi Mtandabui huko kijijini kwetu Malamla. Nilikuwa na uwezo sana darasani na wala sijisifii ila ki ukweli darasani hakukuwa na mtu wa kunifikia uwezo. niliongoza darasani kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba.

Nilikuwa na rafiki yangu darasani ambaye aliitwa Mussa. Mussa alikuwa akinipenda sana Kwa Sababu ya uwezo wangu darasani na mara nyingi tulikuwa tukisaidiana majibu kwenye mtihani (haya mambo nadhani mnayaelewa vizuri)

Alikuwa na uwezo mkubwa pia darasani na mara kadhaa alikuwa anapata nafasi ya pili, ya tatu na akifeli sana ni nafasi ya tano. Mussa alikuwa na kaka yake aliyeitwa Joramu. Joramu alikwa anatuzidi umri sana kwani yeye alikuwa amemaliza shule muda mrefu kidogo.

Sasa Mara nyingi joramu alikuwa akimsema na kumcheka mdogo wake Musa kuwa ni kwanini anazidiwa uwezo darasani na rafiki yake ambaye ni mimi. Angalau basi tuwe tunabadilishana nafasi na wala sio mimi kila siku.

Na mambo hayo yote Mussa alikuwa anakuja ananisimulia kila kitu kuhusu kaka yake anavyomsema na kumsimanga huko nyumbani. Bahati nzuri ni kuwa pamoja na yote hayo bado Mussa hakuwahi kunichukia wala kuonyesha kujaribu kushindana na mimi.

Jambo ambalo litanishangaza mpaka kesho ni sababu ya chuki ambayo Joramu alikuwa nayo kwangu maana sasa aliamua kuionyesha wazi wazi. Hakuwa akiniangalia vizuri kila tulipokuwa tunakutana.
Na hata nilipokuwa naenda kwao kumtembelea Mussa
alikuwa akiongea maneno fulani ya vijembe, huku akisema najifanya nina akili sana kuliko watoto
wenzangu ninao soma nao.

Nilikuwa siwezi kumjibu
Kwa Sababu ni mkubwa kuliko mimi na ni mtu mzima na zaidi sana ni kuwa nilikuwa nikimuogopa pia.

Alikuwa mkali sanaa kwangu pale ambapo tulikuwa tukifanya kosa lolote kwao. Si unajua watoto, kufanya
makosa ni jambo la kawaida Kwa Sababu fahamu zinakuwa hazijakomaa kidogo. Alionyesha kuchukia sana na kunisema sana hata kunipiga vibaya pale nilipokuwa nikikosea hapo nyumbani kwao Kuna wakati nilitamani kabisa nisiwe naenda kwao Mussa Kwa Sababu nafikiria nikikosea tu Joramu atanipiga sana. Lakini Musa alikuwa ananilaumu kwa nini ananitembelea sana kwetu halafu mm kwao siendi
hivo nililazimika kuwa naenda pia.

Mtu kuwa na chuki kwa mwingine
Ni jambo la kawaida. Na hata hayo yote
ningeyahesabu ni sawa kama si kitendo hiki ambacho naenda kukueleza, kwani kilidhihirisha chuki isiyokuwa ya kawaida. Na kiliusononesha moyo
wangu mpaka kesho kwani ninajiuliza siku zote kuwa ni kosa gani mimi nilimfanyia Joramu

Basi kuna siku hiyo nilikuwa kisimani kuchota maji. Sasa kwa bahati mbaya lile kopo la kuchotea maji liliniponyoka na kudondoka kisimani ndani. nikawa nahangaika kulitoa ili niendelee kuchota maji nikaogopa kwenda nyumbani kuwaambia. hivo nikaenda moja kwa moja kwa kina Musa ili aje anisaidie nilipofika nikamkuta joramu nilipomueleza akakubali.

niende naye (nilishangaa sana kaamua kutoa msaada kwangu) tulipofika kwenye kisima badala anisaidie
kutoa kopo kwani yeye ni mtu mzima alianza kunifokea na kuniita mjinga na kusema kuwa nina akili za darasani tu ila mambo mengine ni zero. Alinizaba kofi akanishika na kunitupa kwenye kisima cha maji na kuondoka. Alitaka nife Nilihangaika mnooo humo ndani. Nilikuja kupata fahamu najikuta niko nyumbani mwili mzito sanaa na unauma kila mahali.

Wakati huo wamenipaka dawa fulani za jadi. Ndipo waliponisimulia kuwa niliokotwa na mzee fulani hapo kijijini ambaye aliona mwili unaelea kwenye kisima. Kila mtu alijua nitakuwa nimekufa hivo walinichukua kama mwili maiti mpaka walipofika nyumbani bibi yangu ambaye anautaalamu fulani katika tiba za jadi aliposema bado niko hai wakaanza kunishughulikia mpaka fahamu ziliponirudia. Niliogopa kuwaelezea kilichotokea kwani nilimuogopa sana joramu kuwa anaweza akaniua tena.

Na baada ya siku kadhaa kama tatu hivi alihama pale kijijini akiogopa kuwa siku moja naweza kuongea siri
ile halafu ndugu wakaamua kulipiza kisasi. Na baada ya siku kadhaa tangu aondoke ndipo na
mimi nilipochukuliwa na Shangazi yangu aliyekuwa akiishi mjini. Nikaishi naye huko mpaka nilipofikia
kiwango hicho cha elimu (chuo kikuu). Na huko nyumbani nilikuwa nikienda wakati wa likizo tu. Hivyo sikuweza kuwasimulia habari ile

Story hii niliwasimulia pale nyumbani usiku huo baada ya kukaa sawa na wakaanza kuniuliza sababu ya kukasirika kiasi kile baada ya kusikia Joramu ndiye muoaji.

Kila mmoja alipigwa na butwaa wengi walilia sanaa hasa akina mama wenye mioyo myepesi. Ikabidi atafutwe joramu ili athibitshe yale maneno. Na kumbe aliposikia kuna jambo limetokea kule nyumbani kisa nimesikia yeye ndiye muoaji alitoroka usiku huo huo na kurudi alipokuwa akiishi mwanzo.

Akiogopa kuwa naweza kufanya maamuzi ya kulipa kisasi pamoja na ndugu zangu. Waliniomba msamaha pale nyumbani na mdogo wangu aliruhusiwa kuendelea na masomo na saivi anafanya kazi pale TBS
Na aliolewa na mwanaume aliyekuja Kumpenda mwenyewe na saivi wana mtoto mmoja wa kike.

Tuna mengi sana ya kujifunza hapa. Lakini muhimu ni Tupendane, tusameheane na kuheshimiana pia bila
kusahau kuthaminiana kwani huijui kesho ya mwenzako. Chuki haiwezi kuwa na mwisho mzuri hata mara moja. Na cho ndo alichokikosa Joramu

MWISHO

Napatikana Whatsap 0747671795
Twitter andika bayona_stories
Tiktok andika bayona_stories
Instagram andika bayona_stories
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom