Simuamini tena mke wangu!

doh, hii mada imenivutia sana ndugu zangu mi nachokiona wanaume tuendelee kukaza buti kutafuta pesa za kujikimu kwa familia nzima kuwepo na exces baada ya kukidhi maitaji yote kwani now days ada ya mtoto ni basic need
 
Kutuma hela kwao ni bora sana, isipokuwa kwa wapendanao lazima mshirikishane, hvyo kama analeta jeur cmama kama mwanaume kabla hajafika mbal, kata huo mtoko wa fedha na aanze kukushirikhisha mara mnja, kwan ww hujui mapato na matumiz yke kwa mwez huo ndo msing wa kuanzia

Ahsante kwa kujua kutuma hela kwao mke si tatizo.. wengine hiyo hakuna, wanakaba mpk penalti, halafu hela ni ya mwnamke sasa,
Ila hapo mwanamme kusimamia na kujua mapato na matumizi ya hela ya mwanamke huu ni UPARE sasa!
Hela hiyohiyo inasaidia kwao, hapo hapo na wewe unai bajetia, hapana Wise boy! Tafuta yako, shukuru umepata mwanamke asiye tegemezi anajimudu mwenyewe na hata familia yake bila kuingiza mkono mfukoni kwako!
Mwanamme ukishindwa hapo sasa wewe hufai! Akichangia ni vzr. Na sidhani kama mnapendana eti ana kipato aache hata kununua chumvi, si kweli!
 
mie mwanamke asiyetaka kumsaiidia mumewe na hali anao uwezo namuonaga kilaza wa kwanza, sasa mihela unaitafuta aile nani kama si uwapendao, mume na watoto wakiwemo? Kujazana ujinga tu, mwanamme majukumu, kama naye siku hiyo hana, na kweli hana, na mke unazo kwa nini usimpe? Labda kama kidumu.
Yaani unanuoma mume kapanda kitandani anasononeka hana hela ya ada, na mke anazo, na bado unakataa kumsaidia? Kwanza kufanikiwa kwa watoto sio sifa ya mume tu, ni sifa kwa familia nzima.

Hizi elimu bado hazijakomboa baadhi wanawake kabisa. Mtu anapata hela halafu hazitumii kwa wahusika wa kwanza? Tufyakwa!


yaaaani hapo ndo huwa nakupenda sasa straight on nails kama nyundo
 
doh, hii mada imenivutia sana ndugu zangu mi nachokiona wanaume tuendelee kukaza buti kutafuta pesa za kujikimu kwa familia nzima kuwepo na exces baada ya kukidhi maitaji yote kwani now days ada ya mtoto ni basic need

Thank you!:You are a real man! Yaaani hii ni kauli ya kiume!
 
Edison, samahani nimeenda nje ya mada. But hizi ndoa separate zinaletaga migongano isiyo na miguu! Unaweza ukakuta mnatofautiana tu kwasababu mnakaa mbalimbali!na mara nyingi mapenzi yanapungua, mnakuwa hamna mawasiliano mazuri, yeye kakujibu kwa ufupi, but hujui anachowaza, ukute anajiuliza huna hela zimeenda wapi? Mi natamani ufanye mchakato mkae pamoja.
 
Edson vaa viatu vya baba wa familia na hudumia familia yako. Pesa za kina mama zinawatosha kwa saloon na kucheza kibati si vinginevyo

Kweli kibati, ila kama unazidiwa na mimi naweza ni vzr kuwajibika pia. haina maana wewe umekosa kabisa alaf Mimi ninazo nikatae kutoa hayo si mapenzi bwana labda ni bizness partnership!
 
Last edited by a moderator:
Mimi na wife tumebahatika kupata watoto 2 wa kiume! Mm nafanya kazi dsm yy anafanyia mara. kijana wetu yupo grade 1 kwenye hizi academy! Takriban wiki kadhaa nilienda kumsabahi! Nije kwenye pt niligundua amekuwa akiwatumia ndg zake pesa nyingi paspo kunijulisha nahc kuna business wanafanya yy na dadake! Niligundua baada ya kumwambia kwamba mm kulingana na ujio wangu siko fresh kiuchumi hivo jitahidi ada ya mtoto make ndo wanafungua mwezi wa tisa kwa kifupi alinipa majibu ya kunikatisha tamaa akadai hana hela na isitoshe kwenye ubini wa mtoto anaandikwa yy au mm? Km sitaki kumsomesha akae nyumbani! Nikamuuliza km waweza tumia ndg zako malaki ya pesa unashimdwa nn kumlipia mwanao? Akakanusha wakati mm nilicheki kwenye mpesa ametuma pesa two times tena last month! Tukazinguana sana mm nikapanda basi nikasepa kwa ufupi hana mpango wa kusaidiana na mm ktk kusukuma gurudumu! Nimfanyaje mke wa namna hii?

fanya uchunguzi wa kina na muweke wazi kaka yangu wanawake wengine huwa wachoyo sana ndani ya familia zao bt huwa wana tapeliwa sana na hao watu wa nje ,swala kama hilo pia nimewahi shuhudia kwa majirani zangu bt kwhawa mume alikuwa anachukua mali za mke wake na kwenda kustarehee na vimwana so nahic naye pia ana waza hivyo kwa kuwa we uko mbali
 
Haya ndiyo matatizo ya wanaume wa cku hizi wanaoa wanawake wenye kazi ili kupunguziwa majukumu yao! Aaaagh! Kwani kutuma pesa home ni tatizo? Labda kama hajakushriksha! Je,mlikubalianaje kuhusu matumizi yenu ya pesa?au umemkurupusha tu?afterall mwanaume ndiye mwenye jukumu la kutunza familia zakwangu nitatoa nikiamua tena penye ulazima eboo! usilalamike kakope! ndo uanaume huo!

Hahahahahaaaaaa utamjua tuu! Mchuungu akakope khaaa si akope kwa mkewe bac?,
 
Hahahahahaaaaa vinalika ila ujue namna ya kuvila... sio unakuja na mihasira huko, leta mshahara wako, mbona unafichaficha, ukiambiwa school fees unajibu huku uko mlangoni c ulipe wewe kila siku mm! khaa utavila wp! Vitajenga nyumba za watoto!
Ukibembeleza ukajua kumtreat mwanamke hela unaila wala haina kokoro iyo! Mbona wanaume weengi hapa town wanaishi kwa kutegemea wake zao? Ni maelewano na mapenzi!

Unaanza kupendeka mamy!!!!!!
 
Haya ndiyo matatizo ya wanaume wa cku hizi wanaoa wanawake wenye kazi ili kupunguziwa majukumu yao! Aaaagh! Kwani kutuma pesa home ni tatizo? Labda kama hajakushriksha! Je,mlikubalianaje kuhusu matumizi yenu ya pesa?au umemkurupusha tu?afterall mwanaume ndiye mwenye jukumu la kutunza familia zakwangu nitatoa nikiamua tena penye ulazima eboo! usilalamike kakope! ndo uanaume huo!

Lakini mimi nijuavyo, mwanaume anapaswa kuwajibika kwa kila namna. Ukipata msaada kutokwa kwa mwanamke hiyo ni bahati yako.
 
Nawashukuru kwa ushauri mzuri! Nimemhangaikia sana huyu bbie na kaanza kazi mwaka huu hana muda mrefu i thought akianz kaz pengine ningepata ahuen lkn sion kabisa mwanzon alianza vizuri akawa yupo wazi kwa vile ndo alikuwa hajastabilize nikaona ngoja nivae ubaba hizi siku ambazo nimekaa naye nimebaini mambo yake yako private sana anyway almost huwa namwambia kila mpango wangu ninaotaka kuufanya lkn yy wapi hata nikituma 20 elfu kwa bibi ntamwambia da nilienda kuangalia jinsi ya kumfanyia uhamisho na nikawa nimeingia gharama kwa jinsi alivyoniboa nimeamua nisitishe hilo zoezi nijaendelee na maisha yangu! Khnachoniuma nimepotez dili zangu nyingi na nimeacha kazi kibao zinanisubiri then naishia upuuzi very disappointing!

This is serious now! Tafuta ushauri kwa wakubwa wenu. Usikate tamaa hivyo! Usipojali hujui ndoa itavunjika? Huoni kama unawapa watoto wenu wawili adhabu? Mchukue mkeo, then waiteni wakubwa watawashauri. Na uhakika mambo yatakuwa sawa!
 
Kwanza mkishaoana biblia kwa sisi wakristo inasema mtakuwa mwili mmoja, sasa huu mwili wenu umegawanyika nusu mara na nusu dsm,, ni lazima uone mapicha picha kama hayo maana hakuna tena umoja wa kimwili kati yenu.
Pili wewe umesema hauko vyema kiuchumi,ni wazi pia kwamba humshirikishi mkeo matumizi yako ya fedha ndio maana hata haoni haja ya kushirikiana nawe ktk kumsomesha mtoto.
Cha msingi fanya bidii kupanga maisha tena muishi pamoja ndipo mtakapoweka mipango yenu ya maisha sawa na kuwa na mawazo mamoja. La sivyo mwisho wa siku ndoa nayo inaelekea pabaya.
 
Ujinga huu ndio unasababisha watu wengi wakishaoa wanawaachisha wake zao kazi! maana mwaka mzima yuko kazini lakini hakuna anachosaidia hapo nyumbani. si bora ashinde nyumbani tu! mkuu Edison hebu jipe muda kidogo utafakari kisha fanya maamuzi magumu, mrudishe mama nyumbani alee familia. hizo kazi zake hazisaidii familia yenu.

Kama wewe baresa muachishe kazi! mume wa kwanza kazi baba! hivi hamjui ee? Ukibadilika ukaanza ile hulka yenu, nitakuwa mgeni wa nani? Ni bora nitoe mshahara wangu wote nikupe lakini kazi yng nisiiache lol!
 
doh, hii mada imenivutia sana ndugu zangu mi nachokiona wanaume tuendelee kukaza buti kutafuta pesa za kujikimu kwa familia nzima kuwepo na exces baada ya kukidhi maitaji yote kwani now days ada ya mtoto ni basic need

Lakini mkuu rizq hutoka kwake muumba wanasema jitihada haishindi qudra kuna kipindi unapiga mishe ndoo inaishia robo tatu tu kujaa hapo inabidi boosting method ihusike!!!!!

Generaly jukumu la kutunza familia linabaki kiwa la baba lakini nini umihimu wa kuwa na mtu.ndani as partner wa maisha kuzaaaa????? Au papuchi ya kulala nayo????

Haina haja ya ku entertain mtu stingy kama huyu lakini je na wewe mkuu Edson uko transparent kiasi gani kwa mkeo,huwezi jiweka wazi kwa kila kitu ila inabidi ajue basics mkeo!!!

Wakati anakujibu huo ujinga wa surname why didnt you slap her,????!!!!!!Usiache makofi yote kwenye bag next time huwezi jua sa ngapi utahitaji japo moja!!!!! Yaani huyo kwa style hiyo god forbid anaweza kukujibu lolote kuna wakati ukikutana na mtu juha wewe inabidi uwe chizi maana huwa wanapima upepo smtimes!!!!

Hakuna formula katika migogoro ya ndoa so tulia muombe muumba piga kazi kuongeza kipato. Somesha wanao ila anatakiwa ajue wewe ni mume na ajue mipaka yake!!!
 
wanaume wa siku hizi sijui mpoje!!kulia lia tu kila siku..fanya majukumu yako ya baba na kichwa cha familia..kuna ulazima gani wa mke kulipia ada ya mtoto wakati wewe upo?pengine amekugomea kwasababu kuna vitu haupo sawa..wanaume wa siku hizi mwanamke akishaonesha kuwa anaweza kuchangia kwenye familia basi hiyo ndo inakua sheria kuwa lazima wafanye nusu kwa nusu kila kitu..baada ya hapo heshima yako ndani ya nyumba itatoka wapi??sikatai kusaidiana majukumu ila isiwe ndo lazima..
 
Kama mwanamke ana akili timamu, lazima pesa yake ataiweka kwenye kapu la familia. Dhana ya uwajibikaji na kuwa raia mwenye manufaa kwa jamii yako.
Jamii yako ya kwanza kwa mwanamke mwenye mume na watoto ni familia yake.

Utakuwaje wa manufaa kwa jamii? Kusaidia watoto yatima wakati wanao na wana shida hadi makalioni? Stupidity.

Labda nikuulize, ukipata mume ana pesa kama baresa na wewe una kazi, pesa zako utafanyia nini?

! Siyo lazima pesa za mwanamke ziwekwe kwenye kapu la familiaaa! Labda kama kuna MAKUBALIANO hayo! Otherwise kama ni mwanamke mwenye BUSARA na HEKIMA atamsaidia mumewe kwa hili na lile! Otherwise otherwise otherwise pesa zangu ni zangu na zake ni zetu.kuna baadhi ya wanaume ukiwaendekeza kwa hilo hata kyupi hununui! Mweh!
 
Mi sioni maana ya watu kumshauri jamaa akomaee kutunza familia............sasa kama huyo mke anaonekana hataki kuwa familia, au hii familia wanayozungumzia inajumuhisha watoto na baba.Sijui lakini endelea kuwasikiliza wajuzi wa ndoa...
 
Back
Top Bottom