Simbachawene: Uhamisho kwa watumishi wenye ndoa ruksa

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,970
2,184
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akijibu hoja za wabunge, hasa la uhamisho wa watumishi wakiwemo wanandoa wanaotenganishwa,

Amekemea tabia ya Maofisa watumishi kuzuia wenye ndoa kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwa lengo la kuwafuata wenzao.

Alisema kuwazuia ni kuwanyima haki ya msingi, na kuwaagiza wabunge katika maeneo yao wasaidia kusimamia haki za watumishi.

Lazima sheria za utumishi zizingatiwe, walimu hawa au watumishi wanayo haki ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini pia kuishi na wenza wao, lakini utadhani mtumishi anapoomba ni kama anasaidiwa, hapana ni haki yake ya msingi, waheshimiwa tusimamie haki za watumishi,”
 
kasema lini hiyo? itakuwa vyem sana maana siri ya mtungi aijuaye kata kwa kweli. Lakini pia angesema je kwa wale walioomba na maombi yapo hukofisini kwake nini kinaendelea?
 
Ni mwendo wa kurushiana mpira tu, ukienda tamisemi unaambiwa hatujaruhusiwa, tz bana dah
 
Back
Top Bottom