Simba Yashindiliwa 4-1 na Toto Africans

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054


Simba yamong'onyolewa Mwanza

@Yashindiliwa 4-1 na Toto Africans

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Simba jana iliwalaza mapema mamia ya mashabiki wake baada ya kukubali kipigo kitakatifu cha mabao 4-1 kutoka kwa Toto Africans katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mjini Mwanza.

Katika mchezo huo, askari wa kutuliza ghasia waliingilia kati kuwaokoa wachezaji na viongozi waliokaa kwenye benchi la ufundi baada ya mashabiki waliojawa na hasira kuvurumisha mvua ya mawe baada ya timu hiyo kuchapwa bao la tatu.

Simba inatarajiwa kuvaana na wapinzani wao wakubwa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Toto Africans ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata ilianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya nane ya mchezo lililofungwa kwa kichwa na mchezaji, Juma Seif. Seif aliyekuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Simba aliipatia timu yake bao la pili.

Uzembe wa mabeki wa Simba uliigharimu timu hiyo baada ya kuiruhusu Toto kupata bao la tatu lililofungwa dakika 44 na Oscar Joshua.

Saidi Dilunga alihitimisha kipigo cha mabao kutoka kwa vijana hao wa Msimbani baada ya kufunga bao la nne dakika 82.

Simba ilipata bao la kufutia machozi dakika mbili kabla ya mpira (Tusi)(Tusi)(Tusi)(Tusi)lizika kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na mshambuliaji kutoka Nijeria, Orji Obinna.

Baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba Kasmir Bezisnki alisema safu ya ulinzi ya timu hiyo ilicheza chini ya kiwango kwa kuruhusu mabao ya kizembe.

Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu ya Kagera Sugar iliichapa Azam United mabao 2-1.

Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika



 
Huu ni mwaka wa Shetani au Itazinduka? Tusubili labda itaziduka kama ilivyozinduka taifa stars mechi mbili za mwishoni
 
Hii migogoro itaziua klabu zetu,kama kiongozi hatoi rushwa kwa makomandoo wanamharibia.Soka la Tanzania halitaendelea mpaka klabu ziwe na wenyewe sio wanachama.
 
Timu ni mbovu na kocha ni dhaifu period, hakuna cha mgogoro wala nini? kwa nini Dalali anang'ang'ania madaraka? apishe na wengine waongoze. PM uko wapi? au mko kwa KAPUYA mnatafakari kipigo?
 
Dalali ameshajiuzulu kwa mara ingine? au kocha keshatimuliwa? sinema ya simba tamu sana hii.
 
Huyo dalali si member humu katika jf pamoja na jamaa wengine wa friendofsimba ? Kwanini asiwe banned kwa muda mpaka simba itakapoanza kushinda ?
 
Huyo dalali si member humu katika jf pamoja na jamaa wengine wa friendofsimba ? Kwanini asiwe banned kwa muda mpaka simba itakapoanza kushinda ?

he he he eeeee, halo ya simba yaani sinema ndio inaanza kama hivi....
 
Mi nadhani Dalali asijiudhuru ili aje ajiudhuru siku wakipigwa na mabingwa watetezi Yanga ya Afrika jumamosi.
Hapo dozi itakuwa imetosha na hapo anaweza kujiudhuru vizuri bila mikwala.
Si mnakumbuka alisema alipojiudhuru mara ya kwanza alikuwa ameweka mti ndani ya kijito kujua urefu?
Sasa nadhani ameshajua urefu ni bora ajiudhuru vizuri.
 
naona safari hii hatachinjwa kuku klabuni bali mbuzi.
hayo ndio matokeo ya kutibu dalili badala ya ugonjwa.
sijui sasa atafukuzwa nani.
inasikitisha.
 
Yanga mnajipa moyo tu, USIONE SIMBA KANYESHEWA MVUA UKADHANIA NYANI!

Simba yamtimua Mzungu
2008-10-20 11:13:15
By Badru Kimwaga

Simba imeamua kuachana na kocha wake, Mbulgaria, Krasimir Bezinsk kufuatia timu hiyo kusuasua kwenye Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara.

Habari za kuaminika zilizopatikana jana zinaeleza kuwa viongozi wa klabu hiyo walikutana jana na wanachama wa kundi la Friends of Simba na kuazimia kumwomba Bezinsk `aachie ngazi` na kurejea kwao.

Maamuzi mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho kilichofanyika, jijini, Dar es Salaam ilikuwa ni kuwaomba Syllersaid Mziray na Abdallah Kibadeni kuinoa timu hiyo.
Kikao hicho kilifikia maamuzi hayo kutokana na Simba kufanya vibaya katika siku za karibuni katika ligi, ambapo iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 13.

SOURCE: NIPASHE
 
We ngoja wafungwa na YANGA wiki ijayo ,lazima bakora itatembea
 
friends of simba haisambaratiki sisi tupo na tutaendelea kuwepo jamani kama kuwa wapenzi wanataka kutuunga mkono muwe munakuja breakpoint karibu na kile kibanda cha simu utaona nyekundu wale wote ni friends of simba na kila jumapili asb tupo pale
 
Hatuna raha wapenzi wa simba na jana nimesikia kiongozi mmoja akisema tumevamiwa na mafisadi daah hii sijui imekaa vipi au ndiyo tumechanganyikiwa....
 
Back
Top Bottom