Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,287
- 9,923
Kuelekea Mchezo wa Derby ya Kariakoo inayotegemewa kuchezwa jumapili Movembe 5, 2023
Hebu tuangalie Staili ya kucheza ya makocha hawa Miguel Gamondi wa Young Africans na Roberhno wa Simba
Tukianza na Kocha Gamondi Staili yake ya kucheza inamvutia shabiki yeyote ambaye anataka kutazama soka safi, amekuwa akiitengeneza timu yake kucheza mchezo wa kuvutia kwenye kila mechi, pasi nyingi, kosa kosa nyingi na zaidi mpira wa burudani, Hii ni staili bora ambayo mashabiki wanaipenda na amekuwa na uwezo wa kubadilika kwenye kila mchezo kwenye eneo la ushambuliaji, kiungo na hata mabeki kutokana na kikosi chake kuwa na watu wengi.
Siyo jambo la ajabu kucheza bila mshambuliaji kwenye mechi zake, siyo ajabu kumuona Mzize akianza na siyo ajabu kumuona akiwatumia mabeki watatu badala ya wanne kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Azam.
Kwa upande wa Kocha wa Simba Robertinho, amekuwa tofauti na Gamondi msimu huu timu yake haijacheza mechi hata moja ikivutia, lakini ni timu ambayo ni ngumu kupoteza mchezo kwenye dakika tisini pamoja na kwamba imekuwa ikiruhusu mabao mengi kwenye timu yake.
Robertinho amekuwa akibadili kikosi chake kila kila kinachopata bao au kinaporuhusu bao kwenye mchezo wowote, ni kocha ambaye analinda alichonacho, huku Gamondi akiendelea kutafuta kitu kipya hata baada ya kupata, akifunga bao moja anatafuta la pili, Robertinho akifunga moja analilinda hilohilo.