Simba SC yapokwa pointi 3 dhidi ya Kagera Sukari

Kweli mpira wa Bongo kizungumkuti. Yaani suala la kujua kama mchezaji alipewa kadi au la linakuwa gumu kiasi hiki! Basi na hiyo kamati iliyokuwa imefanya maamuzi ya awali ivunjwe kabisa na kuundwa upya.
Badala ya kulilia point za mezani, dawa ni kushinda ndani ya dakika 90 ili kupata point zisizo na magumashi.
 
Maamuzi hayo yametangazwa leo na Katibu mkuu wa TFF Selestin Mwesigwa katika ukumbi wa habari wa TFF.

Sababu za kufutwa pointi hizo ni
kucheleshwa kwa malalamiko ya Simba Sc dhidi ya Kagera Sugar.

Simba SC kushindwa kulipia ada ya kukata rufaa kwa maamuzi ya mechi hiyo
na kukosekana kwa uhalali wa kamati ya saa 72 kwa kuwahusisha wajumbe waalikwa ambao hawakutakiwa kuwepo kwenye kamati hiyo.

Sasa Simba ipo kileleni mwa VPL ikiwa na Pointi 59, Yanga wakiwa wapili na Pointi 56 huku wakiwa wamezidiwa michezo miwili na Simba.
by isack kalindi
 
KISICHO riziki hakiliki! ndiyo kauli pekee ambayo unaweza kutumia kufuatia timu ya Simba kupokwa pointi tatu ilizopewa baada kupeleka malalamiko kuhusu beki Mohamed Fakih wa Kagera Sugar kucheza mchezo dhidi yao akiwa na kadi tatu za njano mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba Aprili 2.

Maamuzi hayo yametolewa na Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kufuatia Kagera Sugar kuomba mrejeo wa kesi (Review) kutokana na Kamati ya masaa 72 kuipoka pointi tatu na kuipa Simba.

Akitoa majibu ya Kamati hiyo Katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa alisema kamati hiyo imebatilisha maamuzi ya kamati ya masaa 72 yaliyoipa Simba pointi tatu kutokana na mambo matatu yaliyojitokeza hivyo matokeo ya mchezo huo yamebaki kama yalivyokuwa.

zaza.jpg

Celestine Mwesigwa kulia akiingia kikaoni katika hoteli ya Protea
Mwesigwa alisema “Jambo la kwanza malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa kwa wakati kwa mujibu wa kanuni ya 20(1) inayotaka malalamiko yoyote kuwasilishwa bodi ya ligi ndani ya masaa 72.

“Jambo la pili malalamiko hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni ya 20 (4) ambapo inasema malalamiko yoyote hayatasikilizwa kama hayatakuwa yamelipiwa ada kwa wakati”.

“Jambo la mwisho kikao cha kamati ya masaa 72 hakikuwa na uhalali kutokana na kuwahusisha watu ambao walikuwa hawahusiki,” alimaliza Mwesigwa.

Mwesigwa alisema Kamati imemuagiza katibu mkuu wa TFF kuwapeleka baadhi ya viongozi wa bodi ya ligi mbele ya kamati hiyo kutokana na kupindisha ukweli juu ya sakata hilo.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba Simba ililala kwa mabao 2-1 ambapo sasa itabakiwa na pointi 59 ikiwa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Yanga.


SOURCE: E-FM 93.7 Dar es Salaam
 
Kumbe "Sheria" ilivunjwa ili "Sheria" nyingine ifanyiwe kazi! Halafu watu wanalalamika eti acha sheria ifanye kazi.
 
Kwa hiyo kumbe pamoja Na kagera kujua mchezaji ana kadi 3 bado kagera gains kosa

Kagera Sugar wanaweza kuwa na kosa lakini je sheria ilizingatiwa kwa mlalamikaji alifuata sheria kuwasilisha rufaa yake?

Kama wangewasilisha kwenye muda ilo suala la kadi ya njano ndipo lingeanza kufanyiwa kazi.
 
Kagera Sugar wanaweza kuwa na kosa lakini je sheria ilizingatiwa kwa mlalamikaji alifuata sheria kuwasilisha rufaa yake?

Kama wangewasilisha kwenye muda ilo suala la kadi ya njano ndipo lingeanza kufanyiwa kazi.
Source ya taarifa yako ni wapi mkuu?
 
Back
Top Bottom