Kumekucha: kamati ya waamuzi (ZFF) yasema Simba ilipendelewa

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,774
24,209
Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), imesema kuwa Mwamuzi Nasri Salum hakustahili kuipa Simba kona iliyoifanya ipate bao la kusawazisha, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati ikicheza na Singida Fountain Gate jana kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Waziri Shekha amesema uamuzi wa kuipa Simba kona katika dakika za nyongeza, haukuwa sahihi na kwa mwamuzi huyo alifanya makosa, japo kamati hiyo haiwezi kumpa adhabu.

"Nilikwambia kwamba tutachunguza na tumekutana leo, tumebaini kwamba kulikuwa na makosa ya mwamuzi. Haikupaswa kuwa kona. Hakuna sehemu ambayo mpira ulichezwa na mchezaji wa Singida na kipa akaudakia nje, hivyo haikuwa sahihi kuwa kona,” amesema na kuongeza;

“Ni makosa ya kibinadamu na ndio kosa pekee tumeliona baada ya kupitia ripoti na marudio ila sehemu zingine zote alikuwaa sahihi. Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”
 
Nafsi imewasuta
1704982251294.jpg
 
Si wanajificha kwny mgongo wa Simbaa wanajua wanajiuza brand yao itakua...ila
Kuanzia mechi ya Uto...
Mechi ya mlandege...
Yani hizo ni kelele za chura sisi waleeee...
Now Dunia nzima itajua Simba tunabebwa
 
Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), imesema kuwa Mwamuzi Nasri Salum hakustahili kuipa Simba kona iliyoifanya ipate bao la kusawazisha, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati ikicheza na Singida Fountain Gate jana kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Waziri Shekha amesema uamuzi wa kuipa Simba kona katika dakika za nyongeza, haukuwa sahihi na kwa mwamuzi huyo alifanya makosa, japo kamati hiyo haiwezi kumpa adhabu.

"Nilikwambia kwamba tutachunguza na tumekutana leo, tumebaini kwamba kulikuwa na makosa ya mwamuzi. Haikupaswa kuwa kona. Hakuna sehemu ambayo mpira ulichezwa na mchezaji wa Singida na kipa akaudakia nje, hivyo haikuwa sahihi kuwa kona,” amesema na kuongeza;

“Ni makosa ya kibinadamu na ndio kosa pekee tumeliona baada ya kupitia ripoti na marudio ila sehemu zingine zote alikuwaa sahihi. Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”
Ndio maana APR amesema hawatashiriki tena yaani wameitoa yanga refa amegomea goli na mlandege watu wapo kimyaa!
 
........ Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”
Hii makosa ya marefa huwa ni makubwa Sana sijui kwann huwa hayapewi uzito unaostahili. Hivi kweli kamati inaweza ikasema uzito WA Kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu? Hivi wanajua kama Hilo Kosa ndio limesababisha Singida kutolewa? Unasemaje Kosa halina uzito?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom