Simba SC bado gonjwa gonjwa!

Wana Simba msiwe na hofu, mimi jana nilikuwa uwanjani, ni kweli tumefungwa lakini tuseme tu bahati haikuwa upande wetu hiyo jana, timu ilicheza vizuri na tumefika golini mara kibao ndo maana baada ya mechi bado vijana tuliwapigia makofi kuwapongeza kwa soka waliloonyesha, hakuna shaka Azam lazima wakae hiyo j4 na Yeboyebo nao lazima wakae siku ya tarehe 03/10.


Nilibahatika pia kuiona Simba kipindi cha pili. Haya ni yale niliyoyaona.

Sofapaka ni timu nzuri, ila si sana. Simba sio mbaya kitimu na hata kwa mchezaji mmoja mmoja. Ubora na ushindi wa Sofapaka ulitokana na makosa yale yale yanayofanywa na Simba miaka nenda rudi. Tatizo la Simba si ubovu wa wachezaji mabeki, ila ni mfumo wa ulinzi. Simba inacheza soka la kufunguka na haifanyi marking ya kutosha kuanzia kwenye kiungo ndio maana inakuwa exposed kwa urahisi.

Nasema na timu nzuri ila yenye kasoro hiyo ambayo inapaswa kufanyiwa kazi haraka. Uzuri wa Simba ni kwenye kumiliki mpira, kucheza kwa mtiririko unaotakiwa na hata kwenye ladha yenyewe ya mpira. Halafu kikubwa zaidi ni kwamba uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ni mzuri, kama Ngasa, Akuffo, Boban, Christopher na wengine kadhaa. Kinyume na wengi wanaojaji kutokana na matokeo ya jana, hata beki kama Ochieng ni mzuri na alizheza vizuri. Hili n i gumu kuelezeka kwa shabiki wa kawaida na hasa shabiki kichaa. Na ndio maana katika kipindi hiki nilichokiona, Simba iliweza kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga japo kwa mshangao wa wengi ilikosa zote ikiwemo nafasi za wazi zaidi ya 3. Kitendo cha kutengeza nafasi tena sio za kulazimisha dhidi ya timu iliyojilinda vizuri kama Sofapaka, ni hatua nzuri.

Ubovu wa Simba ni mfumo mzima wa ulinzi. Baada ya kutaka kutafuta goli la kusawazisha kipindi cha pili na kuonekana kuielemea Sofapaka, akili yote ya timu haikuwa ktk kujihami. Na kila mipira waliyokuwa wakipokonywa Simba ilikuwa ni hatari sana kwa kuwa kulikuwa na mianya mingi an defence nzima ilikuwa ikicheza mbali mbali na ndio maana magoli ya Sofapaka yalionekana kupatikana kwa urahisi sana.

Narudia Sofapaka ni timu nzuri lakini si tishio. Hata upatikanaji wake wa magoli ulitokana na mianya iliyoachwa na Simba wenyewe na sio kutokana na mashambulizi ya maana. Ikikutana na timu yenye nidhamu kubwa kwenye ulinzi kwa mfano Yanga, nadhani inaweza kuwa kwenye matatizo zaidi. Kilichoibeba timu jana ni kupatikana kwa goli mapema kulikoifanya timu i-relax na kuendelea kufunga magoli rahisi. Sofapaka walionekana kumpa kazi sana golikipa wao na kumfanya nyota wa mchezo kwa kuokoa michomo kadhaa au kuwafanya Simba kukosa magoli wenyewe, kitu ambacho wakikutana na timu itakayotumia udhaifu huu, inaweza kujikuta matatizoni,

Mwisho, nipongeze mashabiki wa Simba kwa kuishangilia timu yao baada ya mechi licha ya kufumuliwa 3 -0. Ni moja ya matukio ya ajabu kwa mashabiki wa kitanzania kushangilia timu iliyofungwa hata bao 1-0, sembuse 3.
 
Yule wa kujifunga na kusababisha Penalt kila siku? yule bomu mbaya bora hata Juma Nyoso wetu,bado nakumbuka tambo za Mzee Zacharia Hans Pop ya kuwa sasa hivi wameamua kujikita kwenye kuchukua wachezaji wa Africa Magharibi ksbb wa ukanda huu wa Africa Mashariki hawajui mpira na si waaminifu,haya sasa kazi wanayo na pazia la usajili ndo lishafungwa

jipeni moyo tu, mkila mkono mwingine sijui mtajiteteaje!!
 
Back
Top Bottom