Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,153
Leo Simba na Yanga zimecheza hatua ya pili ya mtoano (klabu bingwa Afrika) zikiwa ugenini, Simba ikitoa sare kwa taabu sana dhidi ya Power Dynamos ya Zambia na Yanga ikipata ushindi wa kawaida wa goli mbili bila dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Bila kumumunya maneno, ni wazi Yanga na Simba zitavuka kirahisi kwenda hatua ya makundi katika kombe la klabu bingwa Afrika, na hii ni kwa sababu zimekutana na timu dhaifu.
Tukianza na Simba, mechi ya leo imeonyesha wazi Simba kuwa na safu ya ulinzi mbovu na safu ya ushambuliaji lege lege.
Tukija kwa Yanga ambayo iko kwenye moto mkali na imekutana na timu dhaifu kutoka Sudan imeshindwa kupata ushindi mnoo wa goli tano (kawa ilivyo kawaida yao) na kuishia kupata ushindi wa goli mbili tu.
Kwa wadadisi wa mpira wanajua wazi, Simba na Yanga zilipaswa kumaliza issue ya kufuzu makundi leo (kwa kupata ushindi mnono ugenini) , kuliko kungojea mechi za marudiano Dar.