Simba muwekeni kwenye eneo lenu la Makumbusho Athuman Mlenda, shabiki wenu aliyejiua kwa kujitumbukiza kwenye pipa la maji moto mwaka 1975

Brothers Karamazov

Senior Member
Jul 13, 2023
152
391
Tabora si haba kwa historia.

Mwaka 1975, Simba ilipigwa Na Yanga fainali ya Mapinduzi. Sasa Pale choma chankola, Igunga. Babu yake na Aden Rage, Mzee Dahel, alirecord matangazo ya ule mpira. Kisha Mzee akachukua bus mbili na kujaza mashabiki wa Yanga na kuanza kuzunguka mjini na spika zao zikitangaza huo mpira.

Sasa wamefika mtaa mmoja, kuna mama anawasimamisha, na kuwaeleza;

"kuna mtu amejidumbukiza kwenye pipa la maji moto".

Jamaa huyu alikuwa akiitwa Athumani Mlenda.

Simba kama Club waliubeba msiba huu na maziko yalifanyikia mtaa wa Mihogoni, Tabora mjini. Pia walicheza mechi ya hisani na Combine ya Tabora ambapo mapato yote ya Mechi, familia ya Mlenda ilipewa.

Kisa hiki nimesimuliwa na kaka wa Athumani.

Tukio la huyu jamaa kujiua tena kwa kujitumbukiza kwenye pipa la Maji moto, ni la kipekee na la kihistoria kwa mpira wa Simba na Tanzania kwa ujumla.

Kwa sababu ni tukio ambalo Simba inalifahamu pasi na shaka, nawashauri kwenye 'Section' yao pale Makumbusho ya Taifa muiweke.
 
Makolo watakuambia umetunga story, bora usawekee na hayo mahojiano na kaka wa muhanga.
 
Aden Rage aliwahi kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Simba bila yeye kuwepo...na mweka hazina wake alikuwa Said Salim Bakhresa.....1982

Simba ina history sana....

Mwingine aliewahi kuwaletea kocha Simba halafu mshahara ukawa unalipwa na serikali ni Samuel Sitta
 
Funguka mkuu ilikuwaje?
 
Hahaha. Dah! Huyu alikuwa Simba kindakindaki. Hivi, Nyerere alikuwa Timu gani?
Nyerere alikuwa Yanga Damu
Best wake alikuwa Mwenyekiti wa Yanga anaitwa Mzee Tabu Mangara...walikuwa wanacheza bao msasani....
Tabu Mangara ndo aliojenga jengo la Yanga pale Jangwani... inawezekana na serikali iliweka pia hela pale kimyaa kimyaa...Yanga ilikuwa timu ya wenyeji wazaramo...Huyo Mzee Mangara alikuwa mzaramo maarufu Sana...Simba ilikuwa timu ya waarabu wa mjini na wageni ambao hawataki Sana siasa... mpira Tu na burudani na biashara...Yanga ilikuwa na wenyeji ambao walikuwa pia wanashiriki siasa
 
i hope Nyerere hakuchukizwa na hilo 'kosa' la Sita.

Kuhusu hiyo historia ya Simba.

Huyo Mzee alinisimulia kuwa, Yanga ilikuwa timu ya wanaTAA. Serikali ya mkoloni ilianzisha Sunderland Sports Club ku-counter Yanga.
 
Huu ni upuuzi wa mwisho.
Natamani nimuone anamuambia nini mungu wake uko alipo.
Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom