Simba kuikamua Yanga milioni 50 za Hassan Kessy

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
kessy (1).jpg

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limeiamuru klabu ya Yanga kuilipa Simba shilingi milioni 50 kama fidia ya kukiuka utaratibu wa usajili wa mchezaji Hassan Ramadhani Kessy pamoja na kuitoza faini ya shilingi milioni 3.

Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:

1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.

2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.

3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.

4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.

5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Hassan Kessy na Klabu ya Simba.

6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.
HATUA:

Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69 ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania.

Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni
tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).

Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dcidi yake.
 
Wao wanataka billion moja wakati wanashindwa kumlipa Mkude million 80
 
kiko wapi mapovu mengi lakini huyu mchezaji kaponzwa na meneja uchwara meneja anayejua wajibu wake asingemuingiza mkenge mchezaji wake hili linatakiwa kuwa somo kwa wachezaji wote wanapaswa kuwa na watu wenye uelewa wa sheria na mikataba haya yote yasingetokea
 
Hii imetulia...maana Mkodisho FC ni malimbukeni sana kwa wachezaji wa Simba SC

Kwa Twite, walipanda dau wakalipa Simba 35ml

Kwa Ngasa walilipa 45ml

Na sasa kwa Kessy 50, na TFF 3ml na walimpa 50ml kwahivyo Total 93ml hii yote kwa ajili ya shobo nyingi sana.. na wasubiri rungu la Caf....!
 
1.Yanga haikupigwa fine issue ya Twite,Rage alipigwa bao

2.Ngasa alilipa deni lake mwenyewe Yanga haikulipa hata shilingi
 
Kama ukitumia akili ya ziada utagundua kuwa hiyo ni pesa ndogo sana kwa klabu kama ya Yanga inayomnunua Chirwa kwa mil 200.

Viongozi wako wamechanganyikiwa na vipesa hivyo.... Wewe shabiki unavifurahia. Dohhh... Ama kweli **********!
.
.
.
 
Swala la Twite Yanga walirudisha millioni 30 za Simba na kulipa gharama walizotumia kwenda Kigali.Ngassa alikatwa nusu mshahara kwenye deni lake.Aliposusia ikabidi ziachwe.

1.Yanga haikupigwa fine issue ya Twite,Rage alipigwa bao

2.Ngasa alilipa deni lake mwenyewe Yanga haikulipa hata shilingi
 
Kama ukitumia akili ya ziada utagundua kuwa hiyo ni pesa ndogo sana kwa klabu kama ya Yanga inayomnunua Chirwa kwa mil 200.

Viongozi wako wamechanganyikiwa na vipesa hivyo.... Wewe shabiki unavifurahia. Dohhh... Ama kweli **********!
.
.
.
Manji asipolipa itabidi mchange. Na kumbuka ni deni .Anadai bilioni 11 alizowakopesha. Chirwa si mchezaji hata wa millioni 20.Aliyetoa kaingizwa chaka big time.
 
Kama ukitumia akili ya ziada utagundua kuwa hiyo ni pesa ndogo sana kwa klabu kama ya Yanga inayomnunua Chirwa kwa mil 200.

Viongozi wako wamechanganyikiwa na vipesa hivyo.... Wewe shabiki unavifurahia. Dohhh... Ama kweli **********!
.
.
.
Mpira ni biashara hivyo mil 53 huwezi ukasema ni pesa ndogo wakati bingwa Wa vpl inayochezwa karibu miezi nane analipwa kiasi hicho hicho...
 
Mkuu Crashwise milioni 50 kwa siku 5 ni milioni 10 kila siku. Mkataba ulibakisha siku 5.Kwa kiherehere cha kuzoea kubebwa wakajua hamna kitakachotokea. Milioni 45 za Ngassa walimsusia alipe mwenyewe aliposusia ikabidi walipe .Leo wavimba macho wenye matatizo hata ya pesa ya vocha wanasema ni pesa ndogo sana.
 
View attachment 444260
Shirikisho la Soka Tanzania TFF limeiamuru klabu ya Yanga kuilipa Simba shilingi milioni 50 kama fidia ya kukiuka utaratibu wa usajili wa mchezaji Hassan Ramadhani Kessy pamoja na kuitoza faini ya shilingi milioni 3.

Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:

1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.

2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.

3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.

4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.

5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Hassan Kessy na Klabu ya Simba.

6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.
HATUA:

Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69 ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania.

Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni
tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).

Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dcidi yake.
na walipe tu na fitina fitina zao...!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom