Wewe uko ovyo. Kumbuka nchi hii imeendelea kuwa maskini kwasababu ya ujinga wa viongizi wachache kumbuka mikataba ya madini ambayo nchi hii iliingia na wazungu kwa miaka Zaid ya 100Umeinukuu kutoka wapi?
Naona umejitangaza kuwa upo Chuo Kikuu Mzumbe; huko hawawafundishi namna ya kuweka nukuu?
Ni lini na nchi gani ambako mtu binafsi alikwenda kukopa akaweka rehani ardhi, na aliposhindwa kulipa ardhi ya nhi hiyo ikatwaliwa na kuwa ya nchi nyingine. Unayo mifano ya namna hiyo utuwekee hapa nasi tuione?
Mradi wa Bagamoyo ni deni?
Inaonyesha huna ufahamu wa lolote unaloandika, kwa hiyo unachosha kusoma hata hayo mengine yaliyobaki kusomwa.
Mbona wanaoonekana kuwa wasomi wetu wamekuwa wajinga kiasi hiki?
Sasa usije hapa na kulalamika nawatetea Wachina au hao wakopaji wanaoweka rehani ardhi, kwa sababu najua kuna matapeli wengi, na kwa uhakika iwe ni nchi au taasisi unaowaendea kutafuta msaada (mkopo), ni lazima tu watataka wakugonge kiasi cha kutosha kama hujui unachotafuta.
Kwa usomi na uwezo huu mnaotuonyesha hapa, ni hakika kabisa tunapowatuma kwenda kufanya mapatano huko na hawa watu, nyinyi ni watu wa kugongwa tu, kwa sababu hamjiamini na wala hamna uthubutu wa kuonyesha uwezo mnao.
Nyinyi ndio wale wale, akina Chenge, wanaojidai wao mikataba haiwapi taabu kuielewa; wanaweza kuamshwa usingizini na kujua mkataba mzuri na mbaya! Majigambo yasiyokuwa na ukweli wowote tukichukulia mikataba aliyoipitisha akiwa Attorney General.
Na nyinyi, sio akina Chief Mangungo, kwani huyu hakupata fursa kama mliyopewa nyinyi. Tulijinyima sana kuwapa kidogo tulichokuwa nacho ghalani wakati wa njaa ili mkahemee kijiji cha jirani. Matokeo yake ndio haya tunayaona sasa hivi na akina Chenge na watu kama mleta mada.
Kama kweli unataka nchi yako ifanikiwe, usitumie udhaifu huu wa kutafuta sifa zisizo na maana. Kaa chini na hao unaojadiliana nao, ukijua vyema maslahi ya nchi yako na ukitambua unayejadiliana naye pia anayo maslahi yake.
Kosa nadhani tunafanya kuita vitu hivi kuwa ni 'msaada'. Hii sio misaada. Watu wanafanya biashara, hata kama ni mikopo.
Sasa hayo masharti unayotuletea hapa kama upo kwenye kampeni za siasa, sisi zitatusaidia nini kama si kukuona kuwa una ujinga umekujaa kichwani.
Imebidi niandike hivi, kwani inachosha sana kutufanya sote kama wapumbavu hivi tusioweza kuelewa kitu chochote.
Safari nyingine ukiandika kuhusu matapeli ya KiChina na serikali yao, jaribu kujitahidi ueleze pia jinsi wanavyojitetea kujikinga na kampeni hizi nyingi wanazofanyiwa na baadhi ya hao wanaowachota akili nyinyi.