Simama na Rais Magufuli kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo: Hatuwezi kuuza ardhi yetu vipande vipande kwa wageni

kibokomchapaji

Senior Member
Aug 18, 2017
165
307
Na
Felician Andrew
Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro

“Kuna watu wamechukulia mikopo mikubwa ya fedha kwenye mabenki ya ulaya huku dhamana zikiwa ni ardhi ya Tanzania hivyo wakishindwa kurejesha mikopo hiyo maana yake ardhi yetu itakuwa ni mali za mabenki hayo ya ughaibuni”

Nimeamua kuanza na nukuu hiyo ili uone mahala ambapo nchi yetu imefika kiwango ambacho watu wachache wenye uwezo wa kifedha wanaweza wakaweka rehani ardhi ambayo mababu zetu na wapigania uhuru walimwaga damu zao ili leo hii iweze kuwanufaisha watanzania wote. Ukaribu kabisa wa jambo hili linafanana na mkataba wenye masharti ya kinyonyaji ambao kampuni ya kibepari ya China Merchants Port Holdings Company Limited yenye Makao yake makuu Hong Kong inataka Tanzania kuingia mtego na mwisho kujimilikisha ardhi na mali za taifa hili kwa muda mrefu.

Historia inaonyesha ya kuwa mjerumani Karl Peters maarufu kama Mkono wa Damu akiwa na umri wa miaka 28 katika mwaka 1884 alisafiri kutoka Ujerumani akijifanya fundi makenikia (Machenical Engineer )hadi kufika Zanzibar na baadae kuingia bara katika mwaka huo huo. Walifika Saadani mkaoni Tanga wakasafiri tena hadi Uzigua ambako hapo ndio walimsainicha Chifu Mbwela wa Uzigua mkataba wa kwanza na kila walikopita waliwasainisha machifu mikataba ya ulaghai iliyokuw an alengo la kuina ardhi kutoka mikononi mwa wazawa na kwenda chini ya himaya ya ujerumani.

Mkataba maarufu unaotajwa sana ni ule wa Chifu Mangungo wa Msovero na Karl Peters uliofanywa Novemba 1884, sehemu ndogo ya mkataba huu ilisema ya kuwa….
“Mangungo offers all his territory with all its civil appurtenances to Dr. Karl Peters, as the representative of the Society for German Colonization, for the exclusive and universal utilization for German colonization.” Kwa tafisiri rahisi ya Kiswahili ilimaanisha ya kuwa “Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani (Society for German Colonization), kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.”

Sehemu kubwa ya wizi na uporaji wa haki ya watu hawa waliokuwa chini ya Mangungo ulifanywa na aliyekuwa mkalimani aliyejulikana kwa jina la Ramzan ambaye kwa sehemu kubwa alimpotosha Mangungo mpaka kuingia kwenye Maktaba huu wa ulaghai na mwisho kkujikuta wamegawa kwa wajerumani sehemu yote ya ardhi pamoja na watu wao.

KISA CHA MANGUNGO NA BANDARI YA BAGAMOYO
Mwaka 2015 serikali ya Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete iliingia makaubaliano ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo ilikuwa inagharimu zaidi ya shilingi za kitanzania trlliioni 22. Kwa mujibu wa makubaliano ya Mradi huu kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited iliyoanzishwa mwaka 1997 ndio ilikuwa na jukumu la ujenzi huku fedha nyingine zikiwa ni ushirikiano baina ya serikali ya Oman na Tanzania.

Mradi huu ambao kwa muonekano wa kibiashara ni mzuri na wenye faida nyingi lakini ndani yake ulijaa masharti magumu ambayo yangepelekea mpaka kukamilika kwa ujenzi wake basi Tanzania isingekuwa na uwezo wa kulipa deni hilo na mwisho bandari hiyo kurudi tena mikononi mwa kampuni hii kubwa ya China ambayo imekuwa ikifanya michezo hii kwa mataifa mengi duniani.

Masharti yaliyomo kwenye mkataba au makubaliano haya yanailazimisha serikali ya Tanzania kuwa tayari kuachia bandari kuendeshwa na wachina kwa muda wa miaka 33 hadi 99 mpaka pale kampuni hoiyo itakapokuwa imerudisha fedha zake; mtego huu ndio sababu ya watanzania wote tuatakiwa kusimama na kumuunga mkono Rais Magufuli kwani kama serikali ingekubali mradi huu kutekeelzeka kwa matakwa ya kampunii hii basi sehemu yote ya Bandari hiyo ingekuwa chini ya umiliki wa Kampuni hii ya China kwa muda mrefu mpaka miaka 99.

Huu ni mfano tosha wa mkataba wa Uchimbaji wa gesi kule mkoani Mtwara ambapo katika mkataba sehemu ya gesi iliyokuwa inachimbwa ilitakiwa kusafirishwa kwenda nchini China.

Serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli kukataa masharti ya kinyonyaji yaliyomo ndani ya mikataba hii ya makampuni makubwa kunamfanya Rais Magufuli kuishi maneno ya Mwalimu Nyerere baada ya kukataa makampuni ya kinyonyaji kuchimba madini na kusema tutachimba madini siku tukiwa tayari tukiwa na vizazi vyenye uwezo wa kusimamia madini yao na tukiwa na wataalamu wakutosha kuongoza sekta hiyo ya madini nchini. Hata sasa Rais Magufuli amehakikisha jambo hili halifanyiki kwani kama angekubali basi taifa linhekuwa limeingia katika mtego wa kuingia kwenye mkataba wa ulaghai.

Kisa cha Djibout na Kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited
Hadi kufikia Februari 2019, nchi ya Djibout iliiingia kwenye mgogoro mkubwa wa umiliki wa Bandari iliyojengwa na kampuni hili kubwa ya kichina ambayo ilipelekea nchi ya Djibout kukosa uhalali wa umiliki wa bandari yao ambayo ndio bandari kubwa kabisa katika rasi ya afria Mashariki.

Kupitia mikataba hii ya kilaghai viongozi wa taifa la Djibout wamejikuta sasa wana deni kubwa ambalo ni sawa na asilimia 44 ya Mapato ya taifa hilo yaani GDP fedha ambayo inaifanya basnari hiyo kuw achini ya umiliki wa ampuni hii yakichina kwa muda wa miaka 30 huku kampuni hiyo ikiw ana uwezo wa kujenga tena na kupanua au kufanya biashara kwenye badnari hiyo kadriwatakavyo bila kuingiliwa na nchi ya Djibout. UNaweza ukashangaa mambo haya yanafanyikaje katika dunia ya leo ila huu ni mfano halisi wa mikataba ya ulaghai ambayo nchi masikini au zinazoendelea zimekuwa zikiingia mkenge kwenye kampuni hili kubwa la China.

Kisa cha Bandari ya Sri lanka na Kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited
Mwaka 2017 serikali ya Sri Lanka iliingai makubalinao na kampuni hii kwa ajili ya ujenzi wa Bandari iliyojulikana kama Hambantota Port huku makubaliano yakiwa yanahusisha utaoji wa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 1.2 kwa mkataba wa miaka 99 huku kampuni hiyo ikiwa inachukua asilimia 85 ya umiliki wa Bandar na eneo la zaidi ya hekari 15000.

Kutokana na uharaka wa viongozi wa Sri Lanka na kwa kuwa walikuwa wakielekea kwenye uchaguzi wakajikuta wanaingia makubaliano yale na kusaini kuuza ardhi na bandari yao kwa kampuni hii ya kichina kwa muda wa miaka 99 kutokana na deni hilo kukua kwa kasi kulinganisha na uwezo wa taifa hilo kulipa deni hilo kubwa.

Ni mikataba kama hii ndiyo imeifanya leo nchi jirani ya Zambia kuwa katika hatari kubwa ya kuporwa Shirika lake la Umeme (ZESCO), Shirika la Utangazaji Zambia (ZNBC) pamoja na Airpot ya Keneth Kaunda ili kufidia deni ambalo lilikopwa na serikali ya Zmabi kutoka China

Nchi ya Angola imepata pia pigo kama hilo baada yakushindwa kulipa deni lae na kujikuta ikitakiwa kutoa sehemu kubwa ya mafuta yanayozalishwa nchini humo kupelekwa China kama sehemu ya kupunguza deni ambalo wanadaiwa na makampuni ya fedha ya nchini China ikiwemo EXIM BANK CHINA, Benki ya Viwanda na Biashara ya China na Beki ya Maendeleo ya China yenye thamani ya dola za marekani bilioni 14.5 na jambo hili sasa linaifanya China kuwa taifa la pili kwa usambazaji wa mafuta duniani nyuma ya Saudi Arabia.

Yako mataifa mengi ambayo yameingia katika mikataba hii ya ulaghai na kampuni hii kubwa ya ujenzi wa Bandari kutokea China ambayo ni moja katik ya makampuni makubwa duniani yenye uwezo mkubwa wa kifedha huku India ikiwa ni moja kati ya mataifa ya mfano duniani kukataa ofa kama ile waliyopewa Sri Lanka ya ujenzi wa bandari.

Mwisho:
Rais Magufuli kwa niaba ya watanzania wote ameweka mbele maslahi ya nchi hii na muda wote amesimamia maslahi ya nchi yetu kwa kupigania na kuwapinga wanyonyaji hadharani. Uhuru wa nchi yetu na rasilimali zake lazima ulindwe kwa gharam zote kwani ni jambo la aibu kuingia makubaliano ambayo mwekezaji atakuwa mamlaka makubwa ya kiwango ambacho ndiye atakua mmiliki wa bandari na atakuwa mwenye mamlaka ya kupnaga kiwango cha tozo badnarini, atakuwa na mamlka ya kukusnya tozo za bandarini na kuusimamia mradi bila kuingiliwa na mtu yeyote mpaka hapo atakapokuwa amerejesha gaharama zake. Mikataba ya hivi ni mikataba ya kikoloni yenye lengo ya kuzirudisha nyuma nchi za kiafrika katika zama za ukoloni.

Kwa mantiki hii tuwakatae wanasiasa wote wanaotumika na makampuni haya makubwa ili kushinikiza utekelezaji wa miradi hii ya kinyonyaji nchini na kujikuta tunaingia kweny emitego kama ambayo nchi nyingine duniani na afrika zimeishaingia.

Tanzania ni moja, na Hakuna Tanzania nyingine hivyo miradi yote na mambo yote lazima yazingatie maslahi mpana ya taifa letu kama ambavyo amefanya Rais Magufuli.
Nasimama na Rais Magufuli, Nachagua kuwa Mzalendo.
 
JPM knows what is doing as a president.
 
Kuna watu wamechukulia mikopo mikubwa ya fedha kwenye mabenki ya ulaya huku dhamana zikiwa ni ardhi ya Tanzania hivyo wakishindwa kurejesha mikopo hiyo maana yake ardhi yetu itakuwa ni mali za mabenki hayo ya ughaibuni”
Umeinukuu kutoka wapi?
Naona umejitangaza kuwa upo Chuo Kikuu Mzumbe; huko hawawafundishi namna ya kuweka nukuu?

Ni lini na nchi gani ambako mtu binafsi alikwenda kukopa akaweka rehani ardhi, na aliposhindwa kulipa ardhi ya nhi hiyo ikatwaliwa na kuwa ya nchi nyingine. Unayo mifano ya namna hiyo utuwekee hapa nasi tuione?

Mradi wa Bagamoyo ni deni?
Inaonyesha huna ufahamu wa lolote unaloandika, kwa hiyo unachosha kusoma hata hayo mengine yaliyobaki kusomwa.

Mbona wanaoonekana kuwa wasomi wetu wamekuwa wajinga kiasi hiki?

Sasa usije hapa na kulalamika nawatetea Wachina au hao wakopaji wanaoweka rehani ardhi, kwa sababu najua kuna matapeli wengi, na kwa uhakika iwe ni nchi au taasisi unaowaendea kutafuta msaada (mkopo), ni lazima tu watataka wakugonge kiasi cha kutosha kama hujui unachotafuta.
Kwa usomi na uwezo huu mnaotuonyesha hapa, ni hakika kabisa tunapowatuma kwenda kufanya mapatano huko na hawa watu, nyinyi ni watu wa kugongwa tu, kwa sababu hamjiamini na wala hamna uthubutu wa kuonyesha uwezo mnao.

Nyinyi ndio wale wale, akina Chenge, wanaojidai wao mikataba haiwapi taabu kuielewa; wanaweza kuamshwa usingizini na kujua mkataba mzuri na mbaya! Majigambo yasiyokuwa na ukweli wowote tukichukulia mikataba aliyoipitisha akiwa Attorney General.

Na nyinyi, sio akina Chief Mangungo, kwani huyu hakupata fursa kama mliyopewa nyinyi. Tulijinyima sana kuwapa kidogo tulichokuwa nacho ghalani wakati wa njaa ili mkahemee kijiji cha jirani. Matokeo yake ndio haya tunayaona sasa hivi na akina Chenge na watu kama mleta mada.

Kama kweli unataka nchi yako ifanikiwe, usitumie udhaifu huu wa kutafuta sifa zisizo na maana. Kaa chini na hao unaojadiliana nao, ukijua vyema maslahi ya nchi yako na ukitambua unayejadiliana naye pia anayo maslahi yake.

Kosa nadhani tunafanya kuita vitu hivi kuwa ni 'msaada'. Hii sio misaada. Watu wanafanya biashara, hata kama ni mikopo.

Sasa hayo masharti unayotuletea hapa kama upo kwenye kampeni za siasa, sisi zitatusaidia nini kama si kukuona kuwa una ujinga umekujaa kichwani.

Imebidi niandike hivi, kwani inachosha sana kutufanya sote kama wapumbavu hivi tusioweza kuelewa kitu chochote.

Safari nyingine ukiandika kuhusu matapeli ya KiChina na serikali yao, jaribu kujitahidi ueleze pia jinsi wanavyojitetea kujikinga na kampeni hizi nyingi wanazofanyiwa na baadhi ya hao wanaowachota akili nyinyi.
 
Kwa mantiki hii tuwakatae wanasiasa wote wanaotumika na makampuni haya makubwa ili kushinikiza utekelezaji wa miradi hii ya kinyonyaji nchini na kujikuta tunaingia kweny emitego kama ambayo nchi nyingine duniani na afrika zimeishaingia.
Ala, kumbe ni kampeni ya kisiasa!
 
maneno ya Mwalimu Nyerere baada ya kukataa makampuni ya kinyonyaji kuchimba madini na kusema tutachimba madini siku tukiwa tayari tukiwa na vizazi vyenye uwezo wa kusimamia madini yao na tukiwa na wataalamu wakutosha kuongoza sekta hiyo ya madini nchini.
Yaani unapoandika maneno mazito kama haya wakati huu huoni aibu kweli? Au huelewi Mwalimu alikuwa anasema nini?
 
Mwaka 2015 serikali ya Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete iliingia makaubaliano ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo ilikuwa inagharimu zaidi ya shilingi za kitanzania trlliioni 22. Kwa mujibu wa makubaliano ya Mradi huu kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited iliyoanzishwa mwaka 1997 ndio ilikuwa na jukumu la ujenzi huku fedha nyingine zikiwa ni ushirikiano baina ya serikali ya Oman na Tanzania.
Hii ina nichanganya: Mkulu alikuwa waziri katika serikali hiyo, najiuliza hakuyajua hayo au ndiyo kaamka toka usingizini?
Pili kwa maandishi haya na mengine kuhusu jambo hili inaelekea yule aliyekuwa anaitwa rafiki wetu mkubwa mwenye misaada, mikopo n.k. isiyo na mashariti nae ni BEBERU wa aina yake.
Tatu Mifano yote aliyetoa mwandishi wa mada hii-ni dhahiri kuwa wahusika wenyewe kwa sababu wanazozijua wao walimwaga wino wakijua mashariti ya mikataba hiyo au kuna aliyelazimishwa?
Nne mikataba mingi ya aina hii inakuwa siri wanafahamu wenyewe, je ni percent ngapi hutembea hapa?
SOMO 1: Hapa nafikiri ndiyo BUNGE linapotakiwa kusimamia mambo haya kwa uwazi, nchi haiwezi kutegemea matakwa ya raisi aliye madarakani, mmoja na serikali yake (akiwemo JPM) walikuwa wameshatuingiza mkenge na sasa mwingine JPM inasemekana "katukomboa". Akija mwingine tunauzwa tena (kwa katiba hii, UCAHAMADOLA na ukondoo wetu hatuwezi kumzuia akitaka). Tuna institutions dhaifu (hata kama Ndugai anataka tuamini vinginevyo) na Maraisi wenye nguvu kupitiliza ndio maana wanatugeuza wapendavyo wakati bunge lenyewe halijitambui. Bila mabadiliko ya kimifumo haya hayatakwisha.

SOMO 2: UBEBERU na URAFIKI havina rangi kama watu fulani walivyotaka kutuaminisha. Kila nchi ilinde masilahi yake. Ukilala unaliwa tu-haijalishi kuwa unadeal na nchi gani.
 
that bagamoyo thing is not mkopo,it an investiment,Direct Foreign Investment
Mimi Nataka nijue tu, hao wachina Watalipa kodi?

Kwenye negotiations serikali ikiona mchina anakaza na wao waweke vipengele vipya! Mchina ale operations za bandari ila atoe mkopo nafuu wa kutandaza SGR vipande vilivyobaki na makandarasi awe huyu huyu mturuki.
 
hiyo project ingefanana na project iliyoko pakistan,Gwadar port,google that,au bandari ya chabahar ilojengwa na india,lakini mi naona tuachane na hii kitu,maana maneno yamekuwa mingi sana,mwisho watu wataumia kwa vitu kaa hivi
 
..mimi siamini kama Jiwe ni muadilifu.

..ana rekodi ya kuuza nyumba za serekali nchi nzima kwa bei ya kutupa.
 
Na
Felician Andrew
Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro

“Kuna watu wamechukulia mikopo mikubwa ya fedha kwenye mabenki ya ulaya huku dhamana zikiwa ni ardhi ya Tanzania hivyo wakishindwa kurejesha mikopo hiyo maana yake ardhi yetu itakuwa ni mali za mabenki hayo ya ughaibuni”

Nimeamua kuanza na nukuu hiyo ili uone mahala ambapo nchi yetu imefika kiwango ambacho watu wachache wenye uwezo wa kifedha wanaweza wakaweka rehani ardhi ambayo mababu zetu na wapigania uhuru walimwaga damu zao ili leo hii iweze kuwanufaisha watanzania wote. Ukaribu kabisa wa jambo hili linafanana na mkataba wenye masharti ya kinyonyaji ambao kampuni ya kibepari ya China Merchants Port Holdings Company Limited yenye Makao yake makuu Hong Kong inataka Tanzania kuingia mtego na mwisho kujimilikisha ardhi na mali za taifa hili kwa muda mrefu.

Historia inaonyesha ya kuwa mjerumani Karl Peters maarufu kama Mkono wa Damu akiwa na umri wa miaka 28 katika mwaka 1884 alisafiri kutoka Ujerumani akijifanya fundi makenikia (Machenical Engineer )hadi kufika Zanzibar na baadae kuingia bara katika mwaka huo huo. Walifika Saadani mkaoni Tanga wakasafiri tena hadi Uzigua ambako hapo ndio walimsainicha Chifu Mbwela wa Uzigua mkataba wa kwanza na kila walikopita waliwasainisha machifu mikataba ya ulaghai iliyokuw an alengo la kuina ardhi kutoka mikononi mwa wazawa na kwenda chini ya himaya ya ujerumani.

Mkataba maarufu unaotajwa sana ni ule wa Chifu Mangungo wa Msovero na Karl Peters uliofanywa Novemba 1884, sehemu ndogo ya mkataba huu ilisema ya kuwa….
“Mangungo offers all his territory with all its civil appurtenances to Dr. Karl Peters, as the representative of the Society for German Colonization, for the exclusive and universal utilization for German colonization.” Kwa tafisiri rahisi ya Kiswahili ilimaanisha ya kuwa “Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani (Society for German Colonization), kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.”

Sehemu kubwa ya wizi na uporaji wa haki ya watu hawa waliokuwa chini ya Mangungo ulifanywa na aliyekuwa mkalimani aliyejulikana kwa jina la Ramzan ambaye kwa sehemu kubwa alimpotosha Mangungo mpaka kuingia kwenye Maktaba huu wa ulaghai na mwisho kkujikuta wamegawa kwa wajerumani sehemu yote ya ardhi pamoja na watu wao.

KISA CHA MANGUNGO NA BANDARI YA BAGAMOYO
Mwaka 2015 serikali ya Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete iliingia makaubaliano ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo ilikuwa inagharimu zaidi ya shilingi za kitanzania trlliioni 22. Kwa mujibu wa makubaliano ya Mradi huu kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited iliyoanzishwa mwaka 1997 ndio ilikuwa na jukumu la ujenzi huku fedha nyingine zikiwa ni ushirikiano baina ya serikali ya Oman na Tanzania.

Mradi huu ambao kwa muonekano wa kibiashara ni mzuri na wenye faida nyingi lakini ndani yake ulijaa masharti magumu ambayo yangepelekea mpaka kukamilika kwa ujenzi wake basi Tanzania isingekuwa na uwezo wa kulipa deni hilo na mwisho bandari hiyo kurudi tena mikononi mwa kampuni hii kubwa ya China ambayo imekuwa ikifanya michezo hii kwa mataifa mengi duniani.

Masharti yaliyomo kwenye mkataba au makubaliano haya yanailazimisha serikali ya Tanzania kuwa tayari kuachia bandari kuendeshwa na wachina kwa muda wa miaka 33 hadi 99 mpaka pale kampuni hoiyo itakapokuwa imerudisha fedha zake; mtego huu ndio sababu ya watanzania wote tuatakiwa kusimama na kumuunga mkono Rais Magufuli kwani kama serikali ingekubali mradi huu kutekeelzeka kwa matakwa ya kampunii hii basi sehemu yote ya Bandari hiyo ingekuwa chini ya umiliki wa Kampuni hii ya China kwa muda mrefu mpaka miaka 99.

Huu ni mfano tosha wa mkataba wa Uchimbaji wa gesi kule mkoani Mtwara ambapo katika mkataba sehemu ya gesi iliyokuwa inachimbwa ilitakiwa kusafirishwa kwenda nchini China.

Serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli kukataa masharti ya kinyonyaji yaliyomo ndani ya mikataba hii ya makampuni makubwa kunamfanya Rais Magufuli kuishi maneno ya Mwalimu Nyerere baada ya kukataa makampuni ya kinyonyaji kuchimba madini na kusema tutachimba madini siku tukiwa tayari tukiwa na vizazi vyenye uwezo wa kusimamia madini yao na tukiwa na wataalamu wakutosha kuongoza sekta hiyo ya madini nchini. Hata sasa Rais Magufuli amehakikisha jambo hili halifanyiki kwani kama angekubali basi taifa linhekuwa limeingia katika mtego wa kuingia kwenye mkataba wa ulaghai.

Kisa cha Djibout na Kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited
Hadi kufikia Februari 2019, nchi ya Djibout iliiingia kwenye mgogoro mkubwa wa umiliki wa Bandari iliyojengwa na kampuni hili kubwa ya kichina ambayo ilipelekea nchi ya Djibout kukosa uhalali wa umiliki wa bandari yao ambayo ndio bandari kubwa kabisa katika rasi ya afria Mashariki.

Kupitia mikataba hii ya kilaghai viongozi wa taifa la Djibout wamejikuta sasa wana deni kubwa ambalo ni sawa na asilimia 44 ya Mapato ya taifa hilo yaani GDP fedha ambayo inaifanya basnari hiyo kuw achini ya umiliki wa ampuni hii yakichina kwa muda wa miaka 30 huku kampuni hiyo ikiw ana uwezo wa kujenga tena na kupanua au kufanya biashara kwenye badnari hiyo kadriwatakavyo bila kuingiliwa na nchi ya Djibout. UNaweza ukashangaa mambo haya yanafanyikaje katika dunia ya leo ila huu ni mfano halisi wa mikataba ya ulaghai ambayo nchi masikini au zinazoendelea zimekuwa zikiingia mkenge kwenye kampuni hili kubwa la China.

Kisa cha Bandari ya Sri lanka na Kampuni ya China Merchants Port Holdings Company Limited
Mwaka 2017 serikali ya Sri Lanka iliingai makubalinao na kampuni hii kwa ajili ya ujenzi wa Bandari iliyojulikana kama Hambantota Port huku makubaliano yakiwa yanahusisha utaoji wa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 1.2 kwa mkataba wa miaka 99 huku kampuni hiyo ikiwa inachukua asilimia 85 ya umiliki wa Bandar na eneo la zaidi ya hekari 15000.

Kutokana na uharaka wa viongozi wa Sri Lanka na kwa kuwa walikuwa wakielekea kwenye uchaguzi wakajikuta wanaingia makubaliano yale na kusaini kuuza ardhi na bandari yao kwa kampuni hii ya kichina kwa muda wa miaka 99 kutokana na deni hilo kukua kwa kasi kulinganisha na uwezo wa taifa hilo kulipa deni hilo kubwa.

Ni mikataba kama hii ndiyo imeifanya leo nchi jirani ya Zambia kuwa katika hatari kubwa ya kuporwa Shirika lake la Umeme (ZESCO), Shirika la Utangazaji Zambia (ZNBC) pamoja na Airpot ya Keneth Kaunda ili kufidia deni ambalo lilikopwa na serikali ya Zmabi kutoka China

Nchi ya Angola imepata pia pigo kama hilo baada yakushindwa kulipa deni lae na kujikuta ikitakiwa kutoa sehemu kubwa ya mafuta yanayozalishwa nchini humo kupelekwa China kama sehemu ya kupunguza deni ambalo wanadaiwa na makampuni ya fedha ya nchini China ikiwemo EXIM BANK CHINA, Benki ya Viwanda na Biashara ya China na Beki ya Maendeleo ya China yenye thamani ya dola za marekani bilioni 14.5 na jambo hili sasa linaifanya China kuwa taifa la pili kwa usambazaji wa mafuta duniani nyuma ya Saudi Arabia.

Yako mataifa mengi ambayo yameingia katika mikataba hii ya ulaghai na kampuni hii kubwa ya ujenzi wa Bandari kutokea China ambayo ni moja katik ya makampuni makubwa duniani yenye uwezo mkubwa wa kifedha huku India ikiwa ni moja kati ya mataifa ya mfano duniani kukataa ofa kama ile waliyopewa Sri Lanka ya ujenzi wa bandari.

Mwisho:
Rais Magufuli kwa niaba ya watanzania wote ameweka mbele maslahi ya nchi hii na muda wote amesimamia maslahi ya nchi yetu kwa kupigania na kuwapinga wanyonyaji hadharani. Uhuru wa nchi yetu na rasilimali zake lazima ulindwe kwa gharam zote kwani ni jambo la aibu kuingia makubaliano ambayo mwekezaji atakuwa mamlaka makubwa ya kiwango ambacho ndiye atakua mmiliki wa bandari na atakuwa mwenye mamlaka ya kupnaga kiwango cha tozo badnarini, atakuwa na mamlka ya kukusnya tozo za bandarini na kuusimamia mradi bila kuingiliwa na mtu yeyote mpaka hapo atakapokuwa amerejesha gaharama zake. Mikataba ya hivi ni mikataba ya kikoloni yenye lengo ya kuzirudisha nyuma nchi za kiafrika katika zama za ukoloni.

Kwa mantiki hii tuwakatae wanasiasa wote wanaotumika na makampuni haya makubwa ili kushinikiza utekelezaji wa miradi hii ya kinyonyaji nchini na kujikuta tunaingia kweny emitego kama ambayo nchi nyingine duniani na afrika zimeishaingia.

Tanzania ni moja, na Hakuna Tanzania nyingine hivyo miradi yote na mambo yote lazima yazingatie maslahi mpana ya taifa letu kama ambavyo amefanya Rais Magufuli.
Nasimama na Rais Magufuli, Nachagua kuwa Mzalendo.
Mkuu umezunguka sana ila huna ulichokiongea. Tupe vipengele vya mkataba vinasemaje na sio kutupa mifano ya bandari za nchi nyingine. Je kama mkataba wetu mzuri je kiliko wa hizo nchi ulizotaja
 
Hii ina nichanganya: Mkulu alikuwa waziri katika serikali hiyo, najiuliza hakuyajua hayo au ndiyo kaamka toka usingizini?
Pili kwa maandishi haya na mengine kuhusu jambo hili inaelekea yule aliyekuwa anaitwa rafiki wetu mkubwa mwenye misaada, mikopo n.k. isiyo na mashariti nae ni BEBERU wa aina yake.
Tatu Mifano yote aliyetoa mwandishi wa mada hii-ni dhahiri kuwa wahusika wenyewe kwa sababu wanazozijua wao walimwaga wino wakijua mashariti ya mikataba hiyo au kuna aliyelazimishwa?
Nne mikataba mingi ya aina hii inakuwa siri wanafahamu wenyewe, je ni percent ngapi hutembea hapa?
SOMO 1: Hapa nafikiri ndiyo BUNGE linapotakiwa kusimamia mambo haya kwa uwazi, nchi haiwezi kutegemea matakwa ya raisi aliye madarakani, mmoja na serikali yake (akiwemo JPM) walikuwa wameshatuingiza mkenge na sasa mwingine JPM inasemekana "katukomboa". Akija mwingine tunauzwa tena (kwa katiba hii, UCAHAMADOLA na ukondoo wetu hatuwezi kumzuia akitaka). Tuna institutions dhaifu (hata kama Ndugai anataka tuamini vinginevyo) na Maraisi wenye nguvu kupitiliza ndio maana wanatugeuza wapendavyo wakati bunge lenyewe halijitambui. Bila mabadiliko ya kimifumo haya hayatakwisha.

SOMO 2: UBEBERU na URAFIKI havina rangi kama watu fulani walivyotaka kutuaminisha. Kila nchi ilinde masilahi yake. Ukilala unaliwa tu-haijalishi kuwa unadeal na nchi gani.
Huu ujinga mtauacha lini eti Magu hakuwapo ktk hiyo serikali, yeye alikuwa rais? Ufipa mmelaaniea kwa kweli na Mungu awasukumizie zaidi huko kwenye laana zaidi!
 
Umeinukuu kutoka wapi?
Naona umejitangaza kuwa upo Chuo Kikuu Mzumbe; huko hawawafundishi namna ya kuweka nukuu?

Ni lini na nchi gani ambako mtu binafsi alikwenda kukopa akaweka rehani ardhi, na aliposhindwa kulipa ardhi ya nhi hiyo ikatwaliwa na kuwa ya nchi nyingine. Unayo mifano ya namna hiyo utuwekee hapa nasi tuione?

Mradi wa Bagamoyo ni deni?
Inaonyesha huna ufahamu wa lolote unaloandika, kwa hiyo unachosha kusoma hata hayo mengine yaliyobaki kusomwa.

Mbona wanaoonekana kuwa wasomi wetu wamekuwa wajinga kiasi hiki?

Sasa usije hapa na kulalamika nawatetea Wachina au hao wakopaji wanaoweka rehani ardhi, kwa sababu najua kuna matapeli wengi, na kwa uhakika iwe ni nchi au taasisi unaowaendea kutafuta msaada (mkopo), ni lazima tu watataka wakugonge kiasi cha kutosha kama hujui unachotafuta.
Kwa usomi na uwezo huu mnaotuonyesha hapa, ni hakika kabisa tunapowatuma kwenda kufanya mapatano huko na hawa watu, nyinyi ni watu wa kugongwa tu, kwa sababu hamjiamini na wala hamna uthubutu wa kuonyesha uwezo mnao.

Nyinyi ndio wale wale, akina Chenge, wanaojidai wao mikataba haiwapi taabu kuielewa; wanaweza kuamshwa usingizini na kujua mkataba mzuri na mbaya! Majigambo yasiyokuwa na ukweli wowote tukichukulia mikataba aliyoipitisha akiwa Attorney General.

Na nyinyi, sio akina Chief Mangungo, kwani huyu hakupata fursa kama mliyopewa nyinyi. Tulijinyima sana kuwapa kidogo tulichokuwa nacho ghalani wakati wa njaa ili mkahemee kijiji cha jirani. Matokeo yake ndio haya tunayaona sasa hivi na akina Chenge na watu kama mleta mada.

Kama kweli unataka nchi yako ifanikiwe, usitumie udhaifu huu wa kutafuta sifa zisizo na maana. Kaa chini na hao unaojadiliana nao, ukijua vyema maslahi ya nchi yako na ukitambua unayejadiliana naye pia anayo maslahi yake.

Kosa nadhani tunafanya kuita vitu hivi kuwa ni 'msaada'. Hii sio misaada. Watu wanafanya biashara, hata kama ni mikopo.

Sasa hayo masharti unayotuletea hapa kama upo kwenye kampeni za siasa, sisi zitatusaidia nini kama si kukuona kuwa una ujinga umekujaa kichwani.

Imebidi niandike hivi, kwani inachosha sana kutufanya sote kama wapumbavu hivi tusioweza kuelewa kitu chochote.

Safari nyingine ukiandika kuhusu matapeli ya KiChina na serikali yao, jaribu kujitahidi ueleze pia jinsi wanavyojitetea kujikinga na kampeni hizi nyingi wanazofanyiwa na baadhi ya hao wanaowachota akili nyinyi.
Mkuu sijakuelewa haswa point yako nini hapa, kama unamuona huyu mleta uzi hoja yake mufilisi hebu sema hoja yako ni ipi haswa? Vyo vyote tutakavyobishana kuhusu tija ya huu mradi wa Bagamoyo na mingine kama hii tukumbuke kama ni kuwapa uendeshaji wa 100% kuna hatari zake haswa pale mbele ni wakati wa uendeshaji kunapotokea migogoro ya aina yoyote ile kwa mfano: uendeshaji mbaya au wakibaguzi kwenye huo mradi unaofanywa na kampuni yenye mradi. Kwenye hali kama hiyo mnafanyaje isije ikawa WaTanzania wananyanyaswa kwenye Ardhi yao na serikali haina cha kufanya sababu ya mikataba inayowafunga mikono. Ukiangalia kwa upande wa tamaa ya maslahi ni rahisi kurukia na kusema ndio njia rahisi kuelekea maendeleo lakini kuna misemo mingi ya hekima inayotupa tahadhali sana na kitu fadhira. Cha mtu Mavi na Wafadhiraka Wapundaka kwa maana anaekufadhili ndio atakae kugeuza punda. Sidhani kama WaTanzania tumefika mahali pa kuweza kujadili mikataba yenye kuangalia na kutetea maslahi ya nchi yetu kiasi cha kuamini kuingia mkataba kama huo. Kama ulivyosema tunao wakina Chenge wengi tu ambao hawasiti kuuza Ardhi kwa manufaa binafsi angalia mfano wa Loliondo hivyo huwa tunajiuliza vizuri jinsi gani nchi ya Tanzania iliuza kipande cha Ardhi yake tena sehemu ya mbuga za Wanyama kwa familia ya kifalme ya Uarabuni au tumeshasahau??? Hii sio ile ya wakina Chifu Mangungo tunazungumzia juzi tu hapa na hata wahusika mpaka leo wako hai na wanatawala au mkuu hujui hii? Achilia mbali hiyo; mikataba ya madini iliyoingia na serikali yetu ilikuwa ni sawa na kugawa bure tuna mifano hai ya hata hao Wazungu waliokuwa wanachimba huko kutuambia wazi wazi kuwa sisi wajinga sana kwa jinsi wasivyoamini jinsi tulivyowaachia mali zetu bila hiyana!!! Sasa mkuu mpaka hapo hujaumwa na nyoka na ukiona ujani unashtuka?? Tusione hatupigi hatua tukadhani kuna lolote gumu sana linalosababisha, la hasha!!! Adui yetu ni sisi wenyewe kwa kiwango kikubwa sana. Hata hapo serikali ya awamu ya 5 ilipositisha makinikia hata wazungu hawakubisha kabisa sababu walijua walikuta mwenyewe kalala na sasa kaamka!!!! Inatia hasira sana, hata kama ningekuwa mimi Magu ningesitisha mikataba yote kwanza tuanze moja sio sababu ya chuki binafsi au kupinga maendeleo lakini tu kwa kujifunza kutokana na makossa mengi yaliyofanyika nyuma. Nafikiri imefika mahali haswa WaTanzania tuamkeni na kuchunguza Zaidi nini kinachoendelea badala ya kuwa wepesi kutoa maoni kuhusu masuala muhimu ya nchi bila kuzingatia maslahi mapana ya nchi. Hebu uliza majirani zetu wa Kenya hapo ambao kuna Mabepari wa Kiingereza walimilikishwa Ardhi toka Enzi ya Baba wa Taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyata wanavyonyanyasika. Tusiwe na tamaa ya mambo makubwa kama uwezo wetu mdogo bado ni bora tukaangalia namna ya kujizatiti kiweledi kuongeza uwezo wetu kujenga nchi yetu kwa kutumia akili na rasilimali zetu kuliko kurukia hawa wakezaji halafu majuto ikawa mjukuu.
 
Back
Top Bottom