Sikukuu ya wana-jf

GABLLE

Member
Jan 29, 2011
59
7
Napenda kutoa ushauri kwa wanaJF kuwa, ni vyema tukawa na sikukuu yetu ambayo pamoja na mambo mengine itatoa tathmini kuhusu michango mbalimbali inayotolewa na mbember wa JF. Pawepo pia na mshindi ambaye atakuwa amechangia kuliko wachangiaji wengine wote. Hili ni wazo langu. Wenzangu nanyi mwasemaje??????
 
Ni wazo zuri na kuweza kujuwa na kujadili pamoja matatizo yanayoikumba JF, ila natumaini ujumbe umefika kwa walengwa ni vyema tukasubili maoni zaidi.
 
Napenda kutoa ushauri kwa wanaJF kuwa, ni vyema tukawa na sikukuu yetu ambayo pamoja na mambo mengine itatoa tathmini kuhusu michango mbalimbali inayotolewa na mbember wa JF. Pawepo pia na mshindi ambaye atakuwa amechangia kuliko wachangiaji wengine wote. Hili ni wazo langu. Wenzangu nanyi mwasemaje??????
kwanza KARIBU JF
SIkuku yetu ni bora tuifanyie humuhumu kwenye jukwaa-maana members wa JF wapo all over the world-wakiwa busy na mihangaiko ya kila siku-so kuwakutanisha itakuwa ni ndoto-ni bora ifanyike humuhumu kwenye forum-na ingekuwa vizuri ifanyike siku ambayo ni siku ya birthday ya JF
 
MODS:
Kwanza, Hii thread ilitakiwa kuwa kwenye habari mchanganyiko

Pili, Siyo kuchangia tu kuliko wote bali iwe constructive contributions katika maada mbalimbali zilizotolewa katika majukwaa excluding jukwaa la wakubwa, chart etc
 
big up sana ndg yangu...yani hapo ndo tutajua kama JF inasaidia au vp...tutapata muda wa kufahamiana zaidi na kubadilishana mawazo...i lyk ur thinking capacity....tupo pamoja:drum:
 
Siungi mkono hoja, tafadhali....
Sherehe ifanyike humuhumu kama alivyosema Ed Teller...... kama kuchangia JF Invisible ametoa muongozo!
 
Napenda kutoa ushauri kwa wanaJF kuwa, ni vyema tukawa na sikukuu yetu ambayo pamoja na mambo mengine itatoa tathmini kuhusu michango mbalimbali inayotolewa na mbember wa JF. Pawepo pia na mshindi ambaye atakuwa amechangia kuliko wachangiaji wengine wote. Hili ni wazo langu. Wenzangu nanyi mwasemaje??????
Ni wazo zuri lisilo weza kutekelezeka......
 
Maoni ya wadau ni mazuri. Kwa kuwa Wana-JF wapo dunia nzima tunawezafanya kwa kila eneo then baada ya kupata data kutoka kila sehemu duniani ndo tukajua BINGWA wa JF ni kutoka nchi fulani. Kwa BIG BROTHER inakuwaje?? Mtandao haungopi. Wanaotumoredeti nao ni rahisi sana kupata data zetu.
 
we sema aanzihse forums ya siku ya jf na sio kukutana maana watasema tunampango wa kupundua nchi kwani ukisoma post zingine zinakuonesha kabisa kuna watu wametumwa..
 
issue siyo kukutana. Kubwa ni kumpata mshindi wa JF. Sisemi kupambanisha kama Bongo star.
 
Nahisi humu ndani watu wanogopa kukutana, inawezekana wake na waume tuko humu lakini hatujui kuwa ni wake au waume zetu. Nasharui kila sehemu ifanye kivyake, tulioko dar tupange tukutane ufukweni mwa bahari ya hindi tucheze michezo yote mpaka ya baba na mama! (joke) wanaojua kuimba, kukimbia, kucheza mipira aina zote tucheze.

Wenye hofu na usalama wao wasije sisi tusio na mipaka tukutane. walioko nchi za nje basi nao wafanye hivyo hivyo matokeo tutapewa na mod.

Nawasilisha.
 
Hapa hapa jamvini kila kitu kinafanyika!! mbona huwa tunakuwaga na online meeting?

Its good idea,
Ila kila jukwaa napendekeza liwe na siku yake maalumu au hata wiki yake maalumu, yaani wiiki nzima tunaelekeza kipaumbele/nguvu zote kwenye jukwaa hilo husika. Mfano: Kama ni siasa basi inaweza fanyika wiki ya kwanza ya mwezi october, au elimu wiki ya kwanza ya mwezi january kila mwaka na mwisho wa siku tutacompile report na kuwapelekea wahusika kwa Email/Barua/DHL/UPS or whatever way zinazoweza kuwafikia na kuyafanyia kazi. Ni mawazo mazuri, Hope MODS watayafanyia kazi!!
 
Back
Top Bottom