Heri Ya Sikukuu Ya Christmass Wana JF

90sgeneration

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
275
375
Niwatakie Sikukuu njema wana Jf wote, wa dini zote, kabila zote na race zote.

Jesus Christ akawe faraja katika maisha ya kila mmoja wetu, kila alie na hitaji basi Mungu akatupatie tunavyohitaji, alie na njaa akapate chakula, asie na makazi akapate makazi, asie na kazi akapate kazi, anaehitaji kupanda cheo au daraja akafanikiwe, alie na biashara ikaimarike, alie na kampuni ikafanikiwe zaidi, alie mkulima akavune extra, alie masomoni akafaulu masomo yake, asie na mtoto akapate uzao, alie mgonjwa akaponywe magonjwa yake, asie na furaha Mungu akampe kimfurahichacho na mengine yote yaliyo mema tuyaombayo.

Kwa kuwa ni sherehe ya kuzaliwa Yesu Kristo, basi akawe baraka katika maisha yetu sote wana JF, akawe mlinzi, mbariki na mponyaji, ukawe mwaka wenye heri na faraja na furaha ya mafanikio, kila tuliombalo likapate kua. In Jesus Name Amen.

Cha muhimu ndugu zangu
*Ikiwa jirani yako ana shida na iko ndani ya uwezo wako kumsaidia, basi roho yako ikifurahi msaidie.

*Kama mtu amekukosea , tafadhari tusameheane, tusiwatwishe mizigo na kuwakosesha baraka waliotukosea, tuanze upya na mioyo isio na kinyongo wala hasira kwa watu wengine.

*Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao ikiwa iko katika uwezo wako kuyafanya.

*Usiingie nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi isiwe too much, asije akakuchoka na kukuchukia.

*Tusikate tamaa in every situation, wakati mwingine ni ngumu sana kibinadamu, lakini may this christmass create new hope to you and me.
*Tuwe karibu na familia zetu zaidi na tusiwahau wenye mahitaji panapo nafasi.
*Chaoa kazi (kwa wenye kazi) kwa nguvu zaidi, na kwa malengo makubwa na kwa mbinu zilizo na faida na kwa ufanisi na Mungu akukutanishe na fursa kila wakati.

Amen Mbarikiwe, pia alie na connection ya ajira muwe mnapitia pitia post zetu tunaotafuta kazi yoyote hata vibarua, mnatushika mkono na mnakua mmetuokoa.
 
Brian Decon... "Yesu" wa wakristo
Screenshot_20221225-010551.jpg
 
Amina! 🙏

Ukiona mpaka Mohamed Salah (among of devoted muslims in the world) ametuunga mkono! Hakika tunafarijika. Maana Dunia inatakiwa iende kwa mfumo huu, wa kuishi kama ndugu.
 
Niwatakie Sikukuu njema wana Jf wote, wa dini zote, kabila zote na race zote.

Jesus Christ akawe faraja katika maisha ya kila mmoja wetu, kila alie na hitaji basi Mungu akatupatie tunavyohitaji, alie na njaa akapate chakula, asie na makazi akapate makazi, asie na kazi akapate kazi, anaehitaji kupanda cheo au daraja akafanikiwe, alie na biashara ikaimarike, alie na kampuni ikafanikiwe zaidi, alie mkulima akavune extra, alie masomoni akafaulu masomo yake, asie na mtoto akapate uzao, alie mgonjwa akaponywe magonjwa yake, asie na furaha Mungu akampe kimfurahichacho na mengine yote yaliyo mema tuyaombayo.

Kwa kuwa ni sherehe ya kuzaliwa Yesu Kristo, basi akawe baraka katika maisha yetu sote wana JF, akawe mlinzi, mbariki na mponyaji, ukawe mwaka wenye heri na faraja na furaha ya mafanikio, kila tuliombalo likapate kua. In Jesus Name Amen.

Cha muhimu ndugu zangu
*Ikiwa jirani yako ana shida na iko ndani ya uwezo wako kumsaidia, basi roho yako ikifurahi msaidie.

*Kama mtu amekukosea , tafadhari tusameheane, tusiwatwishe mizigo na kuwakosesha baraka waliotukosea, tuanze upya na mioyo isio na kinyongo wala hasira kwa watu wengine.

*Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao ikiwa iko katika uwezo wako kuyafanya.

*Usiingie nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi isiwe too much, asije akakuchoka na kukuchukia.

*Tusikate tamaa in every situation, wakati mwingine ni ngumu sana kibinadamu, lakini may this christmass create new hope to you and me.
*Tuwe karibu na familia zetu zaidi na tusiwahau wenye mahitaji panapo nafasi.
*Chaoa kazi (kwa wenye kazi) kwa nguvu zaidi, na kwa malengo makubwa na kwa mbinu zilizo na faida na kwa ufanisi na Mungu akukutanishe na fursa kila wakati.

Amen Mbarikiwe, pia alie na connection ya ajira muwe mnapitia pitia post zetu tunaotafuta kazi yoyote hata vibarua, mnatushika mkono na mnakua mmetuokoa.
".........kila alie na hitaji basi Mungu akatupatie tunavyohitaji, ............"
Naongezea tu kwenye sentensi iliyonukuliwa hapo juu ⬆️ kwa wakati unaofaa
 
Brian Decon... "Yesu" wa wakristo
View attachment 2457199
Mkuu , mbona huyu Brian Decon ni mtu kama wewe au mimi aliyeigiza filamu (kwa malipo/contract) na wala hana uhusiano wowote na Yesu wa Nazareti? Je, umependa kutufurahisha sikukuu hii Dec,2022 kwa kutuonesha kwamba ww hujui tofauti au kutofautisha kati ya muigizaji-msanii na mtu-mhusika halisi? Haya bhana tumeisoma komenti yako ili nawe ufurahi pia.
Ila Nijuavyo mimi ni kwamba watoto wa mama mdogo wana hasira sana.
 
Back
Top Bottom