Siku ya Madai ya Maji; nini cha kufanya?

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Tarehe 22 Machi ni siku ya kimataifa ya maji. Ujumbe wa mwaka huu hapa nchini ni "Maji na Usalama wa Chakula", hata hivyo tunahimizwa kuutafakari ujumbe mpya bila kuelezwa matokeo ya ujumbe wa mwaka mmoja uliopita wa "Maji kwa ajili ya Miji: Kukabiliana na changamoto mbalimbali mijini".

Kazi ya wabunge na bunge kwa mujibu wa katiba ibara ya 63 ni kuwawakilisha wananchi na kuisimamia serikali na mamlaka zake katika kuwezesha maendeleo kwa kutumia rasilimali za umma na za wadau wengine.

Kwa nafasi hiyo natoa mwito kwa wananchi wa Jimbo la Ubungo na wa Jiji la Dar es salaam kwa ujumla kwamba badala ya kuadhimisha siku ya bila ya maji kila mmoja ashiriki kwa namna mbalimbali katika Siku ya Madai ya Maji.

Kila mmoja anaweza kushiriki katika siku hii ya madai ya maji kwa njia mbalimbali, njia mojawapo ambayo natoa mwito kwa wananchi wa Jimbo la Ubungo kuitumia ni kushiriki madai ya maji kupitia mitandao ya kijamii kwa kuandika barua pepe kwa bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) kuitaka ifanye kazi ipasavyo ya kuharakisha upatikanaji wa maji kwa mujibu wa sheria, kanuni, mipango na mikataba.

Waandikie wajumbe wa bodi ya DAWASA madai ambayo unataka wayafanyie kazi katika eneo lako na nakala ya barua pepe hiyo kuituma kwa
mbungeubungo@gmail.com kwa ajili za hatua zaidi za kibunge za uwakilishi na usimamizi.

Bodi ya DAWASA ni kama ifuatavyo:
Mwenyekiti Dr. Hawa E. Sinare(e.sinare@rexattorneys.co.tz), Makamu Mwenyekiti-Alhaj Said H. El-Maamry-elmaamry@cats-net.com, wajumbe: Bw. Laston Msongole (lmsongole@mof.go.tz), Bi. Mary Mbowe (mrymboowe@yahoo.co.uk) , Bi. Christine Kilindu(christinekilindu@cti.co.tz), Bw. Daniel Machemba (dmachemba@tccia.com, dmachemba@gmail.com), Alhaj Bakari Kingobi (brmkingobi@yahoo.com), . Mary G. Musira(drtc@cats-net.com), B. Florence S. Yamat (yamatf@dawasa.co.tz), Mh. Amina N. Mkilagi (Mb), Mhandisi. Archard Mutalemwa-Afisa Mtendaji Mkuu (dawasaceo@dawasa.co.tz).

Tuungane pamoja kutaka serikali kuu na serikali za mitaa zitumie siku hii kutoa maelezo kwa umma kuhusu hatua iliyofikiwa katika kutekeleza miradi ya maji na pia kuharakisha uzinduzi wa miradi ilicheleweshwa.

Njia hii ya kuunganisha nguvu ya umma kwa kutumia TEHAMA (sms, facebook, twitter, email na njia nyingine) tuliitumia tarehe 1 Disemba 2011 wakati wa kuhamasisha umma kushiriki mkutano wa wadau uliotishwa na EWURA kuhusu ombi la TANESCO kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa 155% (zaidi ya mara tatu ya bei iliyokuwepo). Hatimaye umeme ulipandishwa lakini si kwa kiwango hicho cha awali bali kwa wastani wa 40% kwa kuzingatia pia viwango vya utumiaji.

Mtakumbuka kwamba Machi Mosi 2012 niliungana na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) katika kata saba Jimboni Ubungo kwenye kazi za kuboresha upatikanaji wa maji.

Tarehe 2 Machi 2012 nilifanya mkutano na wanahabari na kutaka hatua za ziada kuchukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) na Wizara ya Maji.

Nashukuru kwa hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa na DAWASCO na EWURA katika masuala kadhaa; hata hivyo sijaridhika na namna ambavyo DAWASA na Wizara ya Maji wanavyoshughulikia masuala ya maji katika maeneo mengi; hivyo wiki ya madai ya maji kupitia mitandao ya kijamii itumike kuongeza msukumo wa umma kabla ya kuchukua hatua zaidi za kibunge katika Mkutano wa Saba wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 10 Aprili 2012. Zipo kazi ambazo tutazifanya siku ya tarehe 22 Machi na zingine 23 Machi; kwa maelezo zaidi kuhusu maeneo mahususi unaweza kurejea:http://mnyika.blogspot.com/2012/03/wiki-ya-madai-ya-maji.html , naomba tuendelee kushirikiana. Umoja ni Nguvu.
 

Kazi ya wabunge na bunge kwa mujibu wa katiba ibara ya 63 ni kuwawakilisha wananchi na kuisimamia serikali na mamlaka zake katika kuwezesha maendeleo kwa kutumia rasilimali za umma na za wadau wengine.
..

Mh. John, tatizo la maji pia linaweza kupungua kwa kuwaelimisha wananchi na kutoa msukumo namna ya kuvuna na kuyahifadhi maji ya mvua. Tufike mahali teknolojia rahisi kama hii iwafikie wananchi wetu kwa kutoa elimu mwanana na kuipa msukumo wa kutosha, hata wa kisera, ili badala ya wananchi kuhangaika na maji hata wakati wa mafuriko, waweze kuvuna na kuhifadhi maji kwa kiwango kikubwa.

Tuone umuhimu wa kuwa na miundombinu ya kuvuna na kuhifadhi maji kama tunavyoona umuhimu wa kuhifadhi nafaka.

Tuko pamoja mkuu.
 
Tarehe Bodi ya DAWASA ni kama ifuatavyo: Mwenyekiti Dr. Hawa E. Sinare(e.sinare@rexattorneys.co.tz), Makamu Mwenyekiti-Alhaj Said H. El-Maamry-elmaamry@cats-net.com, wajumbe: Bw. Laston Msongole (lmsongole@mof.go.tz), Bi. Mary Mbowe (mrymboowe@yahoo.co.uk) , Bi. Christine Kilindu(christinekilindu@cti.co.tz), Bw. Daniel Machemba (dmachemba@tccia.com, dmachemba@gmail.com), Alhaj Bakari Kingobi (brmkingobi@yahoo.com), . Mary G. Musira(drtc@cats-net.com), B. Florence S. Yamat (yamatf@dawasa.co.tz), Mh. Amina N. Mkilagi (Mb), Mhandisi. Archard Mutalemwa-Afisa Mtendaji Mkuu (dawasaceo@dawasa.co.tz).

kwa maelezo zaidi kuhusu maeneo mahususi unaweza kurejea:http://mnyika.blogspot.com/2012/03/wiki-ya-madai-ya-maji.html , naomba tuendelee kushirikiana. Umoja ni Nguvu.

Hivi huyu Hawa Sinare si ndio yule Wakili anayetuhumiwa kula pande mbili Dowans na TANESCO na kuisababisha hasara serikali? Hivi fedha zetu za maji ziko salama kweli kwenye bodi ambayo anaisimamia kama mwenyekiti? Makamu wake Alhaji Said El-Maamary naye si namsikia tu kwenye masuala ya soka CAF na kwingineko? Ana uhusiano gani na masuala la maji?

serayamajimbo
 
kazi nzuri mh mb kuwakumbusha wadau juu ya wiki ya maji na hatua ulizofikia pamoja na nini kifanyike kutatua kero za maji kwa wadau kutuma kero zao kwa mamlaka husika. KITAIFA WIKI YA MAJI INAFANYIKA IRINGA NAONA WENYE NCHI WAMELAZIMISHA KUUCHAFUA MJI KWA VITAMBAA VYA KIJANI VYENYE JEMBE+,KISA MKULU NA WATU WAKE WATAKUJA ZNDUA HII PROGRAMA.kila kitu kimewekwa kisiasa sijui kama tutatua tatiyo la maji kwa stail h?i
 
Hivi huyu Hawa Sinare si ndio yule Wakili anayetuhumiwa kula pande mbili Dowans na TANESCO na kuisababisha hasara serikali? Hivi fedha zetu za maji ziko salama kweli kwenye bodi ambayo anaisimamia kama mwenyekiti? Makamu wake Alhaji Said El-Maamary naye si namsikia tu kwenye masuala ya soka CAF na kwingineko? Ana uhusiano gani na masuala la maji?

serayamajimbo

Pia Alhaj Bakari Kingobi si ndio mtuhumiwa mkuu katika kashafa ya UDA, alikuw andiye mkurugenzi wa Jiji. Kwa jali hii bodi ya DAWASA imejaa mafisadi hatuwezi kupata maji hata siku moja.
 
  1. Umeme ukikatika watu watawasha Mshumaa au taa ya chemli
  2. Usafiri wa daladala ukikosekana mtu anaweza kusafiri kwa miguu
  3. Je, Maji yakikatika nini itakuwa mbadala wa maji?

TAFAKARI CHUKUA HATUA!
 
Mh Mb leo nilikusika katika kipindi cha Super Mix umedai kuwa matatizo ya umeme pia yana mchango mkubwa sana katika ukosefu wa maji. Naomba kuuliza nini kinakwamisha players wengine kuingizwa katika uzalishaji na usambazaji wa umeme ikiwa Sheria ya Umeme ya 2008 inaondoa ukiritimba wa Tanesco katika sekta ya umeme. Naamabatanisha sheria ya umee kwa wale wanaotaka kujielimisha kwa lengo la kushinikiza Serikali iondoe ukiritimba wa Tanzesco tupate huduma kama tunazopata katika mawasiliano k.m simu.

View attachment ELECTRICITY ACT, 2008.pdf
 
Pia Alhaj Bakari Kingobi si ndio mtuhumiwa mkuu katika kashafa ya UDA, alikuw andiye mkurugenzi wa Jiji. Kwa jali hii bodi ya DAWASA imejaa mafisadi hatuwezi kupata maji hata siku moja.

Umekumbusha kitu kizuri, sasa hii bodi ya DAWASA kama ina watu wa namna hiyo wataweza kweli kuisimamia DAWASCO? Nani anamjua mjumbe mwingine wa hiyo bodi na ufanisi wake?

serayamajimbo
 
kazi nzuri mh mb kuwakumbusha wadau juu ya wiki ya maji na hatua ulizofikia pamoja na nini kifanyike kutatua kero za maji kwa wadau kutuma kero zao kwa mamlaka husika. KITAIFA WIKI YA MAJI INAFANYIKA IRINGA NAONA WENYE NCHI WAMELAZIMISHA KUUCHAFUA MJI KWA VITAMBAA VYA KIJANI VYENYE JEMBE+,KISA MKULU NA WATU WAKE WATAKUJA ZNDUA HII PROGRAMA.kila kitu kimewekwa kisiasa sijui kama tutatua tatiyo la maji kwa stail h?i

Sasa watueleze maadhimisho ya siku ya maji nini kimefuata?

serayamajimbo
 
Back
Top Bottom