Siku JK atakapo kuwa wingu mgao utaisha

Nafikiri ndo tunachosubiri awe wingu then maji yamiminike mtera baada ya hapo shida ya umeme kwisha. Source :jk mwenyewe!

Ni kweli, maana kadai kuna ukame, na umeme wetu wa sasa unategemea maji.
Wacha abadilike awe wingu tu, umeme kwa sasa unatukera mno!
Ila wakuu, ina maana kama kweli mkuu wa kaya angekua kalifungua kibwebwe hili na la DAWASCO, nadhani mpaka sasa
tusingekua tunamponda ivi, ndio maana watu wanapiga kelele kuwa hayo masafari yake yanamfanya kutokujua
shida zetu wananchi, ila watu wa karibu ndio naona ndio kwanza wanachekelea wakisikia kuna vi trip, hakuna wa kumshauri
vinginevyo, hii mbaya sana kwa kumharibia mkuu wetu!
 
Majibu ya kebehi toka kwa rais wa nchi ni hatari sana !

Nafikiri hata Nyumbani kwake huwa haeshimiki kwa majibu yake ya Kijinga. Kama ndio ingekuwa baba yangu nafikiri ningemchapa viboko au ningeamua kumpeleka hospital kuangalia kama yupo sawa au anahitaji msaada, na ningemshauri ajiuzulu mara moja kwa kuwa ameshindwa kuiongoza familia je nchi itakuwaje? Kwani hata kwenye familia yake pia huwa anamajibu ya kuudhi
 
Hivi ile "mvua ya Lowasa" iliishia wapi? Au kwa sababu yeye sio PM tena na kwa hiyo hana mamlaka ya kwenda kuitafuta?
 
haha// mimi naomba niwe jua.. nimmulike aondoke zake

Wala asisikike tena katika anga za siasa za Tanzania. Kama sio ule "utamaduni" wa magamba wa kuachiana kuwepo madarakani kwa miaka 10 basi Watanzania tungemshasahau maana kulikuwepo ushahidi wa kutosha kabisa kwamba Kikwete hana sifa yoyote ile ya uongozi na alishashindwa siku nyingi kama Rais wa Tanzania hivyo asingestahili kugombea tena 2010.
 
Rais anaongea utazani hakuomba kura bana ,au kwasababu anaondoka ,this poor president sucks a lot.
 
Back
Top Bottom