Siku hizi Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wanateta Serikali na kuweka pembeni maslahi ya Wafanyakazi

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,975
3,334
Asalaam Aleykum.

Kwa kweli kama kuna watu wana maisha magumu nchi hii, basi ni wafanyakazi. Wengi wao mishahara haijapanda kwa muda mrefu huku gharama za maisha zikipaa kila siku na viongozi wao wa vyama vya wafanyakazi wapo wapo tu kazi kuiba michango ya wafanyakazi wenzao wanayokatwa kila mwezi kwenda kwenye vyama husika!

Nchi yetu kuna wafanyakazi wanakatwa karibu 50% ya mishahara yao kama kodi (PAYE), Mifuko ya hifadhi ya jamii, nhif, loan board, n.k. Mwisho wa siku wengi wanalazimika kukopa na kukooa ili kuendesha maisha ya familia zao.

Bahati mbaya sana vyama hivi vya kitapeli ni lazima kujiunga navyo, lakini vinginevyo visingepata Wanachama kwa maana hakuna jambo la msingi wanafanya ambalo kwa sehemu kubwa ni kutetea maslahi ya wafanyakazi wenzao.

Anyway, ngoja waendelee kujineemesha wao binafsi maana hata hivyo wafanyakazi wengi nchi hii ni kana kwamba hawajielewi. Yaani wapo wapo tu!
 
Nguvu Iko hapa buanaaaa
 

Attachments

  • Screenshot_20240430-231904.png
    Screenshot_20240430-231904.png
    288.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom