Siku hizi hakuna muoaji wala muolewaji, wote matapeli tu

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
HAKUNA WA KUOA WALA KUOLEWA SIKU HIZI WENGI WABABAISHAJI NA MATAPELI TU ,WAZAZI MMESAHAU WAJIBU.

Wazazi ,watoto wenu wanaanza ngono na tabia mbovu za kishetani wakiwa bado wadogo je mnalitambua hilo au ndio bado mnaamini katika BORA MAISHA NA SIYO MAISHA BORA KWA WATOTO WENU.

Mtakuja kuzuia ndoaa za utotoni ,mimba ya utotoni,watoto wa utotoni ,watoto wasiokuwa na wenyewe ,watoto wasiokuwa na mjomba ,kuvunjika kwa ndoaa ,uchangudoaa ushogaa na upuuzi wote unaofanywa na kizazi cha sasa pale tuu kwamba wazazi mtakapokubali na kutambuaa kwamba watoto wenu huko majumbani mwenu WANAANZA NGONO WAKIWA BADO WADOGO NA KAMA WAZAZI mpo tuu mnayaangaliaa haya yakitokeaa na baadae nyinyi nyinyi wazazi mnaanza kumsingiziaa Sheteni,wengine ohh watoto wa kidigitali,wengine uuhh watoto wa siku hizi hawaambiliki .

kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kusema siku moja kwamba hakuna kitu kinaharibu maisha ya mtu kama NGONO NA POMBE ,mtu yoyote ambaye mambo yake hayaendi ipasavyo asilimia kubwa utagundua kwamba aliendekeza sana NGONO au POMBE, pombe na ngono ni mchawi wa kwanza katika maisha ,vijana wanadogo masikini ya hawa wanakunywa pombe kuliko maji ,wanakunywa pombe kali ambazo hata wazungu wanaziogopa lakini wao wanakunywa kuanzia asubuhi mpaka jioni mwaka mzima ,makosa makubwa kusema watoto hawaambiliki kwani anatakiwa kuwambia na kuwakemea watoto ni nani kama siyo sisi wazazi..??,wazazi mnachangiaa kutokea haya maana mnayafumbiaa macho hamtaki kuyaongea na kuyafichuaa hadharani, chanzo cha yote hayo ni kwamba watoto wenu wanaanza NGONO MAPEMA NA HAMULIONI HILO MNABAKI KUSEMA MWANANGU AMEKUWA MWANANGU SIKU HIZI ANAJITAMBUA .

Ndio maana leo unaona Afrika zaidi ya 70% ni kuanzia miaka 18-45 ,kuanzia miaka 18-35 ni vijana na vijana hao wote hovyo na mzigo maana hawachangii chochote kwa familia zao au kwa taifa ,tutaweza kuilaumu serikali sana lakini wewe kama kijana unakimbilia kuzaa unapaswa kulaumiwa na kunyooshewa kidole maana kabla hujazaa unatakiwa uangalie hali ya uchumi wako ,unatakiwa unaangalia uchumi na mipango ya serikali piaa,vijana wamejaa tamaa tu wanawaza ngono kila wakati na kujikuta wanajaza na wanajazwa mimba kabla ya mda na kuanza kumtafuta mchawi aliyemjaza mimba maana hakumbuki mimba ni ya comred chipomzo au ni ya kijana chapanzi atahangaika apo atakaeingia kingi basi inakula kwake huyo ndio ataitwa baba hata kama alipiga ONE NIGHT STAND..!!.

Wazazi tambueni watoto wenu wanaanza ngono mapema sana ni vyema kama amkachukua hatua mapema siyo kila siku mnapiga kelele wakati vijana wenu wanaanza wakiwa majumbani kwenu ,watoto wadogo wanaweka stutus WANAUME WOTE NG'OMBE TU hamjiulizi na nyie kama wazazi mnaangaliaa tu ndio maana yake nini..??Watoto wa kiume wanaweka stutus za videmu vyao Kwamba THE NIGHT WAS GOOD uku ameweka na picha mtoto mwenzake ,wazazi mnaangalia huu upuuzi unafanywa na vijana wanapost matumbo yako nje ,makalio wamebinuaa ,midomo na nyusi wameweka mitalo mapaja yanag'aa utafikiri yapo buchani , wazazi mnasema mwanangu amekuwa amekuwa au amejiuwa uuh amekuwa au amekorogeka ,siyo vibaya watoto wenu wakikuaa lakini hakikisheni wanakuaa kiuchumi pia ,wanakua kimaadili piaa ,hakikisheni watoto wenu wanakuwa na hofu ya Mungu piaa ,

Mimba za utotoni ni nyingi sana ukizunguka nchi nzima kuna baadhi ya mikoa kunatisha sana naweza kusema hali ni mbaya uko mikoani ,watoto wamewazaa watoto,watu wanazaa pasipo kuangalia hali yake ya kichumi ,wanazaa pasipo kukomaa akili,wao wanajua kuweka miguu juu na macho ndio mwisho wa maisha wanajisahau kwamba WANAPOSIKIA UTAMU NDIO MIMBA INAPOINGIA,na mnapozaa hao watoto mnawaandalia nini katika maisha yao ya baadae ,mimi na wewe tukifa watoto tunawaachia nini.??Elimu mnayowapa watoto wenu uko shuleni haitoshi maana elimu yenyewe hii ni ya kizamani haiendani na wakati hivyo kama wazazi tunajukumu kubwa la kuhakikisha mtoto anatambuaa yeye ni nani na anatakiwa kufanya kitu gani,wewe ni profesa ndio lakini ukifa unakufa na uprofesa wako maana vyeti vyako vinakuwa havina maana kwa watoto wako,wewe ni doctor lakini ukifa watoto hawatakula odoctor wako maana wewe kuwa doctor ,waandaeni watoto wenu namna ya kuishi vyema na namna ya kujitegemea kiakili ,wakumbusheni pia kwa MUNGU HAWEZI KUKUPA VYOTE hivyo wasipende kulazimisha sana mambo mengine lasivyo yatawatokea mdomoni.

Wazazi mnataka nani alaaumiwe kwa tabiaa mbovu na kishetani kwa vijana wenu ,mnakaa na watoto ndani ambao ni vibaka ,malaya ,machungudoa ,wavuta bangi ,matapeli wengine madanga waliokomaa mjini na mnayajuaa hayaa lakini mnawaogopa kuwakemea hadharani mnabaki kuwaambiaa kwamba watajua wenyewe ,mtoto ni mtoto tu kwa wazazi atajuaje mwenyewe ,naamini hakuna mzazi alitepanga kuzaa vibaka na malaya ,mliwazaa watoto wenu kwa lengo la kuja kuwa rai wema na kwa faida ya maisha yao na familia kwa ujumla wake ,kama mtoto wako ana miaka 25-27 bado yupo nyumbani ujue wewe mzazi umechangia 70% kwa mtoto wako kuwa ivoo na ndiyo maana mwisho wa mnapigwa makofi na watoto wenu wenyewe ,mnatukanwa matusi makubwa tena matusi ya shimoni na watoto wenu mnadharaulika kwa sababu yote hayo ni malezi ya makusudi tena mabovuu ,mtoto ana miaka 8 anafanya mambo ya kijinga mnasema muache bado mdogo,mtoto ana miaka 16 anafanya upuuzi anarudi usiku hata kupika hapiki baba anajaribu kuja juu au kumtembezea kichapo mama anamwambia mme wake kwamba utamuuzia mwanangu ati akikua ataacha nani amekwambia ataacha huwa hawaachagi hao ,tena wakina mama huwa mnaaribu sana watoto wenu sana kwa sababu mnatanguliza huruma mbele badala ya kuwanyoosha watoto wenu.

TUWAKUMBUSHE WATOTO WETU KWAMBA THERE IS NO FREE LUNCH ON EARTH ,akila cha mtu awe tayari kuliwa pia ,akimnyanyasa mtu awe tayari kunyanyaswa piaa,akipiga mtu awe tayari kupigwa pia,msiwaafiche chochote bali endelee kuwaambia kwamba Duniani hakuna cha bure kila kitu kinalipiwa,wakumbusheni kwamba wasione vinapendeza vinawenyewe wamevitolea jasho ,Watengenezeni kuwa watafutaji na kuwa SMART WORKERS NA SIYO HARD WORKERS ,wakumbusheni kwamba DUNIANI NI MAPAMBANO KUNA KUSHINDWA NA KUNISHINDA PIA jitahidini kuwapa watoto wenu ukweli zaidi kuliko kuwadanganya na watambue kwamba hakuna cha bure katika hii dunia ,kamaa wazazi ni vyema pia mkawakumbusha pia kwamba dunia hii hakuna mtu mzuri na hakuna mtu mbaya na hakuna mtu mbaya na hakuna mtu mzuri pia, ila hapo hapo watambue kwamba MZURI MUNGU PEKEE.

Wakumbusheni watoto wenu sio tu mnakaa sebuleni kuangalia Bongo movie na tatu mzuka ,wakumbusheni kwamba URODA WA USIKU MMOJA UNAWEZA UKAWAFANYA WAJUTE MAISHA YAO YOTE ,waambie katika hii dunia kuna machungu mengi na raha nyingi pia lakini endeleeni kuwakumbusha vijana wenu wanao anzaa ngono wakiwa bado makinda kwamba ANAPOONA UTAMU AJUE UCHUNGU UNAFUATA ,msikae kimya kama wazazi ,hamtakiwi kuwaonea haya watoto wenu pale wanapofanya mambo ya kipumbavu ,na msiogope kuwafunda na kuwapa kipigo kisa mliwazaa kwa uchungu ,msiwanyime watoto wenu mapigo ,ambayo yatawasaidia wanapokuwa wakubwa ,waambieni watoto wengu uhalisia wa maisha jinsi yalivyo ,wambieni watoto wenu kwamba steam zimelipiwa mjini wakizingua wamenasa ,acheni kuwapaka matope watoto kwamba ukishakuwa mwafrika basi ni kupambana mwanzo mwisho maana hakuna mteremko.

wewe unapiga mahesabu ooh nataka kuwa na watoto 3 au 7 hivi hao watoto saba utawalea katika maadili na malezi mema.?tafakuri je utakuwa na mda wa kutosha wa kukaa na watoto wako?mnatamani kuzaa lakini hamjui kulea na hamna Elimu yoyote ile juu ya malezi ya mtoto wenu ,ndiyo mnajikutaa mmezaa watoto wengi lakini ni UNPRODUCTIVE, Kuna mambo mengi sana watu hawajui na tumeendelea kuwa hivyoo hatujui ,TULIO WENGI TUNAJUA KUZAA SANA LAKINI HATUJUI KULEA ,watu wanazaa lakini kulea hovyo ,kuna tabiaa ya watu wanakwambia we zaa tuu KULEA ATALEA MUNGU ,uzae wewe afu kumkuza na kulea atalea Mungu kweli ARE YOU CRAZY..?na wewe kama mzazi mnafanya kazi gani mpaka umuachie MUNGU,mnajisikiaa faraja pale mnapokuwa mmezungukwa na watoto wengi majumbani mwenu kidai mnakuza ukoo ,ndio nakubaliana kwamba mnakuza lakini kumbuka unakuza uko wa KIPUMBAVU kama hamtawaandalia watoto wenu maisha mema na kuwalea vyema .

siku hizi ukienda majumbani huko vijana wadogo tayari wana wajukuu ,vijana wanamiaka 38-45 tayari wameshapata wajukuu,kwa nini basi yote hayo. kwa sababu watoto wenu wanaanza Ngono mapema na mnawaangaliaa tu ,watoto wa kike na wakiume wanaanza Ngono wakiwa wadogo na nyie kama wazazi mmeganda kama sumaki mnaangalia tu na wengine kwa akili zao mfu utawasikia wanakwambia MTOTO WANGU AMEKUWA ,mtoto wako amekuwa ndio lakini mpuuzi na ajitambui ,Wazazi ni wajibu wenu kuwachunga na kuwalinda vina wenu katika maisha yenye kumpendeza Mungu kwa faida ya Taifa na familia zao kwa Ujumla.

Tare 13\06\2018 nilipita Dodoma na baadae Iringa nikashangazwa baada ya kuona watoto wenye umri kuanzia miaka 10 mpaka 15 majira ya saa 5 usiku wanacheza pooltable ,wengine wamelewa wengine walala ovyoo mjini DODOMA ,wazazi mko wapi..??mnafanya nini...?tatizo mnajiandaa kuzaa vibaka ,mnajianda kuzaa majambazi ,mnajianda kuzaa watoto wa mitaani wenyewe maana wengine mnazaa mnawaachie bibi zenu au mama zenu ,ukija Mbeya uku wanyakyusa wamezaa sana kupita maaelezo lakini watoto wengi hawawajui hata baba zao ,mnazaa wato wengi kwa sababu kwenu mpo wengi ,mnazaa bila mahesabu mwisho wa siku wanajikuta mmezaa vibaka na mashoga na majambazi huku mtaani afu mnaanza kulaani watoto wenu mliowazaa kwa matumbo yenu wenyewe bila kusahau nyinyi wazazi ndio mnafanya makosa afuu mnalaumu watoto ,hivi mtoto mpaka anakuwa shoga wewe uko wapi..!?mpaka mtoto anakuleta mimba usiyokuwa na baba wala babu wewe kama mzazi ulikuwa wapi..??mpaka mtoto wako mwenyewe anakuwa kibaka wewe uko wapi kama mzazi ,mpaka mtoto anakuwa kahaba aliyekubuhu kamaa mama kama baba ukoo wapi..??

WAZAZI MNAPASWA KUWA MIFANO KWA WATOTO WENU,wazazi walevi watoto walevi ,mzazi anangonoka ovyo watoto nao wanangonoka pia ,mzazi halali ndani anakesha nje kama popo na mtoto naye anakesha nje ,nani atamuelimisha mwenzake katika familia hiyo ,watoto wavuta bange na baba naye mvuta kamba vilevile ,WAZAZI KUMBUKENI MNACHOKIPANDA NDICHO MTAKACHO VUNA ,mnashindwa kuwalea watoto wenu vizuri tayari huyo mtoto umeshamwaribia maisha yake ,ndio maana watoto wengine wanawashushia kipondo wazazi wao ,watoto wengine kulingana ugumu wa maisha wanageuka kuwa PANYA ROAD,wanageuka kuwa NG'OMBE ROAD,wengine wanaenda mbali zaidi wanakuwa MALAYA ROAD na CHANGUDOA ROAD bila kusahahau MADANGA ROAD.Wazazi mmesahau wajibu wenu katika malezi ,mnawaza mambo ya mitandaono mko bize mnakunywa pombe mnasahau kwamba mna watoto ,mko bize na instadrama ,mko bize na facebuku ,mko bize kweli mnalea vitambi mko bize makazini ,hamkubuki kwamba mbali na Elimu mnayowapa watoto wenu piaa mnahitaji kuwalea katika maadili wajuwe kwamba hawakuzaliwa kimiujiza ujiza kimazingaombwe Zingaombwe bali walizaliwa kimakusudi.

msifurahiee watoto wenu kukua miili yao ,msifurahiee watoto wenu kurefukaa na kuongezeka kwa maumbo yaoo mkaona basi mmekuza na mmeleaa vyemaa na kuna wengine mnaenda mbali kudai kwamba ASANTE MUNGU MWANANGU AMEKUWA bila kujua kwamba UMEKUZA MATATIZO NA SIYO MTOTO,amekuwa kimwili lakini tabia mbovuu chafu ,umesomesha lakini tabia hovyo yaani kichefuchefu ,mtoto anazunguka usiku kama kama popo uku wewe unakoroma na mke wako kitandani tena unaota unafukuzwa na vibaka,mtoto wenu yupo nje usiku wa manane atafikiri anataka kupinduaa nchi wazazi mpo tu wala hamkemei haya,wazazi mmekuwa wavivu hata kukemea watoto wenu bali mmekuwa wepesi wa kunywa pombe na kukuza vitambii tenaa wengine ni wafanyakazi bora uko makazini kwenu maana mnachapa kazi kama misukule lakini watoto wako huku nyumbani ni vibaka wengine hawalali ndani usiku kucha wanawanga kwenye makumbi ya starehe wakilewa wanaanza kutukana wakisha landuka masehetani yamepanic utawasikia Ooh DINGI YANGU MKUDA kweli anampenda dogolasi kampeleka shule mimi kanitema ila Hakuna Shida IPO SIKU DINGI NITAMUONYESHA KAMA MIMI NI KIDUME.

Tulikuwa tunashangaa MUSA Kuvuka bahari ya shamu lakini hilo limeonekana kuwa la kawaida sasa ,tulikuwa tunashangaa ongezeko la makanisa uko mbeya lakini nalo la kawaida sasa ,tulishangaa diamond kumuoa zari ila limekuwa la kawaida pia ,tulishangaa kuona mketema anamuacha Ruge lakini ili nalo limepita ,watu hawakuamini Lowasa kuhama cccm lakini hili halina utamu tena kwa sasa ,watoto kutembea uchi na kuvaaa uchi na kulala uchi siyo jambo la kawaida nalo linaonekana la kawaida ,tulishangaa lissu kuchapwa risasi lakini hili Mungu ameliepushia mbali bado tunaendelea na maomnbi ila nalo linaanza kuonekana la kawaida sasa,watoto wadogo wakike wanajichanganya na madingi,watoto wa kiume kuwa mashoga nalo linaonekana kuwa la kawaida sasa,ukifungua tu facebuka unakutana na makalio ya watu,ukifungua tu instagrama unakutana na mapaja na visura vya watu ,watoto wadogo wa kiume wanajichanganya na majimama wengine bibi zao nalo eti limeonekana kuwa la kawaida pia ,na dunia ipo inayaangalia haya mauchafu yanaendelea wengine wanakuambia fasheni ,wanajiuta mamodel au disigner wengine eti wanatafuta umaarufu wengine nao eti ni mavideo vixen wakati ni ukahaba wanafanya sema ukahaba wa kisasa ,taasisi zipo zinaangalia haya yakiendelea tu pia uku wengine wakidai ni usasa ndio maana watoto wadogo wanasasambua na mijibaba na mijimama tatizo liko wapi wazazi wezangu wengi watakimbilia kusema NJAA AU UMASIKINI .

Liko wapi jukumu la wazazi ,liko wapi jukumu la makanisa na misikiti ,watu wazima kizazi kinaoza hiki tunakiangalia tu ,kizazi kinakufa tunakiangaliaa tu,watoto wanageuka kuwa vituko bado tunaangalia tuu ,inamaana jukumu la WAPENI WATOTO WENU MAPIGO pale mnapoona wameenza dalili za Ushetani,waelimisheni kwa lugha kali na nyepesi pale mnapoona hawaendi sawa na matakwa ya kijamii,watoto wenu hawana adabu kabisa wanaliwa na watu wazima ,wanaliwa na vijana wenzao na waliwa na babu zao ,watoto wadogo wanashinda clubing kuanziaa juma tatu mpaka ijumaa na wazazi ndio mnawapa hela za kwenda huko lakini hamfatilii mienendo ya watoto wanapotoka majumbani mwenu, mpo mnawaangaliaa tu tena mnawalipiaa Ada uko mashuleni ,wanavaa vinguo vinaonyesha mapaja yao na sehemu zingine mbaya lakini mnawaangaliaa tu maana wanatokea majumbani mwenu ,zamani hayakuwepo haya,wazee wengi walikua wamefunzwa kuishi vyema na wake zao ,wazee wengi walikuwa wamefunzwa namna ya kuwa viongozi bora katika jamii zao ndio maana julius kambarage nyerere alikufa akiwa masikini wa mali lakini aliyejaa mawazo yakinifu yatakayodumu milele daima,unapomuona Nkwame Nukuruma alikufa masikini lakini Afrika inajivunia kuwahi kuwa na mtu kama yeye,Thomas isodere sankara alikufa akiwa na lakini mbili tu kwenye account yake maana hakuwa na tamaa ya utajiri katika mambo ya kijinga ,WAFUNDISHENI WATOTO WENU KWAMBA STAREHE YA USIKU MMOJA NA MDA MFUPI ITAWAGHARIMU MAISHA YAO YOTE.

tutaendelea .

vuta pumzi kunywa maji mengi mwambie Mungu ikumbuke kazi ya mikono yangu na hiyo kazi ionekane afu acha maisha yaendelee ,deal na maisha yako usideal na watu ,usichukulie vitu so siriaz maana utaumia .Asante sana
 
Doh!..umeandika yote na ni ya ukweli. Kilakitu,si kibovu wala kizuri kimehalalishwa sikuhizi.
Wazazi pitieni muusome huu uzi wote mtapata mengi ya kuwasaidia wanenu pia akili zitafunguka.
Tuliojikwaa tuamke ambao wako imara wamuombe Mungu awawezeshe wasianguke.
Asante kwa somo.
 
Atakae maliza kusoma huu uzi anitag ili nipate samare
Inshort vijana muache ngono na ulevi na upuuzi wote unaofanya mjione wajanja dunia hii.
Waheshim wazazi wako,fanya kazi kwa bidii na pia umtangulize Mungu kwa kila jambo,atakuwezesha kuushinda uovu.
 
Asante mkuu Leo nimepata support kila siku nalia huku wazazi wanaharibu watoto
Leo afadhali nimepata mtu wakushirikiana kulia
Ipo siku isiyo na jina tutalia sote
 
Kama kuslide tu shughuli je kusoma yote c ndo balaa......atakayeisoma yote aniambie maudhui mengine ukiacha pombe na ngono
 
Back
Top Bottom