Elections 2010 Sikia kioja hiki cha TBC..!

inatia hasira sana,ameingia hapa na msafara wa magari ya kifahari,nissan,vx na v8 then anasema elimu na afya bure haiwezekani,anaimba wimbo wa taifa hapa hata uzalendo hana bora asingeimba tu
 
Makumbusho ya taifa ina nafasi, tutauweka pale katika miaka ijayo. Labda lengo la kukimbiza mwenge libadilike. Kwa mafano mwenge uwe wa kufichua mafisadi, wauaji wa albino na vikongwe, I mean mwenge uwe na kazi ya kumulika maharamia na mibaka uchumi la sivyo nafasi ya kuuzima milele ipo!
 
Naangalia tbc hapa. Yaelekea huu ni mkakati wa kumwondoa zitto, ila too late. Halafu hawa halaiki kiboko. Viko gado sijui vimekula nini. Jk mwenyewe pamoja na kukaa anaonekana hoi. Halafu havikosei. Karibu nusu saa sasa vinapiga gwaride
 
Kuanzia sasa tbc wanataka kujiunga na watangazaji waliopo kigoma,kutuletea matangazo ya kuzimwa kwa mwenge na kikwete,hivi hawana taarifa kuwa kuna mdahalo pale nkrumah udsm wenye tija kwa taifa hasa wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu?au ndio wanataka kupiga kampeni kwa kikwete chini ya kivuli cha kuzima mwenge?huko kigoma kuna mjadala au mdahalo gani wa kuupita huo wa hapo udsm?

CCM wanatamani Mtanzania wa leo awe sawa sawa na Mtanzania wa mwaka 47.

Muda jamani! Muda!

Zuia kila kitu! Huwezi kuzuia muda! Muda haurudi nyuma!

DR. SLAA for Life!!!
 
Akili mbaya kabisa...Wanadhani kila mtu anautaka mwenge, wakati hauna maana yoyote, ila njia ya kufilisi nchi!

Kwanza huko kwenye mikesha yao wanachapana kama nini. Wakiamka asubuhi wanahubiri "Ukimwi ni hatari". CCM bwana!!
 
............leo ni public holiday ya kuzimwa mwenge au nyerere? if mwenge then TBC 1 wapo right ila kama ni nyerere TBC1 wataujibu umma muda ukifika. hapo ndio naona washabiki wa CCM si watanzania....kama mwenge ni ishu ya kitaifa hizo t-shirt, kofia na kanga za CCM zilizojaa uwanjani za nini? jaribu kwenda na bendera yako ya CHADEMA au CUF uone utakavyopotezwa uhai wako na Polisi wakishabikia tu!
 
Huo mwenge kila mwaka unachangiwa, kumbe kupalilia matumbo ya CCM na mafisadi wao. TBC hawajajua historia itawasulubu, kila mtu anaona. Tuna uchungu, kodi zetu hizo zinaangamizwa kulipia TBC na Mwenge kumbe wanasaliti taifa kwa maslahi ya Ufidhuli wa kikundi hicho CCM. Watanzania wachukue hatua, hakuna kuangalia TBC, halafu hakuna kutaza kampeni zisizo na dira za CCM. Wabaki na TBC na wawapigie kampeni, wakumbuke Rwanda watawala walivyoponza vyombo vya habari ktk ugomvi wa kimbari! Butiku, Ulimwengu, Azaveli, na wakali wengine, nchi inawategemea. Wapeni raia mustakabali wa ufidhuli huu. HUU NI WIZI, UTAWATOKEA TU PUANI, TUMUOMBW MUNGU ASHUSHE ULIMI WA MOTO KWA HAWA WANAKULA JASHO LA WATANZANIA MASKINI, WAMAMA NA WATOTO WANAOHANGAIKA KILA KUKICHA BILA HUDUMA....WAANGAMIE KAMA KULE SODOMA NA GOMORA, maana utabiri wa Majini wanaoutegemea umeshaonyesha kuwa njia yao ni ile njia pana ielekeayo kuzimu...kwa wafu wa kifikwa na ki-dira. Tunawazika baada ya Oct 31 Slaa atakapowanyesha nchi inaendeshwa namna gani. Ole wao, watakimbiana...
 
Sifa kubwa ya Mwenge ni Kueneza Ukimwi nchi nzima bila kujali rangi, kabila jinsia au Dini
 
jamaa hapa kasha kasirika,hana furaha kabisa,kajawa na hofu,hapa ni anasa tu hakuna kuzzima mwenge wala nini,ni kampeni tu,anasema watu wamejiandaa kuangalia ze comedy
 
Sifa kubwa ya Mwenge ni Kueneza Ukimwi nchi nzima bila kujali rangi, kabila jinsia au Dini

Bora umesema ukweli,mimi nilishwahi kuhudhuria mikesha mara mbili ya Mwenge pale Uvinza,Kigoma. Mara nyingi kuna mkusanyiko mkubwa wa watu,hii inatoa upenyo wa watu kuchapana maeneo ya Gesti,vichochoroni na kwingineko...

Ni suala la kuwa makini sana...
 
Tido Mhando nilikuwa nampenda sana alipokuwa BBC lakini sasa hivi ameonyesha upande wake wa pili! Unaacha kutuletea mdahalo wa Kumbukumbu ya baba wa taifa for the sake of that 'meaningless' mwenge? Come October and God forbid, things might be in order.
Tido umeona demokrasia ya wenzetu lakini kwa ubinafsi umeshindwa kui-import kwetu ili kulinda masilahi yako binafsi at the expense of tax-payers money! Waafrika ndivyo tulivyo.
 
jamani sasa tumezidi kulalamika tuu, hivi kweli wanaweza tu kujipeleka na kuchukua habari pale? hao walioandaa mdahalo walitakiwa watoe mwaliko mbona mwataka kuwaonea? na hata hivyo mewnge kwa tz ni suala la kitaifa, yuko mkuu wa nchi wasiende, nyie mbona hivyo? eti wamwache mwajiri wao na suala la kitaifa siku ya kumuenzi muasisi wa huo mwenge waende mdahaloni. its amazing u know. sometimes we are not realistic just to blame tu.
 
Back
Top Bottom