Elections 2010 Sikia kioja hiki cha TBC..!

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
Kuanzia sasa tbc wanataka kujiunga na watangazaji waliopo kigoma,kutuletea matangazo ya kuzimwa kwa mwenge na kikwete,hivi hawana taarifa kuwa kuna mdahalo pale nkrumah udsm wenye tija kwa taifa hasa wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu?au ndio wanataka kupiga kampeni kwa kikwete chini ya kivuli cha kuzima mwenge?huko kigoma kuna mjadala au mdahalo gani wa kuupita huo wa hapo udsm?
 
huo mwenge tutauweka pale makumbusho.. hauna tija kwa taifa...

Ni wizi tu kwa watu, ila mwaka tunauchangia huku ukifufua na uanzisha miradi ambayo siyo hitaji la muhimu kwa sasa... Mbona haufichui mafisadi??? wezi??????? walarushwa????????
 
Uko UDSM wanajua watu watakuwa wanaiponda CCM na JK in full swing.
Ulimwengu,Butiku,Lwaitama list iyo kali sana CCM wanaweza poteza kura
 
Akili mbaya kabisa...Wanadhani kila mtu anautaka mwenge, wakati hauna maana yoyote, ila njia ya kufilisi nchi!
 
Walijaribu kuuzuia usiwepo kwa kisingizio eti mkandala hayupo na wanafunzi pia hawapo, naomba huu mdahalo leo uwe na tofauti na midahalo yote iliyopita.
 
Huo mwenge kila mwaka unachangiwa, kumbe kupalilia matumbo ya CCM na mafisadi wao. TBC hawajajua historia itawasulubu, kila mtu anaona. Tuna uchungu, kodi zetu hizo zinaangamizwa kulipia TBC na Mwenge kumbe wanasaliti taifa kwa maslahi ya Ufidhuli wa kikundi hicho CCM. Watanzania wachukue hatua, hakuna kuangalia TBC, halafu hakuna kutaza kampeni zisizo na dira za CCM. Wabaki na TBC na wawapigie kampeni, wakumbuke Rwanda watawala walivyoponza vyombo vya habari ktk ugomvi wa kimbari! Butiku, Ulimwengu, Azaveli, na wakali wengine, nchi inawategemea. Wapeni raia mustakabali wa ufidhuli huu.
 
mbio za mwenge zitakuwa ni mradi wa kigogo mmojawapo kwenye kampuni ya mafisadi CHICHIEMU
 
angalia sasa utumbo wao wanaouonyesha,naona hapa watu wamevaa nguo za ccm,msikie hata mtanngazaji anasema tunamsubiria mgombea urais wa ccm ambaye pia nia rais,upupu mtupu
 
huo mwenge tutauweka pale makumbusho.. hauna tija kwa taifa...

Ni wizi tu kwa watu, ila mwaka tunauchangia huku ukifufua na uanzisha miradi ambayo siyo hitaji la muhimu kwa sasa... Mbona haufichui mafisadi??? wezi??????? walarushwa????????
Ni kweli huo mwenge ulitakiwa uwafichue mafisadi na wala rushwa kwasababu unamulika kila mahali wanavyodai wenyewe!
 
Si ataishia kuahidi tu, walaah akianzisha kampeni this time lazima tuingilie kati, hawezi kutumia mwenge ambao tunauchangia wote kwa manufaa yake binafsi.

N.B: Nikiwa kama mtaalamu wa Kiswahili, naomba urekebishe kichwa cha habari yako, hakuna neno KIHOJA tuna KIOJA, nadhani sasa hili tatizo la kuweka "H" mahali pasipo hitajika linazidi kuwa kubwa. Hata hivyo asante kwa ujumbe mzuri
 
haya wahusu hayo, Mwenge ni wakitaifa zaidi na sio mdahalo
wewe mamba i mean mabuba,umeona hizo gharama zinazotumika hapo?angalia hapo uwanja hao watu wamevishwa kofia,t shirts,unajua kuwa hiyo ni kodi yako ambayo ingeweza kutumika kutoa elimu na afya bure?mental poverty inakusumbua
 
sikia huyu mtangazaji,anawalazimisha wananchi wote wasimame na kushangalia pindi jk atakapoingia,mkwanini uwalazimishe watu kufanya yote hayo?ni kampeni tu hapo
 
sikia huyu mtangazaji,anawalazimisha wananchi wote wasimame na kushangalia pindi jk atakapoingia,mkwanini uwalazimishe watu kufanya yote hayo?ni kampeni tu hapo

Mtani tupe habari zaidi za huko, natamani ningekuwa huko, wangeniamsha kwa winji
 
Mimi naomba masaada kujua HUU MWENGE UNA GHARIMU KIASI GANI KILA MWAKA???
 
Na nyimbo zinazo chezwa huku ni za "fall in love" inamaana hatuna nyimbo za kitamaduni Tanzania?
 
Wanajukwaa hakuna kitu kibaya kama mfumo wa uteuzi wa viongozi wa taasisi nyeti hapa TZ. kutokana na madalaka makubwa ya rais ambapo viongozi wa taasisi wanawajibika kwake. Napata shida kuamini kuwa huyu Tido ndio yule aliyekuwa BBC. Kwa sasa anafanya kazi katika utaratibu ambao anatakiwa kuwafurahisha watawala. Hapa swala la kuwajibika kwa wananchi HAKUNA. Utasikia excuse kibao kwanini hakuna live coverage kwa event muhimu kama huo mdahalo wa Nkurumah.!! Kazi Kweli kweli.
 
Back
Top Bottom