Mbona huyo mwanamke mwongo mwongo? Hasemi ukweli mpaka abanwe!! Hiyo ni indicator inayoashiria kukosa uaminifu.Siku ya leo nimefuatwa na rafiki yangu kipenzi kuniomba ushauri juu ya mpenzi wake.
Rafiki yangu ni mwajiriwa wa kiwanda cha cement na amepanga kufunga ndoa na dada mmoja msomi wa chuo kikuu na kuna taratibu zishaanza kufuatwa
Sasa bas bi dada(shemeji yangu)chuoni kulikuwa na kisherehe cha kuwaaga wahitimu
Sasa siku ya tukio akamwomba ruhusa mshikaji wangu ya kwenda kwenye hiyo sherehe(kuna muda mwanaume alikuwa anamkatalia baadhi ya sherehe kwenda)
Sasa siku hiyo jamaa akampa ruhusa na alichomwambia yule dada ni take "care""(nimenukuu)
Bas jamaa akawa anajiandaa kuingia zake kazini ila cha ajabu kuna kitu kikamtuma apitie sehemu ya hiyo sherehe kabla ya kwenda kazini.
Shetani akiamua lake sasa:::,!!Hamadi jamaa akiwa garini anamuona mchumba ake analetwa na jamaa aliyetambulishwa na mpnz wake kuwa ni marafiki(mara kwa mara jamaa alikuwa anakuta sms za jamaa kwa bidada japo ni za kawaida tu)
Ilipofika usiku wa manane jamaa akaondoka na demu wa rafiki yangu na kumrudisha kwako(kwa mujibu wa shemeji)
Siku inayofuata ambayo ni leo jamaa kamuuliza bi dada alikuja na usafiri gani kwenye hiyo sherehe dada akadanganya kwa boda(wakati jamaa alishuhudia kila kitu)baada ya kubanwa akataja kweli aliletwa na yule mwanamme ambae ni best yake tu na kurud nae hiyo saa 9 usiku;
Sasa amekuja kwangu kuomba ushauri wa vitu vifuatavyo÷
1)Kwanini mpenzi wangu aweze omba ruhusa ya kwenda na kushindwa kusema ataenda na nan?
2) Hii ni kitu cha kawaida?
3) Hana uhakika gan kama bi dada Alienda salama na kurud salama
4) Why akuambiwa na mpenzi wake kuwa atafuatwa na huyo mtu.(hapa dada alijitetea kuwa aliogopa atamzuia)
Ebu niweke wewe kama ndo mshauri kwa ishu kama hii ungeshauri nini maana mimi naona akili yangu kama imegota kutoa ushauri.
Tatizo kuwashauri wapenzi ni ngumu sana.
Jibu/ushauri lizi/uzi-ngatie maswali na majibu yao. Otherwise ni ngumu....kushsuri katika mapenzi.🙇