SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amewapasha wabunge kuwa anaongozwa na kanuni na si matakwa ya wabunge. Amesema hajafungwa kitambaa usoni kiasi cha kushindwa kufahamu anachokifanya anapoongoza vikao vya Bunge.
Kauli ya jana ya Spika Anne inatokana na baadhi ya wabunge kusimama kuomba muongozo wa spika wakati akiendelea kuzungumza mambo mbalimbali bungeni.
Kabla ya wabunge kusimama kuomba muongozo, Godbless Lema (Arusha Mjini-CHADEMA), alihoji jina lake kutokuwepo katika orodha ya wabunge waliomuuliza maswali Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Lema alisema aliwahi kujiandikisha ili kuuliza swali kwa waziri mkuu kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, lakini anashangazwa hakupata fursa ya kufanya hivyo.
"Niliwahi kujiandikisha na kuwa mtu wa nane, lakini Mnyika (John) aliyekuwa mbali zaidi amepata nafasi ya kuuliza swali. Napenda kufahamu kama hakuna sababu ya kuwahi kujiandikisha na badala yake kuna vitu vinavyoangaliwa?" alihoji.
Spika Anne akijibu hoja hiyo alisema idadi ya walioomba kumuuliza maswali waziri mkuu ni kubwa, hivyo alichagua wachache kulingana na jinsia, vyama na majimbo.
Baada ya jibu hilo, wabunge takriban watano waliwasha vipaza sauti kuomba muongozo wa spika, jambo lililomfanya Spika Anne kusimama na kusema:
"Siwezi kuongozwa na wabunge, mimi ndiye naongoza vikao. Siwezi kuongozwa kama nimefungwa kitambaa usoni na sifahamu ninachokifanya," alisema.
TAFAKARI