Sijafungwa kitambaa usoni - Spika

makerubi

Member
Apr 11, 2011
81
3
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amewapasha wabunge kuwa anaongozwa na kanuni na si matakwa ya wabunge. Amesema hajafungwa kitambaa usoni kiasi cha kushindwa kufahamu anachokifanya anapoongoza vikao vya Bunge.

Kauli ya jana ya Spika Anne inatokana na baadhi ya wabunge kusimama kuomba muongozo wa spika wakati akiendelea kuzungumza mambo mbalimbali bungeni.

Kabla ya wabunge kusimama kuomba muongozo, Godbless Lema (Arusha Mjini-CHADEMA), alihoji jina lake kutokuwepo katika orodha ya wabunge waliomuuliza maswali Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Lema alisema aliwahi kujiandikisha ili kuuliza swali kwa waziri mkuu kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, lakini anashangazwa hakupata fursa ya kufanya hivyo.

"Niliwahi kujiandikisha na kuwa mtu wa nane, lakini Mnyika (John) aliyekuwa mbali zaidi amepata nafasi ya kuuliza swali. Napenda kufahamu kama hakuna sababu ya kuwahi kujiandikisha na badala yake kuna vitu vinavyoangaliwa?" alihoji.

Spika Anne akijibu hoja hiyo alisema idadi ya walioomba kumuuliza maswali waziri mkuu ni kubwa, hivyo alichagua wachache kulingana na jinsia, vyama na majimbo.

Baada ya jibu hilo, wabunge takriban watano waliwasha vipaza sauti kuomba muongozo wa spika, jambo lililomfanya Spika Anne kusimama na kusema:

"Siwezi kuongozwa na wabunge, mimi ndiye naongoza vikao. Siwezi kuongozwa kama nimefungwa kitambaa usoni na sifahamu ninachokifanya," alisema.


TAFAKARI
 
Huyu mama ni bomu sana, amewekwa pale ili kupindisha taratibu za Bunge kwa manufaa ya chama chake cha mafisadi.
 
Mama anakuwa kama mwalimu wa darasa asiyekuwa na mood nzuri (mara nyingi) awapo darasani:)
 
Watanzania wameshaona umuhimu wa Spika aliyepita Mh. Samwel Sitta alikuwa makini sana. Huyu Mama aliyepandikizwa na CCM hatalimudu kabisa Bunge. Hakutakiwa kumzuia Mbunge aliyechaguliwa na wananchi kuuliza swali na kutoa dukuduku lake. Huyu Makinda ndiye wa kulaumiwa vurugu zikiingia Bungeni. Huwezi kuongoza kwa upendelea wa wazi kiasi hicho.
 
Mama tuliza mawazo kabisa. Majibu yako yatakuletea maswali mengine tena magumu kabisa. Nafikiri uchague sana maneno ya kuongea kwa hao wabunge kwani unaongoza bunge lenye itikadi tofauti sana.

Namaanisha kwamba Ongea kidogo, fikiria sana.
 
Mama anakuwa kama mwalimu wa darasa asiyekuwa na mood nzuri (mara nyingi) awapo darasani:)
Sasa hivi watu wengi wameamka kisiasa na wameshajua majukumu yao kisiasa, hali hii ndiyo inafanya ionekane kama kiti cha spika kinapwaya lakini ukweli ni kuwa hata angekuwa nani mambo yangeenda vivi hivi kwani kinachotakiwa ni kufuatwa kwa taratibu na sheria zilizowekwa ili kuliongoza bunge. Baadhi ya mabunge mengine Bunge ni eneo la kawaida la masumbwi ila bunge letu bado hatujafikia huko hivyo hakuna sababu ya kuona kuwa huyu mama hawezi.

Kazi ya kuongoza wanasiasa ni ngumu sana.
 
Tumuombee asije pata shinikizo la damu maana kuongoza Bunge la sasa ni kugumu sana.
 
SIX anafaa na atafaa siku zote fitna na ghilba za mafisadi yanayosema yanajivua gamba kama nyoka aibu yao na spika wao..
 
Duh! Kumbe kuuliza swali lazima spika aangalie sura yako kwanza na aipende ukiwa unatisha umeula wa chuya.
 
tatizo ni kuwa hata wabunge wa ccm wanajua hakuwa chagua lao bali la kundi fulani ndani ya chama

Kama walijua hivyo, wangempa Mabere basi. Hii inadhihirisha walivyo wabinafsi; ni genge hatari kabisa lisilojali maslahi na mustakabali wa taifa.
 
Duh! Kumbe kuuliza swali lazima spika aangalie sura yako kwanza na aipende ukiwa unatisha umeula wa chuya.

Halafu ukizangatia muuliza swali aliwahi kumtuhumu muilizwa kuwa amesema uongo hapo naona hatapata nafasi ya swali la papo kwa papo.
 
Kiukweli uongozi huu wa Jakaya umepwaya sana yaani kila mmoja anafanya kile anachoona ni sshihi anafanya hata Kama ni mwiba kwa wananchi,tuona wote upotevu wa bilioni 48 zilivyoibwa kutokana na ripoti ya mkaguzi mkuu wa Serikali na hapohapo mkaguzi huyo hakupewa document zote toka Serikalini.Hivi kwa style hii tutafika?,haya ya Spika kuupendelea upande mmoja ni muendelezo tu wa muvu letu.
 
Hata ukimuita mwendawazimu......"we kichaa njoo" hatakuchekea, Makinda hajijui kama ni bogus na aliwekwa na wale waliotaka Sitta atoke; cheap prize. Namhurumia kuuvaa mkenge ataumia sana hadi kuifikia 2015
 
Jamani huyu mama ,sijui amesoma wapi ...kiingereza chake kibovu ,poor Tanzanians

speaker huyu kweli ????tunamlinganisha na mzee 6 ?? ndio Tanzania ya JK
 
Halafu ukizangatia muuliza swali aliwahi kumtuhumu muilizwa kuwa amesema uongo hapo naona hatapata nafasi ya swali la papo kwa papo.

Hili ndio neno, inaonesha muheshimiwa alipopiga jicho akaona Lema akasema huyu ondoa sitaki kumsikia kabisaaaaa!!!
 
Sasa hivi watu wengi wameamka kisiasa na wameshajua majukumu yao kisiasa, hali hii ndiyo inafanya ionekane kama kiti cha spika kinapwaya lakini ukweli ni kuwa hata angekuwa nani mambo yangeenda vivi hivi kwani kinachotakiwa ni kufuatwa kwa taratibu na sheria zilizowekwa ili kuliongoza bunge. Baadhi ya mabunge mengine Bunge ni eneo la kawaida la masumbwi ila bunge letu bado hatujafikia huko hivyo hakuna sababu ya kuona kuwa huyu mama hawezi.

Kazi ya kuongoza wanasiasa ni ngumu sana.

Kwani huwa mnalipwa hela kutetea udhaifu?

Mbona unajichanganya, kisha unatoa jibu yani ueleweki.

Jibu lako ni tosha kabisa na ndo udhaifu wa mama, kwamba aongoze bunge kwa kufuata KANUNI na sio kwa STRATEGIES za kulinda ccm na serikali.
 
Halafu mama amesahau kua kitambaa alifungwa siku alipokubali kuchukua hayo madaraka, sasa ajue sio kufungwa kitambaa tu alipigwa changa la macho.
 
Back
Top Bottom