gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,274
- 20,673
- Thread starter
- #101
Halafu kwenye siri napo huwa napata utata.
Kuna watu vyumbani mwao utadhani wanaficha madawa ya kulevya, chumba cha wazazi ni siri, siri siri saaaaaaana.
Utaskia, weee, dada atachunguliaje chumbani kwako, hebu leo nijuzeni, kuna shida gani dada kuingia chumbani kwako???
hivi unapata utata gani? kwani wewe huna usiri? binafsi napenda sana usiri hasa kwenye mambo ya maendeleo ya nyumbani kwangu. sipend mtu ambaye mumewe akisafiri tu kesho unalikuta mtaani baba nanii kasafiri ama wamepanga kujenga unaskia kesho yake mtaani.
chumba kutokuzoewa ni heshima na usalama wa nyumba yako. mfano chumbani umeweka hati zako za nyumba magari vito na hata pesa kama mnamiliki silaha basi hata silaha ipo hapo. sasa je waweza kupaacha pawe ni mahali ambapo watu wanaingia hovyo kweli?
nina mfano wa rafiki yangu alikuwa anaacha chumba chake wazi huwez amini alikuta siku mdogo wake wa kiume amelala kwenye kitanda chake na binti wa kazi wanafanya ngono. it was shame aisee.