Siasa zaiondoa BP Tanzania

(on red) kampuni kama hizi unakuta hata wafanykazi anayedumu muda mrefu ni miezi sita labda ukiondoa ndugu zao. angalia hata site zao walizojenga petrol stations, zote zina utata na hata walivyojenga havina hata uimara unaoeleweka alafu utegemee hizi kampuni kuweza kumaintain standards kama za BP au TOTAL!
Tunavutia wawekezaji na sasa 'potential investors' wanaanza kuondoka nasi tunabakia na ngonjera zilezile za 'uchumi unakua'!
Uko sawa kabisa. Ni hasara kubwa sana kwa nchi za Afrika kukosa makampuni makubwa kama Shell na BP. BP na Shell ziko kwenye top ten richest ans large companies in the world. Kwa sasa nafikiri Shell ndio kampuni ya Pili kwa utajiri ikizidiwa na General Electric (GM) ya marekani. Ajira kwenye kampuni hizi ni bora kuliko hata serikali. Yaani tu ni kwa kutojua tunafikiri BP ikiondoka tumepata nafuu lakini tumepata hasara kubwa. Kijana mwenye elimu yake nzuri aliyemaliza chuo kikuu vizuri angepata ajira nzuri kwenye makampuni haya tu na si Moil, Cameloil, Lake oil na wababaishaji wengine. Yaani huko ni wizi tu. Watu hawalipwi vizuri hakuna akiba ya uzeeni. Manake ni kuwa watu wanaokuwa na ajira nzuri wanaoweza kuendeleza jamii zetu maskini wamepungua tunaishia kubanana kwenye hivi vikampuni uchwara vya wahindi, waarabu na wasomali. Ni aibu kwetu waafrika kuwa haya makampuni yamekuwepo miaka 50 wanaondoka hatuna makampuni yetu yaliyosimama tunabaki kuanza upya na wezi wa kihindi na kiarabu. Yaani tumeruka mkojo na kukanyaga mavi.
 
Wana jamii.

Nimesoma katika economic forum na kuona BP imeamua kuuza hisa zake zote ilizokuwa inamiliki katika BP Tanzania kwa mwekezaji mwingine na hivyo kujitoa rasmi katika umiliki wa kampuni hiyo ndani ya Tanzania.

Na sababu walizobainisha ni kwa kuwa biashara ya mafuta inaendeshwa kisiasa zaidi na mamlaka za Tanzania na kwa kuwa wao hawakuwa tayari kugombana na mamlaka hizo ndani ya TZ wameamua kujitoa rasmi kwa kuuza hisa zao zote 50% kwa kampuni nyingine.

My Take: Je ni wapi waTZ watapata mafuta kwa ajili ya magari yao yasiyochakachuliwa? na vipi mafuta ya ndege itakuwaje?

Nawapa Pole wa Tz na kuwapongeza BP kwa kujali ubora wa bidhaa zenu.

jibu lake ni hili " Miafrika ndivyo Tulivyo" by NN
 
Kuna kampuni kibao hapa Bongo nyingine zina majina ya kibantu bado zinao uwezo wa kuagiza mafuta under TPDC, kiburi chao ndo kimewafanya watoweke bongo. WAPUMZIKE KWA AMANI!

Genakai,

BP walishaamua kuondoka muda mrefu na wakati wanapewa bann na serikali walikuwa kwenye kipindi tu cha makabidhiano na Puma Energy amabayo ni undertaking ya Trafigura. Bora uwe na BP au Shell moja kuliko kuwa na hivo vikampuni vya waarabu na Kihindi. Ajira ni ya uhakika, si ubabaishaji na wanafuata taratibu zote za nchi pamoja na kutokwepa kodi za serikali. Hivi vikampuni vya kihindi ni uwizi mtupu. Wanakuwa na short term vision ya kuangalia faida bila kuzingatia athari zake in the long run. Ndio maana hazidumu zinaanzishwa zinafnaya vizuri na zinakufa upepo ukibadilika kidogo tu. Sasa kama nchi inayotaka maendeleo inayotokana na kodi, ajira kwa watu wake na bidhaa bora kwa matumizi ya mitambo na kulinda mazingira ni hasara kubwa sana kuwa na hivo unavoviita makampuni. Nikuambie tu hayo makampuni yangekuwa yanalipa kodi bila kukwepa serikali ingekuwa inapata kodi kubwa lakini wanalipa kidogo tu huku nyingi zikikwepwa kushirikiana na serikali ya kifisadi.
Kuhusu BP kukiuka agizo la EWURA ni kuwa Ewura walikosea kupiga mahesabu yao ya gharama ambayo yangeshusha ili makampuni yasipate hasara na ndio maana EWURA kwa kuogopa kuumbuliwa na BP kwenye baraza la ushindani wamekubali kuweka deal na BP. BP walikuwa wanapata hasara hivo wamekubali yaishe wasiwaumbue EWURA lakini pia wafunguliwe waendelee na biashara. Lakini pia yawezekana rushwa imetembezwa kwa waziri wa nishati na viongozi wa EWURA kutoka kampuni iliyonunua BP yaani Puma make Puma hawana Ethics kama BP za kutojihusisha na rushwa katika biashara.
 
kumbuka na Chevron waliondoka, kumbuka kila kampuni inaweza kufanya biashara ya mafuta lakini credibility ya BP iko juu worldwide na ulipaji kodi pamoja na usalama wa kazi kwao vipo juu sana ukilinganisha na haya makampuni mengine ambayo incentive yao kubwa ni kukwepa ushuru na kodi ili kutengeneza faida kadiri iwezekanavyo

Yes, BP's credibility is high worldwide. But credibility alone doesn't elevate a company to royality at the cost of the country's laws and regulations. Any company may be tempted to dilute the product if the regulatory bodies versed with the task of protecting consumers become weak and collusive. After all, keep in mind that oil worldwide is a cartel business whose incentive is profit. There are reported cases of infidelity in some fuel-selling centres belonging to BP within the country! The credibility they enjoy in other countries is due to strictness of the corresponding regulatory bodies in those countries which we want BP to adhere within this country as well. Don't be easily cheated! "Waache waondoke" if they don't wish to comply with the regulatory demands. Whether the regulations are fair or not is an issue of debate na wala sio kuondoka kwao.
 
Wajanja wale wamesoma nyakati wameona 2015 patakuwa badogo magamba wakichakachua matokeo wale wajanja washasoma nyakati watapata hasara 2015 mana tutachoma kila kitu.
 
Wana jamii.

Nimesoma katika economic forum na kuona BP imeamua kuuza hisa zake zote ilizokuwa inamiliki katika BP Tanzania kwa mwekezaji mwingine na hivyo kujitoa rasmi katika umiliki wa kampuni hiyo ndani ya Tanzania.

Na sababu walizobainisha ni kwa kuwa biashara ya mafuta inaendeshwa kisiasa zaidi na mamlaka za Tanzania na kwa kuwa wao hawakuwa tayari kugombana na mamlaka hizo ndani ya TZ wameamua kujitoa rasmi kwa kuuza hisa zao zote 50% kwa kampuni nyingine.

My Take: Je ni wapi waTZ watapata mafuta kwa ajili ya magari yao yasiyochakachuliwa? na vipi mafuta ya ndege itakuwaje?

Nawapa Pole wa Tz na kuwapongeza BP kwa kujali ubora wa bidhaa zenu.

Kwa taarifa yako BP ilishauzwa kitambo katika nchi nyingine na ilibaki hapa tu. Hata hivyo tunawatakia kila la heri huko kusiko na sheria waendako. Wanyonyaji wakubwa.
 
Waondoke ili wale waliokuwa wanabanwa waingie. Wasituzingue! Walizoea kudekezwa
 
Back
Top Bottom