Siasa zaiondoa BP Tanzania

Halafu naomba waandishi wetu wajifunze ku-analyse habari kabla ya kubandika vichwa vya habari magazetini. The way walivyoripoti hii habari ni kwamba the winner ni EWURA, Kumbe EWURA NA TZ ndo loosers, kwani hata mkuu wa ewura kichwa kilimvimba kwa kuona wamewaweza bp. Kumbe hawa bp walichokifanya baada ya kuuza shea zao zote, Puma sijui nini wakazinunua, wameamua kuwasafishia njia Puma, na ili puma wa-sign deal lazima bp wasiwe na kesi yoyote mahakamani, au bad reputation na partners wao yaani TZ govt. So msamha wa bp si wa kweli, ni kujisafisha tu kwa wanunuzi wa shea zao. Wameona hailipi kufanya business TZ.
 
kumbuka na Chevron waliondoka, kumbuka kila kampuni inaweza kufanya biashara ya mafuta lakini credibility ya BP iko juu worldwide na ulipaji kodi pamoja na usalama wa kazi kwao vipo juu sana ukilinganisha na haya makampuni mengine ambayo incentive yao kubwa ni kukwepa ushuru na kodi ili kutengeneza faida kadiri iwezekanavyo
Sioni tatizo. Waondoke tu. Hakuna pigo lolote kwa mtu anayefikiri na kujua biashara. Wapo wengine watakaofanya biashara hiyo tena kwa ufanisi mkubwa. Kwanza BP ilikuwa mwanahisa tu akishirikiana na serikali katika umiliki. Wapo wengine walikwishalimezea macho dili hilo kwa siku nyingi na sasa watalidaka haraka. Acheni kuwapa bichwa hao makaburi. Kwanza lazima ujue kuwa wakati wamefungiwa kwa miezi mitatu cargo yao ya mafuta ilikuwa inauzwa kama kawaida kupitia kampuni ya Engen ambao ni makaburi wenzao. Kama Engen tu waliweza kuinunua cargo yote ya BP na kuiuza kila kukicha sembuse umiliki!!
 
BP ni moja ya kampuni kubwa ba nzuri ,nazani hii ndio effect ya kuwa na viongozi uchwara,hawaangalii maslahi ya nchi,ila wanabebana wao na wafanyabiashara wanaojuana,bila kuangalia quality ya bidhaa na mambo mengine,
naskita sana kwa wadau wote ajira zao ambazo zinaweza kuwa hatarini
 
Kuna kampuni kibao hapa Bongo nyingine zina majina ya kibantu bado zinao uwezo wa kuagiza mafuta under TPDC, kiburi chao ndo kimewafanya watoweke bongo. WAPUMZIKE KWA AMANI!
 
Serikali ya Tanzania ina hisa ya asilimia 50, na zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na kampuni ya BP Afrika, lakini kwa sasa kampuni hiyo ya BP imeuza hisa zake kwa kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited. Kutokana na hali hiyo kampuni hiyo itabadilishwa jina wakati wowote kuanzia sasa kutokana na kumilikiwa na kampuni nyingine.
Nashukuru kwa taarifa mkuu,
 
Waache wachape mwendo huwezi kuwa na wawekezaji wenye kiburi na dharau kwa Serikali kama BP ambao wanaigomea na kuongoza migomo ya kupandisha mafuta. Makapuni ya mafuta yapo mengi tu na Serikali inaweza kuwa na vituo vyake. Mbona zamani kulikuwa na vituo vya mafuta kwenye taasisi za serikali na magari yalikuwa yakijazwa mafuta hapo.
 
Inabidi wawekezaji wa ndani wajitahidi, tusipate impact yeyote negative kutokana na maamuzi hayo. Hata hivyo Tanzania sasa hivi inawawekezaji wengi sana wakubwa katika sector ya mafuta tuna waarabu wengi tu na wazawa wengi wameibuka katika miaka ya hivi karibuni kama akina Ridhwani Kikwette

Mungu apishie mbali isijekutokea kwamba Ridhiwani kikwete ndiye anategemewa kwa usambazaji wa mafuta nchini. Nchi itaingia kwenye mgogoro mbaya kabisa wa kiuchumi ambao hatujawahi kuushuhudia, ni zaidi ya ngeleja anavyotuimbia mashairi ya mahesabu ya megawati huku tukiendelea kupata mgao wa giza.

Na mimi binafsi sina imani sana na hawa watanzania waarabu juu ya uendeshaji wa biashara ya mafuta, hasa tukiwa chini ya utawala wa magamba na kikwete. Hadi hapo tutakapopata uongozi mpya chini ya chama kipya ndipo tunaweza kutegemea mabadiliko kwenye sekata ya mafuta lakini kwa sasa ambapo serikali ipo ndani ya mfuko wa wafanyabiashara, hakuna jipya.
 
BP imeuzwa tangu mwezi 4 hata kabla ya mgogoro kutokea imeuza share zake kwa puma company in all african countries tz being one of them.
 
Naona wengine wanafurahia BP ambayo "Corporate entity" kuondoka ili tubaki na "family companies"; hatuoni kwamba ni mmoja wa mwajiri mzuri anaondoka tunabakiza kampuni za kifamilia ambazo hata NSSF hazitapeleka?
 
Mie nawaunga mkono CCM kwa hili, kwani wakati mwingine ubabe unafaa, we nenda China au Malaysia au Singapoe au Japan nenda ulete ujinga wako kwa serikali mbona unaadhibiwa, nadhani BP wamefanya kinafiki tu, tena ningekuwa na hela ningezinunua hizo hisa.
 
Nijuavyo mimi BP wameuza share zao kwa PUMA kwenye usambazaji wa mafuta katika nchi nyingi Africa including Tanzania, Zambia, Botswana na Namibia. Inawezekana TZ process imechukua muda lakini ukienda Namibia sasa utakuta nembo ya BP imebadilishwa na kuwekwa ya Puma. Huo ulikuwa ni mkakati wao wa biashara Africa na si TZ pekee. Hili swala la kesi na politics inawezekana kabisa ikawa ni coincidence!!
Ur right mr zero
 
Huko kote waliouza hisa zao ni kwa sababu politics na ufisadi umezidi nchi nyingi za Afrika. Watu wanakwepa taratibu, wanakwepa kodi, hawazingatii taratibu za usalama kazini, wanalipa wafanyakazi pesa kiduchu, ajira za kubabaisha na poor product quality. Kwa maana hiyo wachakachakachuaji wanaolindwa na serikali wanakiwa na cost ndogo na kuuza bidhaa zao bei ndogo huku zile za BP zikionekana na ghali hivo kukosa wateja. Ni makampuni ya nje yaliyoenda shule yanayojua umuhimu wa ubora kama GGM kule Geita na wengine wachache wanaowataka makampuni yenye heshima kama BP na Shell. Siyo BP tu hata Shell wanaondoka Afrika kwasabu hiyo hiyo. Hivi si vikampuni uchwara hivi, vinazingatia viwango vyao vya kutoa huduma na ubora, sio tu vinaweza kufunga shughuli kwa kukosa faida hata taratibu za usalama na ubora unaotakiwa ukikosekana wako radhi kuacha faida ili kutomdhuru mtu au kujiaribia jina.
Unaweza kusema ni business strategy lakini kwa mfano Shell wanasema wanaondoka Afrika kwasabu ni faida ndogo sana wanapata Afrika lakini ndiko wanakoaribu jina lao kila siku kwa kuwa si serkali wala watu wanaozingatia taratibu na sheria za biashara na usalama.
 
Mungu apishie mbali isijekutokea kwamba Ridhiwani kikwete ndiye anategemewa kwa usambazaji wa mafuta nchini. Nchi itaingia kwenye mgogoro mbaya kabisa wa kiuchumi ambao hatujawahi kuushuhudia, ni zaidi ya ngeleja anavyotuimbia mashairi ya mahesabu ya megawati huku tukiendelea kupata mgao wa giza.

Na mimi binafsi sina imani sana na hawa watanzania waarabu juu ya uendeshaji wa biashara ya mafuta, hasa tukiwa chini ya utawala wa magamba na kikwete. Hadi hapo tutakapopata uongozi mpya chini ya chama kipya ndipo tunaweza kutegemea mabadiliko kwenye sekata ya mafuta lakini kwa sasa ambapo serikali ipo ndani ya mfuko wa wafanyabiashara, hakuna jipya.

Unataka hadi mzungu aje ndiyo utakuwa na imani nao
 
Naona wengine wanafurahia BP ambayo "Corporate entity" kuondoka ili tubaki na "family companies"; hatuoni kwamba ni mmoja wa mwajiri mzuri anaondoka tunabakiza kampuni za kifamilia ambazo hata NSSF hazitapeleka?
Uko sawa kabisa. Ni hasara kubwa sana kwa nchi za Afrika kukosa makampuni makubwa kama Shell na BP. BP na Shell ziko kwenye top ten richest ans large companies in the world. Kwa sasa nafikiri Shell ndio kampuni ya Pili kwa utajiri ikizidiwa na General Electric (GM) ya marekani. Ajira kwenye kampuni hizi ni bora kuliko hata serikali. Yaani tu ni kwa kutojua tunafikiri BP ikiondoka tumepata nafuu lakini tumepata hasara kubwa. Kijana mwenye elimu yake nzuri aliyemaliza chuo kikuu vizuri angepata ajira nzuri kwenye makampuni haya tu na si Moil, Cameloil, Lake oil na wababaishaji wengine. Yaani huko ni wizi tu. Watu hawalipwi vizuri hakuna akiba ya uzeeni. Manake ni kuwa watu wanaokuwa na ajira nzuri wanaoweza kuendeleza jamii zetu maskini wamepungua tunaishia kubanana kwenye hivi vikampuni uchwara vya wahindi, waarabu na wasomali. Ni aibu kwetu waafrika kuwa haya makampuni yamekuwepo miaka 50 wanaondoka hatuna makampuni yetu yaliyosimama tunabaki kuanza upya na wezi wa kihindi na kiarabu. Yaani tumeruka mkojo na kukanyaga mavi.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa pale wanamapinduzi wakweli walipo amua kutumia njia ya Passive resistance kufikisha ujumbe kwa jamii yote ya Tanzania. Hamna mtu atakaye andamana ila watavaa nguo nyeusi siku hiyo ya jumatatu kulaani mambo mengi yanayotendeka na hii serikali likiwemo , kukosekana kwa umeme, mikataba mibovu, huduma duni za maji, afya na elimu, Umaskini ulio kithiri, Wingi wa safari za mkuu wa kaya pasipo tija, uzembe na kutowajibika kwa watendaji:

Be part of the change, sms zinazunguka japo Mod anaibania kuiweka kwenye jamii forum wingi wa nguo nyeusi utamaanisha wingi wa wataka mabadiliko the time is now or Never!

Changes always honours the mind that is prepared! Lets do Let go for change! Neither Chadema nor CCM will bring the change that we people of Tanzania can bring. Black garmet is to send the message to the Government!
 
Mkuu BP wamejotoa nchi nyingi za kiafrika. Hapa nchini tatizo lilikuwa uchakachuaji wakati BP wana viwango vyao. Utakuta kampuni ya mafuta inaitwa MbuziOil nayo inauza petrol ambayo imechanganywa na mafuta ya taa na bei inakuwa chini lakini kwa ku maintain quality utakuta BP wako juu. Kisha kukaja haka kakitu kanaitwa Beio Elekezi sijui na bei kikomo.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa pale wanamapinduzi wakweli walipo amua kutumia njia ya Passive resistance kufikisha ujumbe kwa jamii yote ya Tanzania. Hamna mtu atakaye andamana ila watavaa nguo nyeusi siku hiyo ya jumatatu kulaani mambo mengi yanayotendeka na hii serikali likiwemo , kukosekana kwa umeme, mikataba mibovu, huduma duni za maji, afya na elimu, Umaskini ulio kithiri, Wingi wa safari za mkuu wa kaya pasipo tija, uzembe na kutowajibika kwa watendaji:

Be part of the change, sms zinazunguka japo Mod anaibania kuiweka kwenye jamii forum wingi wa nguo nyeusi utamaanisha wingi wa wataka mabadiliko the time is now or Never!

Changes always honours the mind that is prepared! Lets do Let go for change! Neither Chadema nor CCM will bring the change that we people of Tanzania can bring. Black garmet is to send the message to the Government!

Hiii nayo ni BP?
 
Back
Top Bottom