Zanzibar 2020 Siasa za Zanzibar: Hongera Dr. Mwinyi Kwa Ushindi wa Kishindo, Maalim Makamo wa I, Mteue Balozi Amina Salum Ally Awe Makamo wa II, Utoe Sare Sare Maua

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,621
Wanabodi,

Kwa vile uchaguzi wa Zanzibar pia umesababisha vidonda na bado ni vibichi, damu bado haijakauka, hivyo naomba kuanza bandiko hili kwa a healing massage ya kuponya vidonda kwa kuungana na Watanzania wengine wote wapenda haki, amani na utulivu, kutoa pole kwa wahanga wa kilichotokea Zanzibar kwenye uchaguzi huu, ukiwemo umwakigaji damu, natoa pole kwa wote, na kama ni kweli kuna dhulma zozote zilizofanyika, then JAJI MKUU WA MAJAJI WOTE DUNIANI KWA KUTUMIA SHERIA KUU YA HAKI DUNIANI, THE LAW OF KARMA, will take care of this.

Sasa uchaguzi umeisha, life has to go on back to normal huku tukiendelea kuponya majeraha ya uchaguzi, pole sana kwa washindwa, na hongera kwa washindi.

Siasa za Zanzibar, natoa hongera kwa Dr. Hussein Mwinyi, kwa ushindi wa kishindo, cha kihistoria, haijapata kutokea toka Zanzibar izaliwe, ushindi wa zaidi ya asilimia 50%, siku zote uchaguzi wa Zanzibar matokeo huwa ni close range, lakini safari hii, ushindi wa 76% ni landslide ya funga kazi, na funga kalomo kwa vitimbakwiri vyenye maneno maneno kuhusu uchaguzi wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar yenye GNU, japo kwa ushindi wa Dr Mwinyi wa zaidi ya 75%, then Dr. Mwinyi, anaweza kuunda serikali yeye mwenyewe lakini bado analazimiki kuunda serikali ya GNU, na ACT japo ni kwa ushindi kiduchu wa Maalim Seif Sharrif Hamad, ambao umekidhi viwango vya more than 10% ya kujuimuishwa GNU kuwa Makamu wa I, wa rais, ila for the sake of national unity of Zanzibar, and Zanzibaris, namuomba Dr. Mwinyi, amteue tuu Maalim Seif kuwa Makamu wa kwanza hata kama atasusa kama kawaida yake, pia namshauri Maalim akubali uteuzi huo, kwa shingo Wilma ama shingo upande, maana kwa umri wake aliofikia, kipindi hiki kwake ni final finale, kwa uchaguzi wa 2025, kutahitajika damu changa, nashauri Jussa au Hamid apokee mikoba.

Namshauri Maalim Seif akubali uteuzi, kwasababu uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya makosa sana na ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa hayo, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.

Akubali uteuzi wa makamu wa I, Dr. Husein Mwinyi atamteulia wabunge 5 wa kuteuliwa, ili kutimiza idadi ya wabunge 6 wa kuingia kwenye GNU, asifanye tena ujinga kama ule wa 2015!. Kwa umri wake wa miaka 77, akisusa safari hii, ndio imetoka, maana 2025 atakuwa na umri wa miaka 82!.

Tukija kwa Makamu wa II wa rais, japo kwa maoni yangu baada ya Dr. Mwinyi, mtu wa pili kwa u presidential material ni Prof. Mbarawa,

images (24).jpeg
images (27).jpeg
images (26).jpeg
images (25).jpeg
Na rais Magufuli alimshauri Dr. Mwinyi kuchagua makamu toka Pemba, lakini kwa vile Makamu wa I ni Maalim Seif ni kutoka Pemba, then natoa wito kwa Dr. Mwinyi, amteue, Balozi Amina Salum Ally awe Makamu wa II, ili kutoa sare sare maua na makamu wa huku bara, Mama Samia Suluhu Hassan, tena sare ya Amina Salum Ally na Samia Suluhu Hassan, itakuwa ni sare inayoendana hadi macho!.

Nakuwekea picha 2, moja macho mawili na nyingine macho manne

Pasco
Rejea ya macho
 
Maalim Seif apokee tu hiyo position ili akafight kupenyeza baadhi ya ahadi zake nyingi za kampeni zitekelezwe, kwa maslahi mapana ya Taifa.

Pia itampa nafasi ya kuijenga zaidi ACT Wazalendo huku akijiandaa kustaafu siasa kwa heshima.

Akisusa maisha yatasonga tu na haitamsaidia yeye binafsi, chama chake na Wazanzibar wote.
 
Wewe nakuona kama mtu muovu hapa JF na hata siku nikisikia umepatwa na baya kutoka kwa hao unaowatetea hapa JF, hakika sitokuhurumia wala kukupa pole.

Umekosa utu kwa kiwango cha kutisha na ni mtu hatari sana wewe.
Endelea kutoa machungu tu, hakikisha usihamie kwenye pombe bado tunahitaji michango yako humu ndani.
 
Wanzibar 10 tisa wanalalamikia huu uteuzi na uminywaji wa Demokrasia,Bwana pasco bara kuna watu 52M+ na Visiwani 1.5M+, je ni sababu ipi imefanya visiwani kukapigwa kura kwa siku mbili tofauti na Bara?Kwanini mitaa na biashara na kila kitu kimefungwa mpaka sasa na askari na majeshi yanakatiza kila kona za mitaa?

Kama kweli ni ushindi wa kishindo wazanzibari wangekua sahizi wanasherekea kwa ushindi huo unaoutukuza.
 
Naam haijapata kutokea na wala haitotokea, sio kushinda kwa close range tu, hata kushinda kwenyewe CCM zanzibar haitotokea. Watabaki kulindwa na jeshi tu. Walichofanya ni kuthibitisha duniani kuwa bils jeshi CCM Zanzibar haina kura.

Ushauza utu kwa kitu ndio mana ukafikia kusema kuwa twitter ifungiwe ukiamini ina mambo ya kijinga, umesahau kama inaempigia debe yupo huko kwenye huo ujinga.
 
Wanzibar 10 tisa wanalalamikia huu uteuzi na uminywaji wa demokrasia,Bwana pasco bara kuna watu 52M+ na Visiwani 1.5M+, je ni sababu ipi imefanya visiwani kukapigwa kura kwa siku mbili tofauti na Bara?Kwanini mitaa na biashara na kila kitu kimefungwa mpaka sasa na askari na majeshi yanakatiza kila kona za mitaa?

Kama kweli ni ushindi wa kishindo wazanzibar wangekua sahizi wanasherekea kwa ushindi huo unaoutukuza.
Akikujibu nitag nione mtumwa amejibu nini?

Kama umesoma historia ya utumwa utaona kuwa mababu zetu wakiafrika ndio walichangia kuwauza waafrika wenzao kwa kupewa kioo ajione, mfano wa sasa ni huyu mtumwa pascal
 
Wewe nakuona kama mtu muovu hapa JF na hata siku nikisikia umepatwa na baya kutoka kwa hao unaowatetea hapa JF, hakika sitokuhurumia wala kukupa pole.

Umekosa utu kwa kiwango cha kutisha na ni mtu hatari sana wewe.
Mkuu unamuitaje mwenzio shetani?

Kafanya nini?
 
Wewe nakuona kama mtu muovu hapa JF na hata siku nikisikia umepatwa na baya kutoka kwa hao unaowatetea hapa JF, hakika sitokuhurumia wala kukupa pole.

Umekosa utu kwa kiwango cha kutisha na ni mtu hatari sana wewe.
Si unamuona kwa umri alionao, anachowaza Paschal ni kupata ulaji maana anaona umri unaenda na alishasemaga deals zake zimekufa hana kitu wala kazi yoyote. Amefulia. Anataka uteuzi kwa namna yoyote ile hata iwe kwa ubaya gani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom