Pius Kafefa
Member
- Aug 9, 2011
- 88
- 20
Wengi wetu tunafahamu namna ambavyo mikoa hii miwili ya Tabora na Kilimanjaro ilivyo na umuhimu katika siasa nchi hii.
Tangu wakati wa kutafuta uhuru hadi wakati wa siasa za mageuzi mkoa wa Tabora umekuwa chimbuko la wanasiasa wapinzani kama James Mapalala aliyeanzisha CUF, Chief Abdallah Fundikira aliyeanzisha TADEA, Prof. Lipumba aliyejipatia umaarufu ndani ya CUF kwa kuiongoza kwa miaka kadhaa.
Hata hivyo, pamoja na umaarufu wa wanasiasa hao, bado mkoa wa Tabora haukufanikiwa kuwa ngome ya wapinzani. Ni miezi michache tu iliyopita ndipo CUF ilipofanikiwa kupata mwakilishi kwenye Bunge la Tanzania, ambaye hata hivyo mgogoro uliopo umetishia nafasi yake ya uwakilishi.
Kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro, kuna wanasiasa maarufu wengi, kuanzia kwenye vyama vyao hadi majimboni. Augustine Mrema (NCCR Mageuzi & TLP), Edwin Mtei (Chadema), James Mbatia (NCCR Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema).
Swali, imekuwaje wenyeviti wa vyama vya upinzani kutokea mkoa wa Tabora washindwe kuimarisha upinzani mkoani Tabora, ilihali wenzao wa Kilimanjaro wamefanikiwa kukitoa jasho chama tawala?
Doesn't charity begin at home?