Siasa za Upinzani: Kilimanjaro vs Tabora

Pius Kafefa

Member
Aug 9, 2011
88
20
Wengi wetu tunafahamu namna ambavyo mikoa hii miwili ya Tabora na Kilimanjaro ilivyo na umuhimu katika siasa nchi hii.

Tangu wakati wa kutafuta uhuru hadi wakati wa siasa za mageuzi mkoa wa Tabora umekuwa chimbuko la wanasiasa wapinzani kama James Mapalala aliyeanzisha CUF, Chief Abdallah Fundikira aliyeanzisha TADEA, Prof. Lipumba aliyejipatia umaarufu ndani ya CUF kwa kuiongoza kwa miaka kadhaa.

Hata hivyo, pamoja na umaarufu wa wanasiasa hao, bado mkoa wa Tabora haukufanikiwa kuwa ngome ya wapinzani. Ni miezi michache tu iliyopita ndipo CUF ilipofanikiwa kupata mwakilishi kwenye Bunge la Tanzania, ambaye hata hivyo mgogoro uliopo umetishia nafasi yake ya uwakilishi.

Kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro, kuna wanasiasa maarufu wengi, kuanzia kwenye vyama vyao hadi majimboni. Augustine Mrema (NCCR Mageuzi & TLP), Edwin Mtei (Chadema), James Mbatia (NCCR Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema).

Swali, imekuwaje wenyeviti wa vyama vya upinzani kutokea mkoa wa Tabora washindwe kuimarisha upinzani mkoani Tabora, ilihali wenzao wa Kilimanjaro wamefanikiwa kukitoa jasho chama tawala?

Doesn't charity begin at home?
 
Hawana ubunifu,mawazo mapya,hawaoni mbali na kushindwa kufikisha ipasavyo kile walichokikusudia kwa jamii inayowazunguka
 
Fursa ya research hiyo. Itumie vizuri uandike na u publish maana huku google hatuonekani kabisa kwenye tafiti
 
..mbona mimi naona tofauti kidogo na hivyo unavyofikiri.

..Mtei aligombea Arusha 1995 akashindwa.

..Mbowe alishindwa ubunge 1995 na mgombea wa nccr.

..nadhani pia amewahi kushindwa na mgombea wa ccm.

..James Mbatia alishinda 1995 lakini akashindwa mwaka 2000.

..kwa ujumla wananchi huwa wanachagua yule wanayeamini atawaletea maendeleo na ambaye mtazamo wake unafanana na hali ya mazingira wakati wa uchaguzi.

..kwa hiyo mimi sikubaliani na dhana kwamba mkoa wa Kilimanjaro ni ngome ya upinzani.

..sasa nikukumbushe mwanasiasa JOHN CHEYO na chama chake UDP. Kuna kipindi Cheyo na Udp walikuwa na guarantee ya kushinda kila uchaguzi ktk maeneo ya Bariadi Shinyanga.

..labda ni vizuri kulinganisha BARIADI/SHINYANGA na TABORA. kwanini Cheyo alifanikiwa Bariadi lakini Prof.Lipumba hakufanikiwa Tabora.

..nadhani cha msingi ni chama kuwekeza ktk eneo husika na siyo kuibuka tu wakati wa uchaguzi ukitegemea utapata ushindi.
 
Hawana ubunifu,mawazo mapya,hawaoni mbali na kushindwa kufikisha ipasavyo kile walichokikusudia kwa jamii inayowazunguka

Hivi ubunifu, mawazo mapya, etc hupatikana ukiwa opposition?

1. Arusha 1995 ilichukuliwa na upinzani NCCR - Mageuzi, lakini 2000-2005 ikarudi CCM

2. 1995 - 2000 majimbo yote ya mkoa wa mara isipokuwa Musoma Mjini na Tarime yalikuwa chini ya Upinzani ila 2000-2005 lilibaki jimbo moja tu la upinzani la Tarime.

3 . Temeke ilishakwenda upinzani chini ya mrema na baada ya hapo hakuna kitu.

4. Magu ilishakuwa chini ya UDP chini Cheyo msimu mmoja baada ya hapo hakuna kitu, Nyamagana, Ilemela, etc

5. Hivi akina Machali, Mkosamali, Wenye, etc hawakuwa wabunifu? Mbatia alikaa bungeni 1995 - 2000 basi akapoteza, akaja kubebwa na JK - je yeye ubunifu aliupeleka wapi?

Je kama hayo majimbo yalichukuliwa na wabunifu, waona mbali, etc ikawaje yakarudi tena kwenye chama tawala? Nadhani tutafute sababu zingine zinazopelekea hio hali na wala si kutukana wananchi.
 
Hivi ubunifu, mawazo mapya, etc hupatikana ukiwa opposition?

1. Arusha 1995 ilichukuliwa na upinzani NCCR - Mageuzi, lakini 2000-2005 ikarudi CCM

2. 1995 - 2000 majimbo yote ya mkoa wa mara isipokuwa Musoma Mjini na Tarime yalikuwa chini ya Upinzani ila 2000-2005 lilibaki jimbo moja tu la upinzani la Tarime.

3 . Temeke ilishakwenda upinzani chini ya mrema na baada ya hapo hakuna kitu.
4. Magu ilishakuwa chini ya UDP chini Cheyo msimu mmoja baada ya hapo hakuna kitu, Nyamagana, Ilemela, etc

Je kama hayo majimbo yalichukuliwa na wabunifu, waona mbali, etc ikawaje yakarudi tena kwenye chama tawala?
Kuna kuchokwa na kushindwa kutekeleza mana ubunifu wako unakuwa umefika kikomo..mtu kama Cheyo na Mrema unaona ana nini cha ziada ambacho atawambia wananchi wakamwelewa
 
Hivi unadhani chama tawala kinaingia kwenye uchaguzi kikiwa na kura sifuri kama upinzani?
Tusingeona mapicha picha yanayotokea kila uchaguzi.
Sio kila wakati ccm inapochukua jimbo wanastahili kusifiwa, mara nyingi wanastahili kulaaniwa.

Naota jamani ila pia jana nilimeza dawa za Malaria
 
Kuna kuchokwa na kushindwa kutekeleza mana ubunifu wako unakuwa umefika kikomo..mtu kama Cheyo na Mrema unaona ana nini cha ziada ambacho atawambia wananchi wakamwelewa
Mkuu hapa naona tatizo haliko kwa wapiga kura, ila kwa mgombeaji ama chama chake.
 
Nadhani elimu na exposure ya watu wa mkoa husika pia inahusika, Tabora watu wake ukilinganisha na Kilimanjaro (no offense) Kilimanjaro ni watu wasioaminishwa hekaya za ajabu ajabu na ni watu wanaotake risk
Kililimanjaro kuna matatizo ya udini na ukabila tofauti na Tabora hawana udini wala ukabila. Ukitaka kuhakikosha hill angali jimbo la ubungo na kibamba tangu enzi za kina lamwai na zaidi ya hapo
 
Mkuu hapa naona tatizo haliko kwa wapiga kura, ila kwa mgombeaji ama chama chake.
Tatizo muda mwingine linaweza kuwa mgombeaji ama chama wamemchoka/wamekichoka.Mfano mzuri mgombea wa ccm mtwara mjini aliambiwa ukitaka tukupe kura ingia Cuf japo tunajua umetufanyia mambo mazuri ila chama chako hatukitaki akakaidi akapata alichokitaka..kilichomsaidia mbunge wa cuf ni kuteka hisia za wananchi kwa wakiwa bado wanauchungu na chama cha mapinduzi baada ya kuwatenda kipindi cha sekeseke la gesi
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Kililimanjaro kuna matatizo ya udini na ukabila tofauti na Tabora hawana udini wala ukabila. Ukitaka kuhakikosha hill angali jimbo la ubungo na kibamba tangu enzi za kina lamwai na zaidi ya hapo
Kwa hiyo unamaansha hao wa CCM wanaogombea wanakuwa waisilamu au wanakuwa sio wachaga ndio maana wananshindwa?
Basil Mramba hakuwa mchaga na akashindwa mwaka 2010 Rombo? Salakana hakuwa mchaga na kushindwa mwaka 2010 Moshi mjini? Davis Mosha nae hakuwa mchaga? Agrey Mwanry nae hakuwa mchaga akashindwa Siha? Hao walioshindwa mwaka huu walikuwa waisilamu au sio wachaga?
 
Nadhani elimu na exposure ya watu wa mkoa husika pia inahusika, Tabora watu wake ukilinganisha na Kilimanjaro (no offense) Kilimanjaro ni watu wasioaminishwa hekaya za ajabu ajabu na ni watu wanaotake risk

Ili isiwe offensive, naomba mambo haya: una maanisha nini unaposema 'elimu', 'exposure' na 'risk? Halafu tupe mifano walau miwili yenye scientific empirical evidence kwa 'elimu', 'exposure', na 'risk' kwa kila kipindi ndani ya vipindi vya pre-colonial, colonial, and post colonial. Halafu 'hekaya za ajabu ajabu ndio zinakuwaje?

Pia siamini kama Kilimanjaro hakuna watu wa makabila wengine wanaoishi huko na Tabora pia.
 
This is offensive unless it is backed up with scientific empirical evidence.
Very simple try to review different leaders of Public and private sectors in Tanzania as well as view different names of student who join different University and colleges, the same applied modern and good school. I'm not from Kilimanjaro but Inspire them
 
Back
Top Bottom