Siasa za Nape Nnauye ndani CCM zimefika Ukingoni. Je, ACT-Wazalendo Wakimkataa atafanya kazi gani?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Nape Nnauye aliwahi kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano, aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli kabla ya kutenguliwa Uteuzi wake 23 March 2017 na nafasi yake kuchukuliwa na Dr. Mwakyembe. Nape pia alikuwa mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi ambapo anagombea tena.

Nape alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.

Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara. Mzee Nnauye ni mmoja kati ya wanasiasa mashuhuri wa kizazi kinachoondoka, kazi yake ya kwanza ilikuwa ni “ukuli” wa bandari ya Lindi na Mtwara. Baadaye alisoma kidogo na kushiriki kwenye harakati za kudai uhuru akiwa kijana mdogo na baada ya Uhuru alikuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Tanu.

Ukiachilia mbali kulitumikia jeshi kuanzia “ukuruta” hadi kuwa Brigedia Jenerali, kuongoza vita ya Uganda kama mwanajeshi , lakini pia kama waziri mdogo wa Ulinzi, pia Nauye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, mkuu wa mkoa wa Singida, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Naibu Waziri wa Ulinzi na Mshauri wa Rais Mkapa.

Nape alianza elimu ya msingi huko mkoani Singida mwaka 1987-1989 katika shule ya Mwanga iliyopo wilaya ya Iramba (darasa la kwanza hadi la tatu). Alihamia mkoani Mwanza na kuendelea na elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Bukumbi iliyoko wilaya ya Misungwi kati ya mwaka 1989 hadi 1993 alipohitimu darasa la saba. Nape ni kati ya wanafunzi watatu waliofanya vizuri kwenye shule hii, alichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari.

Kati ya mwaka 1994 hadi 1997 Nape alisoma na kuhitimu kidato cha nne katika shule mbili za sekondari. Alisoma kidato cha kwanza na cha pili mwaka 1994 - 1995 katika shule ya Sekondari ya kutwa ya Ngudu iliyoko wilayani Kwimba na baadaye akamalizia kidato cha pili na kuendelea na kidato cha tatu na nne kati ya mwaka 1995 hadi 1997 katika shule ya Bweni ya Sekondari ya Nsumba iliyoko Mwanza ambako alihitimu elimu ya Sekondari.

Nape aliendelea na elimu ya juu ya sekondari kwa kujiunga na mchepuo wa EGM (Uchumi, Jiografia na Hesabu) katika Chuo cha Ualimu Butimba, alisoma kuanzia mwaka 1998 na kuhitimu mwaka 2000.

Kati ya mwaka 2000 hadi 2002 alianza elimu ya juu kwa kusoma Stashahada ya Sayansi ya Jamii katika Chuo cha Sayansi ya Jamii Kivukoni, alihitimu na kutunukiwa stashahada hiyo mwaka 2002 akibobea katika masuala ya Sosholojia, Fiziolojia na Siasa.

Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.


Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.

Nape amekaa na kuongoza kitengo cha Habari na Uenezi cha CCM ngazi ya taifa kwa miaka kadhaa katika kipindi ambacho CCM imepita kwenye wakati mgumu kisiasa. Kitengo alichokiongoza kitaalamu na ndani ya vyama hujulikana kama “kitengo cha propaganda” hata kama wahusika hawawezi kupenda jina hili.

Matarajio ya Nape ni kuweka matamanio yake katika vitendo. Miaka kadhaa iliyopita yeye amekuwa mmoja wa watu walioamini kwamba Serikali ya CCM imekuwa ikiyumba kwa sababu ya kuwa na “mawaziri mizigo” wanaoshindwa kusimamia mambo muhimu mengi ambayo kimamlaka yako chini yao

Katika eneo la habari kuna mambo kama manne ambayo ni changamoto kubwa. Kwanza kuna Muswada wa Vyombo vya Habari ambao sheria yake inalalamikiwa sana.

Jambo la pili ni sheria kandamizi zinazopokonya uhuru wa watu kupashana habari au kutoa habari, sheria hizi ziko nyingi na zimetengenezwa kwa namna ambayo inaiweka Serikali juu ya uhuru huo. Sheria zingine zimekuwapo kwa muda mrefu lakini ya hivi karibuni, (Sheria ya Uhalifu wa Mitandao) ndiyo inatumiwa kama rejea halisi kuthibitisha kuwa Tanzania inaingia kwenye mtego wa kuweka haki za kupashana habari hatarini. Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Milenia (MCC) imesitisha msaada wa zaidi ya shilingi trilioni moja za Tanzania sababu mojawapo ikiwa Tanzania kupitisha na kutumia sheria hiyo.

Jambo la tatu ambalo linabaki kuwa changamoto ya kudumu ni “kutumika vibaya kwa televisheni ya taifa”, televisheni hiyo ambayo inajiendesha kwa kodi za wananchi imeacha kuwa ya taifa na kufanya kazi kama chombo cha propaganda za chama kinachoongoza dola, jambo hilo linamuumiza kila mwananchi anayetambua wajibu wa vyombo vya habari vya taifa kwa wananchi wake.

Shirika la Utangazaji la Taifa halijaishia hapo tu, limekwenda mbali zaidi na hivi sasa linaweza kuthubutu kuahirisha vipindi muhimu kama taarifa ya habari ili kurusha moja kwa moja matangazo ya harusi za watu binafsi. Watanzania wanataka kuona shirika hili linahudumia taifa, vyama vyote vya siasa na wadau wote kwa usawa kabisa na mwenye jukumu la kurejesha nidhamu hiyo ni Nape alishindwa.

Changamoto ya tatu kwenye habari ni maslahi ya waandishi wa habari. Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa waandishi wengi wa habari kwamba baadhi ya vyombo vilivyowaajiri haviwapi mikataba wala malipo mazuri, havizingatii sheria za ajira kwa kuwapa wataalam hawa malipo ya kazi za ziada, likizo na motisha.

Waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye vyombo vya namna hii wamegeuka kuwa watumwa, ombaomba na watu wanaotegemea kulipwa Sh10,000 au Sh20,000 na wadau wakubwa wanaotaka habari zao zitangazwe. Matokeo ya jambo hili ni kuwapo kwa upendeleo wa habari kati ya wale wanaotoa “posho” na wale wasio na uwezo wa kutoa posho. Nape alihitaji mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu kupambana na hali hii. Alishindwa.

Baada ya Utangulizi huo, sasa turusi kwenye mada nitetee Point yangu kwanini Nape hana Uhakika wa Kurudi.

1. CCM wanabebana, kwa sasa hana mtu wa kumtetea ndani ya CCM. Wote waliokuwa wanamtetea hawana nguvu.

2. Nape alikuwa anatembelea Nyota ya Baba yake aliyekuwa Kiongozi wa serikali kipindi cha Mkapa, na Mkapa alimbeba Nape kama kulipa fadhira kwa Baba yake aliyefanya naye kazi kipindi kirefu. Sasa Mkapa kashafariki nani atamtetea?

3. Mwaka 2008 Nape Nauye alifukuzwa CCM na UVCCM na Kuvuliwa vyeo vyake vyote. Kauli hiyo ni kinyume mapendekezo ya Baraza Kuu la UVCCM lililotaka mwanasiasa huyo avuliwe nyadhifa zake zote. Baadaye Rais Kikwete, akitoa taarifa fupi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), alisema chama hicho tawala kitaendelea kumtambua Nape kama mjumbe wake, mwanachama na kutambua nyadhifa zake zote ndani ya CCM.Kauli hiyoilikuwa kinyume mapendekezo ya Baraza Kuu la UVCCM lililotaka mwanasiasa huyo avuliwe nyadhifa zake zote na kufukuzwa.
Naibu Katibu Mkuu wa UV-CCM Asimamishwa!

4. Nape Nnauye ni mmoja ya watu wanaodaiwa kutokubaliana na rais Magufuli kupita bila kupingwa katika katika Mchakato wa Kugombea Urais ndani ya CCM. Alikuwa team Membe.

5. Rais Magufuli hakubaliana na Utendaji wa Nape Nnauye ndo maana hata CCM walikaa kimya alipotishiwa kwa bastola dakika chache baada ya kuvuliwa Uwaziri. Hata Polisi walikaa kimya japo walikuwepo wakati wa tukio, hadi leo hawajamkamata aliyetaka kumuua kwa bastola japo anafahamika. Polisi hawakuona haja ya kutumia picha iliyokuwa inasambaa mitandaoni ili kumkamata. Hata angekufa hakuna ambaye angemlilia Nape ndani ya CCM.

Polisi: Yeyote mwenye taarifa za uhakika za aliyemlenga Nape kwa bastola atujulishe

5. Sauti ya Nape ilivuja akimnanga rais Magufuli kwa maneno ambayo hayaelezi wala hayawezi kusameheka kirahisi. Baadaye aliomba Msamaha, na siku alipoenda ikulu kuomba msamaha, Watendaji wa Ikulu walisambaza picha za kumdhalilisha. Sasa hivi anatumika kisiasa tu.

Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM

Ngetti: Nape ulichokifanya ni aibu ya maslahi sio msamaha, na jimbo la Mtama sio lako tafuta chama kingine hilo lishapangwa kitambo

Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

6. Nape anapata ajali mara kwa mara za gari ambazo yeye anadai zinatengenezwa ila Mungu bado anamlinda. Je, nani anazitengeneza?

7. Nape anajiona yeye ndo ameifikisha CCM hapo ilipo, Magufuli amekutwa kashatafuniwa alichofanya ni kumeza tu. Wengine wakifukuzwa na Rais Magufuli wanashukuru lakini yeye aliumia kiasi kwamba akaanza kumnanga rais. Na bifu likazidi kukua. Hapa chini naweka Nukuu alizoongea baada ya kutumbuliwa.

Nataka aliyeinua bastola hapa aje aseme ameiinua kwa sababu gani" - Nape Nnauye

"Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia."- Nape

"We have nothing to fear, but fear itself."- Nape

"Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola. Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo. Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa."- Nape

"Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka. Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?"- Nape

"Vijana naomba msimamie haki yenu"- Mbunge Nape Nnauye

"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape

"Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke."-Nape.

8. Nape hivi karibuni alionesha dharau kwa Viongozi wake wa juu wanaotaka Uchaguzi huru na haki na kutunzwa kwa amani. Akiongea kwenye mkutano wa Waziri mkuu alisema: Najua ntapitishwa kugombea Ubunge. Nikipitishwa, sitaki mtuingilie, hayo mambo ya amani ni kwenu nyie viongozi wa kitaifa, huku chini tuacheni tuwavunje Miguu. Wakituchokoza tutawavunja Miguu.

Uchaguzi 2020 - Nape Nnauye, Uropokaji wako unakuponza sana. Aahidi kupiga watu Mabuti

9. Kipindi cha Mgogoro wa Korosho, Nape alijifanya hataki kumuunga mkono rais Magufuli akadai yupo upande wa Wapiga kura. Kwamba ndo waliompeleka Bungeni si mwingine. Sasa WENYE CCM YAO wanataka wamuoshe kwamba hao wapiga kura wake si chochote si lolote mbele ya Mwenyekiti wa chama, jina linakatwa na hakuna kugombea chama Pinzani kwani CCM wakitangaza majina tayari muda wa kuchukua fomu utakua umeaisha. Huwezi kuhama chama labda aendelee na Maongezi Mapema na ACT Wazalendo kama inavyosemwa ili akikatwa kesho yake akachukue fomu upande wa Pili.

10. Nape anaonekana bado analeta jeuli kwa mwenyekiti wa Chama baada ya kusema hata akikatwa haogopi kwani yeye ni Msomi. History yake ya Elimu nimeweka hapo juu. Nape Nnauye amesema haogopi jina lake kukatwa kwa sababu amesoma vizuri na ana elimu ya uhakika.
Nape: Hata kama jina langu litakatwa sitakufa njaa kwa sababu nina elimu ya uhakika

Kwa haya Machache naomba kumtakia kila la heri Nape Nauye huko Mtaani. Safari hii hatoboi na ndo utakuwa mwisho wa siasa zake ndani ya CCM ila sio mwisho wa maisha kwani maisha hupanga Mungu.

Sioni dalili ya Nape jina kurudi. Wale wazee wakipiga kura hapenyi. Inabidi Kikwete ashupaze mshipa kumtetea Nape jina lirudi. Je, Kikwete peke yake ataweza kumbeba Nape?
 
Ili kuwasaidia wengine kama mimi ambao muda ni jambo muhimu na kuepuka kusoma story nyingi naomba unijibu hapa kwanini unadhani siasa zake zimefikia ukingoni ? (kama hautojali..., the least the maneno..., the better....
 
Kwa hyo mkuu huyu mwamba elimu yake mwisho stashahada ya chuo cha CCM

Yeye katika Twitter yake katuambia ni msomi mzuri hebu fukunyua fukinyua mkuu upate details zaid za elimu yake
 
Mbona mnahofu sana kwamba atakatwa si aliongoza kura za maoni halafu rekodi yake ndani ya ccm imetukuka akikatwa labda iwe chuki binafsi lakini vinginevyo anastahili kuendelea kugombea ubunge wa jimbo la Mtama.
 
Kuhusu elimu yake naona mmepotosha kwa manufaa yenu.

  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa –Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe.
 
Hawatamkata huyo, kwa moto wanaouwasha upinzani JPM hana jeuri ya kuleta makundi ndani ya chama, atalazika kuwakusanya wote hata ambao hawapendi.
 
Nape huyuhuyu alieomba kibali cha kupiga watu mabuti toka wa Waziri mkuu au kuna nape mwingine?
 
Sasa mkimkata Nape mnamuweka nani? Hapo mtama , siasa azitabiriki hata magufuli anawezwa kurudi chato , sisi wajumbe we tuone hivi hivi.
 
Kwa haya Machache naomba kumtakia kila la heri Nape Nauye huko Mtaani. Safari hii hatoboi na ndo utakuwa mwisho wa siasa zake ndani ya CCM ila sio mwisho wa maisha kwani maisha hupanga Mungu.

Sioni dalili ya Nape jina kurudi. Wale wazee wakipiga kura hapenyi. Inabidi Kikwete ashupaze mshipa kumtetea Nape jina lirudi. Je, Kikwete peke yake ataweza kumbeba Nape? umemchambua zaidi ya karanga
 
Ili kuwasaidia wengine kama mimi ambao muda ni jambo muhimu na kuepuka kusoma story nyingi naomba unijibu hapa kwanini unadhani siasa zake zimefikia ukingoni ? (kama hautojali..., the least the maneno..., the better....
Kwa haya Machache naomba kumtakia kila la heri Nape Nauye huko Mtaani. Safari hii hatoboi na ndo utakuwa mwisho wa siasa zake ndani ya CCM ila sio mwisho wa maisha kwani maisha hupanga Mungu.

Sioni dalili ya Nape jina kurudi. Wale wazee wakipiga kura hapenyi. Inabidi Kikwete ashupaze mshipa kumtetea Nape jina lirudi. Je, Kikwete peke yake ataweza kumbeba Nape?
 
Atatemelea magoti tena kwenda Ikulu,Safari hii itakuwa chamwino Dodoma
 
Back
Top Bottom