Kikwete azuliwa jambo Mbeya
* Mulla asema ni kukaribisha laana ya Mungu
* Akemea tabia ya wanaoendekeza majungu
* Aorodhesha mafanikio lukuki ya mkoa huo
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoani Mbeya, Bw. Nawab Mulla amesema wanadai kwamba Rais Jakaya Kikwete haupendi mkoa huo wamefilisika kiroho na kisiasa na kauli hizo zinakaribisha laana.
Bw. Mulla aliwataka watu hao kuona fahari na kuthamini uamuzi wa Rais Kikwete kuteua mawaziri kadhaa na mkuu wa mkoa, kutoka mkoa huu.
"Wana wa Israel walipozidi kumlaumu Mungu wakati amewapa chakula na neema tele alichukia na kuwapa adhabu ya kula mawe, sasa wana Mbeya nanyi mnataka nini Mungu awape zaidi ya upendeleo mliopewa na Rais wetu ?"Alihoji Bw. Mulla.
Akihutubia wananchi wa kijiji cha Mtakuja kata ya Utengule Usongwe katika kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Elimu kwa Watu Wazima cha Kanisa la Pentekoste Holiness Ministry ,Bw. Mulla alisema kuna watu mkoani hapa wamekuwa wakizuia viongozi wakuu wasije kutokana na maneno yao ya uongo.
Alisema watu hao wachochezi wamekuwa wakitoa maneno ya uongo huku baadhi wakidai kuwa Rais Kikwete haupendi mkoa wa Mbeya,jambo ambalo alisema ni upuuzi na kutafuta laana ya Mungu.
Bw.Mulla ambaye alichaguliwa kushika wadhifa huo kwenye uchaguzi Mkuu wa CCM uliomalizika hivi karibuni karibuni, alisema wakati huu si wa kuzungumza maneno ya uongo kwa ajili ya Mbeya bali kinachotakiwa ni kuzungumzia mshikamano wa dhati na kuijenga Mbeya upya.
"Kipindi kilichopita maneno yalikuwa mengi yenye kukera kwa sisi tunaopenda amani na ninawambia ndugu zangu yamefanya mkoa uonekane kama kisiwa kutokana na ukweli kuwa yaliyokuwa yanazungumzwa hayakuwa na ukweli kabisa na waliokuwa wanafanya hivyo ilikuwa ni kwa manufaa yao na si ya wana Mbeya,"alisema Bw. Mulla.
Akifafanua, alisema uthibitisho kwamba Mkoa wa Mbeya unapendwa na Rais Kikwete ni kitendo cha mkoa huo pekee kupewa Mkuu wa Mkoa wa ambaye ni mzaliwa wa hapo.
"Hii inaonesha ni kwa namna gani Rais ana imani kubwa na wasomi wa Mkoa wa Mbeya,"alisema Bw. Mulla.
Alisema mbali na Mkuu huyo wa Mkoa, Rais aliteua wabunge ambao ni Bw. Thomas Mwang'onda na Bi.Frorence Kyendesya ambaye aliteuliwa kuziba nafasi ya Dkt. Rose Migiro, mbali ya mawaziri wawili na naibu waziri mmoja.
Mbali na hao mkoa huo unajivunia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Magreth Sitta ambaye ni mzaliwa wa Mbeya na na Naibu Waziri wa Maji Bi.Shamsa Mwangunga ambaye ameolewa na Kyela ambapo alisema wote hao wanaonesha jinsi ambavyo Mbeya imepewa kipaumbele.
"Sasa ndio maana nawauliza kuwa ninyi wana Mbeya mnataka nini mnaposema, Rais hawapendi, mnataka hasira ya Mungu ishuke kisha awavue uongozi hawa aliotupa, ninyi mtapata nini? Watumieni vema viongozi hawa waliopo kwa ajili ya kuiunganisha Mbeya ninyi ndio kwanza mnasema mnatengwa na Rais acheni mambo hayo ! Alikemea Bw. Mulla.
Akionesha kukerwa na hali hiyo, alisema kama wakazi wa Mbeya watashindwa kumtumia Mkuu wao wa Mkoa ambaye wanayemfahamu hadi wazazi wake kuleta maendele, itakuwa ni hasara kubwa kwao.
Katika mkutano huo ambao ulikuwa ni wa kuchangia ujenzi wa jengo la kusomea na kulala yatima ,mwenyekiti huyo baada ya kusomewa risala na mahitaji aliahidi kupaua jengo hilo lote lenye vyumba zaidi ya 10 kwa gharama zake.
Alisema kinachotakiwa ni kwa wahusika hao kuhakikisha wanafikisha hatua fulani kisha kumpa taarifa ili afanye kazi hiyo ili watoto yatima na waliokosa elimu wapate nafasi ya masomo.
Source: Majira