Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,963
- 10,457
JF iko makini napata hapa DS 100 na DS 200 kilaini kabisa!!
Bila shaka hutakamatwa DS, hapa tumeshakupa desa murua kabisa. We copy na ku-paste tu.
Endelea kumkoma nyani!
Chukua tano!
JF iko makini napata hapa DS 100 na DS 200 kilaini kabisa!!
Mtanzania,
Maelezo yako hayo yanatosha kabisa, sasa naijua Mbeya vizuri. Hoja na dataz za watu kama wewe ndio zinatufanya wengine tuwe addicted na JF, ubarikiwe sana! Umenisaidia pia ku-confirm yale niliyokuwa nayajua kuhusu Dk wetu Mwakyembe. Haya mimi yalinikuta wakati tunamfanyia kampeni za ubunge za EAC, wewe acha kabisa, huyu jamaa ni kiboko. Huwezi kumjua Mwakyembe kwa kumsoma kwenye magazeti hadi ukae naye ana kwa ana kwa muda.
Tena hupaswi kabisa kumchukulia Mwakyembe on a face value. Yeye huwa anakubali kutumiwa na kutumia akili zake kufanikisha matakwa ya kisiasa ya watu wengine. Unakumbuka Mkapa alivyomtumia kuhalalisha yale mauaji ya polisi kule Zanzibar, alijenga hoja kidogo watu wakubali, kilichosaidia kusambaratisha hoja zake ni hoja maridadi za prof Haroub Othman. Hivyo basi hata kwenye hii report ambayo tunamsifu sana huyu mheshimiwa, mimi ninajua kuna wajanja wachache waliamua kutumia akili zake ili kufanikisha ajenda zao kisiasa. Uzuri wa haya mambo ni kwamba ukweli siku zote hujitenga na uongo, sio muda mrefu tutajua zaidi kuhusu dhamira ya ndani kabisa ya ile report!
In the meantime, ukweli ni kwamba hii report imeinyanyua nyota ya kisiasa ya Dk Mwakyembe ambayo ilikuwa inazidi kufifia; sasa swali ni je, itadumu hadi lini? Time will tell.
Pundit,
Mwakyembe sio mtu wa JK. Ila JK huwa hasemi tu na wala haonyeshi kirahisi kama anamchukia mtu au la.
Mwakyembe alifanya kosa kama la Msekwa. Alienda kuwambia JK kwamba anataka kuacha bunge la EA ili akagombee Kyela. JK akasema sawa, Mwakyembe akachukulia kama ni green light wakati JK alikuwa na yake.
Ilipofika uwaziri, Mwakyembe akaachwa nje.
Mwakyembe ndiye alikuwa mpiga debe namba moja wa prof. Mwandosya kwahiyo
hakukuwa na uwezekano wa kuwa kitu kimoja na JK.
JK na Lowassa mtu wao kule Mbeya ni Mwakipesile. Pia Mwakipesile ndiye anaungwa mkono na vigogo wengi kutoka mkoa wa Mbeya. Mwakyembe anaungwa mkono na Prof. mwandosya.
Wakati mwingine inashangaza hapa jf. huu ni upuuzi, mwakyembe kwenda kumuomba jk agombee kyela!!!!?????
Then alipokubaliwa, baadaye anakuja msapoti mwandosya!! si maajabu haya!!
Takriban wabunge wote hugombea wakitaraji kuwa mawaziri, sio mwakyembe tu, na hii si kosa wala kitu cha ajabu, suala ni kuwatumikia watanzania.
Wakati mwingine tuache upotoshaji na kujifanya tunajua, kumbe wala mambo hayakuwa hivyo!!
Truevoter,
Kabla ya kukosoa wengine angalia facts zako.
Mwakyembe alimuunga mkono prof. Mwandosya kwenye mchakato wa urais kwa CCM ambao ulimalizika mwezi may 2005. Kikwete aliibuka mshindi wa uchaguzi huo.
Dr. Mwakyembe aliamua kugombea ubunge mwezi wa sita/saba na ndio wakati alipomwona JK. Wakati huo JK alikuwa tayari ni mgombea wa CCM na makundi yote yaliungana kumuunga mkono.
Kama ni upuzi sio lazima umeze au usome, wanaotaka kujua watasikia na kujifunza. Nilichoandika hapo juu nina uhakika nacho kwa asilimia 100.
Kama una facts tofauti andika hapa na wananchi watajua nani anasema ukweli na nani anakuja kusagia bila facts, hiyo ndiyo sifa ya JF mkuu.
Mtanzania.
You can connect political events in any form u want to make it bring the interpretation u need!
Lkn mwakyembe amekuwa mbunge a.mashariki, je huko alitaka awe nani??
Mambo haya ya kusema ukweli hadharani mabaya yanapotokea mwakyembe hajaanza sasa!! he dd the same alipokuwa boardmember wa NBC BANK hadi pale alipojiuzuru mwenyewe!!
Kwa maana hy ccm achilia mbali kikwete wanaufahamu msimamo wake vzr!! hata michango yake mingi bungen inajulikana!!
Si kweli kabisa kw mwakyembe alimuomba jk akagombee kyela!!! statement za namna hiyo zinaonyesha dharau kwa wananchi wa kyela ambao ndio wenye vote ya kuchagua mbunge wamtakae.
Hakuna mtu anaomba kibali kwa mtu kwenda kugombea ubunge!! hz ni fikra potofu!!! na kupotosha ukweli wala haziwasaidii watu.
Mwakyembe hajamwuliza au kuomba kibali mtu yeyote kwenda kugombea ubunge kyela!! ni maamuzi yake binafsi.
Usitake watu waamini kwamba nchi hii kugombea nafasi ya uanasiasa hadi upewe idhin na watu fulani, si kweli, ni competence yako tu!!
Nafikiri ni propoganda tu, huyo kijana anaitwa steven Mwakajumilo yuko bot mbeya nathibitisha sio tishio kwa Prof. haya ni mambo yanayokuzwa kwa makusudi na wanamtandao.Kijana huyo hana ujasiri huo unaozungumziwa hapa na ajaribu avune aibu aliyovuna mwenzake Thom Mwang'onda.
Siasa za mbeya ndo zilivyo, ukabila ndo msingi mkuu, hata hivyo mmesahau kuwa mtanzania ni gazeti la fisadi rostam, mnategemema liandike lolote zuri kuhusu mwandosya?