Siasa na malaria Zanzibar

@Riwa
Mkuu heshima yako.
Tafadhali naheshimu mchango wako kama mtaalamu kw ajinsi inavyoonekana,
lakini nakuomba pia uheshimu na mchango wa wengine kama wagonjwa au waathirika wa hili.

Mimi kama mfano halisi kwa sasa kiukweli kabisa Kipimo hiko hakigundui malaria mahospitalini, sasa sijihu ni kwa badhi ya watu au la, ila kwenye familia yangu sijawahi kupeleka mke wala mtoto akawa Postive, kinachofanyika ni ubishi kwenda kununua dawa ya malaria kwa sabbau symptoms tunazijua na zinajulikana, na punde tunapotumia dawa tunapona.

Please narudia tena heshimu maoni yetu kama watumiaji, UNLESS UTUAMBIE UNAMASLAHI NA HIKI KIPIMO, swala la hiki kipimo kusambzwa nchi nzima sio hoja ya maana wala yenye mashiko, swala la kutolewa kwa KLOROQUINE pia sio hoja yenye maana , ukweli ni kuwa Klorokwini huku kwetui tulikuwa bao tunapona vizuri tu na hakuna dawa iliyotutesa kama hizo SP na ALU.

kwa nchi hii UFUSADI ulivyo siwezi shangaa kuwa hiki kipimo ni magumash, kwa maana hakifanyi kazi au ni feki hivi vilivyopo huku hospitalini kwetu.
 
Back
Top Bottom