Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
Wapendwa Salamu,
Hatimaye nimerejea baada ya matibabu ya muda mrefu! KCMC na Agakhan Hospital. Nilipata FB kwenye koromeo. Usijesema ni Face Book ni Foreign Body! Loh!
Back to issue! Mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi unaingia kwenye dosari kubwa baada ya Mbunge Magumashi wa CHADEMA kuingilia mchakato na kutaka shoga aka rafiki yake awe mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na kuwa Madiwani Wateule hawamtaki. Ikumbukwe kuwa uteuzi wa Mbunge wa Moshi Vijijini uligubikwa na utata mwingi. Hata baada ya Mteule wa Makao Makuu kupitishwa, madiwani wengi waliokuwa hawamuungi mkono waliamua kukibeba chama ili kisipate aibu. Katika uchaguzi huo madiwani walioshinda ni 15 kati ya 16 kwa maana ya CCM kupata kiti kimoja tu.
Mbunge wa sasa ameamua kumbeba kwa mbeleko kubwa rafiki yake anayesemekana aliwahi kugombea ubunge Kawe na Kinondoni na mara zote alishindwa kwa kuwa hakubaliki. Baadhi ya Madiwani wamepigiwa simu na mbunge huyo na kuwataka wamuunge mkono. Mpango unaosukwa ni kuwa jina la Mwenyekiti litateuliwa na kutolewa UAMUZI NA KAMATI KUU CHADEMA! Hii sio hali ya kawaida maana haijawahi kutokea! Madiwani wengi wanasema wako tayari kufukuzwa chama na sio kuburuzwa Mbunge na team yake ambayo ina tuhuma nyingi! Anayedaiwa kushirikiana naye zaidi ni kiongozi mmoja makao makuu ambaye amediriki kumteua mama yake kuwa Diwani wa Viti maalumu Jimbo la vunjo! Mbunge wa sasa anatuhumiwa kumteua Dada mmoja anayehusishwa naye kimapenzi!
ANGALIZO
Wabunge acheni kujiingiza kwenye michakato hii la sivyo mtaangamiza chama. CHADEMA sio mahali pa mama na wapenzi ni mahali pa kupambana! Ni harakati sio uswahiba! Kaeni chonjo! Mkitaka na majina tutaweka hapa!
Wasalaam